True story kumhusu ndugu yangu.

True story kumhusu ndugu yangu.

Si unaona hapo, nna uhakika huyo Mzee Karama , hapo Saudia alikuwa si kwao, nae alikuwa ni muhamiaji haramu.

Msaudi hususan mwenye asli ya Jiddah, hawezi kabisa kuhangaika, wao wana "system" ya "Umdah" ambae huyo mzee angekuwa ana asili ya hapo, lazima angemjuwa Umda wake na huyo Umdah asingekubali kabisa apate taabu.

Kati ya Watanzania nnao wajua wenye asili ya Jiddah ni kina Jidawi (wa Zanzibari), hawa ni ukoo maarufu sana Zanzibar na hakuna asiyewajua, ingawa wamechanganya damu "nadhani na wangazija" na watoto wengine wameolewa na kuoa makabila tofauti, lakini asili yao ni watu wa Jiddah na ndio maana wanaitwa "Jidawi". Hawa hata waende leo Ubalozini wakaoneshe roots za na family tree, basi watafanyiwa kila kitu chao kiwe sahali na watapokelewa kwa mikono miwili.

Nna uhakika Mzee Karama alikuwa ni illegal immigrant hapo Jeddah, Saudi Arabia.

Kama bado wapo Saudia na wanahitaji msaada wowote hapo, tafadhali ni PM ntakujulisha wafanye nini na waonane na nani.

FF nakushukuru kwa IQ yako pana ni kweli Mz Karama alikua si raia wa saudia alikua ametokea Yemen ya kusini, baadae nitakuPm kwa habari zaidi.
 
kwani inaruhusiwa kuingia jela na vipuri sio unaandikisha ndo unaviacha ili ukitoka upewe?

Hakufungwa jela huyo, alikuwa ni kwenye kituo cha deportation. Ambacho wanawekwa "illegal immigrants" wakingoja kusafirishwa, hapo hata kula kuna Restaurant, kama una hela yako, unakula unavyopenda, unavaa unavyopenda unangoja safari. Kama una nauli na passport basi hukai kabisa, unasafirishwa.
 
unamalizia lini nina hamu ya kukipata kisa kamili

Muda si mrefu dada yangu wa imani nitaimalizia kuna gari naitengeneza ndy inalambia muda, mara nimeshika spana mara simu, but NAWAOMBA MNIAMINI HII SI INSHU (ISSUE) YA KUBUNI.
NI TRUE STORY NA JINA LA MZ. KARAMA NI JINA HALISI NA YALIOBAKI NDY MAJINA MIDOSHO.
 
Anytime, nimeishi sana nchi za Kiarabu, karibu zile nchi za Gulf zote, kuanzia Yemen, Oman, Saudia, Kuwait, UAE, Qatar, Bahrain na zingine nimezitembea sana. Gozi lilikuwa "consultant" la mambo ya telecommunications huko, kwa hiyo alikuwa ana hamahama sana hizo nchi kutokana na shughuli zake, na mimi karibu hizo nchi zote nimefanya kazi, zingine part time zingine full time.

Hapo Jeddah anapopasema nilishawahi kuwa "part time" mkalimani wa hizo sehemu za kusafirishia "illegal immigrants" kwa hiyo kwa kesi kama yake nnaijuwa sana.

okay thanx n big up mamie.
 
Back
Top Bottom