Tujiandae kuishi kama mashetanani kwa kulazimisha hata visivyowezekana.
Salary Slip;
Naomba nitofautiane na wewe kwa hili.
Nadhani hapa ishu si kutowezekana. Kila kitu kinawezekana kabisa
Tatizo ninaloliona mimi ni kutamka kwa hisia tu kuwa serikali itafanya hivi au vile bila kuonesha ni kwa namna gani
Chukulia mfano ishu hii ya treni ya umeme ifikapo mwezi juni, 2017.
Kutamka tu si ishu na ofcoz kila mtu angependa kuliona hilo linafanyika hata kabla ya desemba, 2016 achilia mbali hadi hiyo juni 2017
Changamoto inayojitokeza na hata watu kutia mashaka ukiwemo wewe ni kipi kianze kwanza (setting priorities) kati ya umeme au treni yenyewe au zile ndege zingine moja ya kubeba abiria 160 na nyingine zaidi ya 240 au Tanzania ya viwanda
Mimi nasema hili kwa sbb mpaka sasa umeme bado ni shida ktk nchi yetu. Tuna umeme usio wa uhakika kwa 100% na hautoshi. Mimi siishi DSM, niko zangu Shinyanga.
Hebu tuelezane ukweli. Kuna siku inapita bila kukatika kwa umeme hata mara mbili hadi sita? Huku kwetu Shy ni kila siku na ilishakuwa ni "culture" na tumezoea, sina hakika huko DSM ambako wanatarajia kuletewa treni ya umeme unaokatikakatika ovyo ndani ya chini ya mwaka mmoja ujao!!
Sasa swali la kujiuliza ni kipi kianze kwanza? Uimarishe upatikanaji wa umeme kwanza au Tanzania ya Magufuli ya viwanda au madege makubwa ya Airbus??
Kingine ni muda. Tunaambiwa ni ndani ya mwaka mmoja tu yaani juni, 2017 treni za umeme na ndege zingine mbili kubwa za kupaa kutoka DSM hadi New York - USA ama Beijing - China bila kutua popote zilete watalii. Kwa hiyo tunajiuliza hii mipango ni realistic kweli au ni hisia za mwendokasi wa kilevi tu?
Naweza kuhitimisha kwa kusema hivi;
Kuwa na mipango ya kupata hiki au kile ni jambo moja lakini kupata kitu hicho ni jambo jingine kabisa!
Ndo kusema tunayo mikakati na njia halisia za kupitia ili kukiendea tunachokitaka au ni ndoto za mchana tu hizi?
Hili halina tofauti na lile tamko la kimwendokasi la mtakatifu sana na watakatifu wadogo wadogo kudaka na kuigiliza kama ndege kasuku la "ifikapo septemba, 2016 serikali itakuwa imehamia Dodoma!!"....
Lakini mwisho wa siku waka retreat na kumeza matapishi yao wenyewe walipoingia ktk utekelezaji na kuona kumbe hii ni "mipango hewa" na badae wakaja na rekebisho kuwa sasa itakuwa ni hadi 2020!!