Treni ya umeme inakuja July 2017

Treni ya umeme inakuja July 2017

Kila kitu kinawezekana, watanzania bado wana ile dhana waliyojengewa tangu awali kuwa Tanzania ni maskini, na hakuna linalowezekana nchini...

Kwa hiyo kwa sasa ndo serikali hii inawaambia kuwa kila kitu kinawekana, na wao hawaamini hadi waone...

Zile safari alizofanya JK. miaka 10 yake, Zaidi ya safari 400, pesa hizo zingefanya mambo makubwa sana chini
Hakuna anayekataa kuhusu hilo. Tena naamini usafiri wa treni ukiboeshwa unaweza hata kuleta tija kuliko wa anga. Kinachohojiwa ni huo muda uliotajwa. Kimsingi, mleta uzi anasema treni hiyo itaanza kufanya kazi ndani ya miezi 9 ijayo. Hiyo reli ya kisasa ambayo bado haijaanza kujengwa, anaweza kutuambia itaanza lini kujengwa na itachukua miezi mingapi kuikamilisha?
 
Tatizo hizo train za umeme zitapita ktk reli zipi? Ama wananunua na kuweka godown wasidanganye watu. Kila siku nasema hapa jf tuna ushabiki wa kinafiki hii habari kama ni ya kweli basi Magufuli yupo ktk nchi ya kufikirika. Hapa Manchester kishection kidogo cha tram kilianza mwaka 2013 mpaka leo hawajamaliza na umbali wake ni kama fire na magomeni itawezekana vipi ubungo mpaka mjini wamalize kwa miezi 10?
Barabara ya mwendo kasi tu imechukua muda kibao...
 
View attachment 408957

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imepanga kununua treni ya umeme inayotarajiwa kuwasilini nchini mwezi Juni, 2017.

Treni hiyo inatarajiwa kufanya safari katika jiji la Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema serikali inauwezo wa kutekeleza ahadi hiyo kwa kuwa fedha za kununulia treni hiyo zipo.

Pia Magufuli amesema serikali iko katika harakati za uboreshaji na ujenzi wa miundo mbinu ya usafiri, ikiweno ujenzi wa reli za kisasa kuanzia Dar es Salaam, Mwanza na nchi jirani ikiwemo ya Rwanda.
Vile vile serikali yake iko katika hatua za ujenzi wa daraja la kisasa litakalo anzia maeneo ya daraja la Sarenda litakalo pitia baharini.
Hadi sasa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu inaendelea nchi nzima ikiwemo mradi wa barabara za juu (Flyover) maeneo ya Tazara.

Aidha, Dk. Magufuli amesema serikali yake iko katika hatua za kutengeneza na kuboresha miji yake ili iwe ya kisasa.

hii ni movie sasa .....treni ya umeme wakati umeme wenyewe hauko sawa...mara unawaka na kuzima, mara siku nzima hakuna umeme, mara unapungua na kuongezeka...hiyo treni si itaua watu....
 
Sitaki kupinga ila kufanikisha hilo swala kwa hiyo timeline ni next to impossible, tutakuwa tunadanganyana tu

Hiyo tuu kwenda Dodoma iliyosemwa ni mwezi September nilikataa kuwa haiwezekani watu wakabisha...kilichotokea ni kuwa haiwezekani...Viongozi wetu wakisema kitu ni mwezi ujao we hesabia mwaka au miaka miwili ijayo
 
VIGELEGELEEEE!!!! VIGELEGELEEEEE!!!!! WATANZANIA VIGELEGELEEEEE!!! HII AWAMU YA TANO INA LADHA YA VANILA!!! VIGELEGELEEE!!!!
 
View attachment 408957

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imepanga kununua treni ya umeme inayotarajiwa kuwasilini nchini mwezi Juni, 2017.

Treni hiyo inatarajiwa kufanya safari katika jiji la Dar es Salaam. Rais Magufuli amesema serikali inauwezo wa kutekeleza ahadi hiyo kwa kuwa fedha za kununulia treni hiyo zipo.

Pia Rais Magufuli amesema serikali iko katika harakati za uboreshaji na ujenzi wa miundo mbinu ya usafiri, ikiweno ujenzi wa reli za kisasa kuanzia Dar es Salaam, Mwanza na nchi jirani ikiwemo ya Rwanda.

Vile vile serikali yake iko katika hatua za ujenzi wa daraja la kisasa litakalo anzia maeneo ya daraja la Sarenda litakalo pitia baharini.

Hadi sasa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu inaendelea nchi nzima ikiwemo mradi wa barabara za juu (Flyover) maeneo ya Tazara.

Aidha, Dk. Magufuli amesema serikali yake iko katika hatua za kutengeneza na kuboresha miji yake ili iwe ya kisasa.
Na umeme huu wa kukatika katika? Si itakuwa majanga?
 
Huwa ninafurahishwa sana na optimism ya JPM anapozungumzia miradi mikubwa "FEDHA IPO"- lakini ukichimbua kwenye bajeti ya serikali huoni hiyo helaimetengwa wizara gani na kwenye kifungu kipi?
 
Yangu macho, pengine ni ile tamthilia ambayo inaisha bila kufahamu hatma yake
 
Mwanzo mlisema JPM anafuata sera za upande wa pili, sasa hivi mnatakiwa kusikilizia tu kwani mtazidi kuumia bure!
 
Back
Top Bottom