Treni ya umeme inakuja July 2017

Treni ya umeme inakuja July 2017

Rebo Tz

Senior Member
Joined
Sep 26, 2016
Posts
169
Reaction score
125
1475149365354.jpg

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imepanga kununua treni ya umeme inayotarajiwa kuwasilini nchini mwezi Juni, 2017.

Treni hiyo inatarajiwa kufanya safari katika jiji la Dar es Salaam. Rais Magufuli amesema serikali inauwezo wa kutekeleza ahadi hiyo kwa kuwa fedha za kununulia treni hiyo zipo.

Pia Rais Magufuli amesema serikali iko katika harakati za uboreshaji na ujenzi wa miundo mbinu ya usafiri, ikiweno ujenzi wa reli za kisasa kuanzia Dar es Salaam, Mwanza na nchi jirani ikiwemo ya Rwanda.

Vile vile serikali yake iko katika hatua za ujenzi wa daraja la kisasa litakalo anzia maeneo ya daraja la Sarenda litakalo pitia baharini.

Hadi sasa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu inaendelea nchi nzima ikiwemo mradi wa barabara za juu (Flyover) maeneo ya Tazara.

Aidha, Dk. Magufuli amesema serikali yake iko katika hatua za kutengeneza na kuboresha miji yake ili iwe ya kisasa.
 
Kila kitu kinawezekana, watanzania bado wana ile dhana waliyojengewa tangu awali kuwa Tanzania ni maskini, na hakuna linalowezekana nchini...

Kwa hiyo kwa sasa ndo serikali hii inawaambia kuwa kila kitu kinawekana, na wao hawaamini hadi waone...

Zile safari alizofanya JK. miaka 10 yake, Zaidi ya safari 400, pesa hizo zingefanya mambo makubwa sana chini
 
View attachment 408957

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imepanga kununua treni ya umeme inayotarajiwa kuwasilini nchini mwezi Juni, 2017.

Treni hiyo inatarajiwa kufanya safari katika jiji la Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema serikali inauwezo wa kutekeleza ahadi hiyo kwa kuwa fedha za kununulia treni hiyo zipo.

Pia Magufuli amesema serikali iko katika harakati za uboreshaji na ujenzi wa miundo mbinu ya usafiri, ikiweno ujenzi wa reli za kisasa kuanzia Dar es Salaam, Mwanza na nchi jirani ikiwemo ya Rwanda.

Umeme upo wapi bana?

Hata likijengwa ni kwa ajili ya kujitangaza kisiasa tu si kutatua matatizo ya wananchi.

Amini usiamini, nimeomba niingiziwe umeme katika mashine ya kusaga. Kila kitu kimeshapita na nimeshalipia, leo hii ni mwezi wa pili sijaingiziwa umeme, kisa eti waya za 3 phase hazipo. Naendelea kusubiri. Pazuri hapo!!!!!!!!
 
Treni ya Umeme inakuja July Mwakani, kulingana na maelezo yako
Reli ya kisasa itaanza kujengwa lini na itakamilika lini?
 
Umeme upo wapi bana?

Hata likijengwa ni kwa ajili ya kujitangaza kisiasa tu si kutatua matatizo ya wananchi.

Amini usiamini, nimeomba niingiziwe umeme katika mashine ya kusaga. Kila kitu kimeshapita na nimeshalipia, leo hii ni mwezi wa pili sijaingiziwa umeme, kisa eti waya za 3 phase hazipo. Naendelea kusubiri. Pazuri hapo!!!!!!!!
Ahaha hapo wanataka pesa uwapoze kwanza
 
Kila kitu kinawezekana, watanzania bado wana ile dhana waliyojengewa tangu awali kuwa Tanzania ni maskini, na hakuna linalowezekana nchini...

Kwa hiyo kwa sasa ndo serikali hii inawaambia kuwa kila kitu kinawekana, na wao hawaamini hadi waone...

Zile safari alizofanya JK. miaka 10 yake, Zaidi ya safari 400, pesa hizo zingefanya mambo makubwa sana chini
Tatizo hizo train za umeme zitapita ktk reli zipi? Ama wananunua na kuweka godown wasidanganye watu. Kila siku nasema hapa jf tuna ushabiki wa kinafiki hii habari kama ni ya kweli basi Magufuli yupo ktk nchi ya kufikirika. Hapa Manchester kishection kidogo cha tram kilianza mwaka 2013 mpaka leo hawajamaliza na umbali wake ni kama fire na magomeni itawezekana vipi ubungo mpaka mjini wamalize kwa miezi 10?
 
Kiukweli watanzania wamejiwekea dhana ya kuongopewa kwahiyo hata wakisikia kitu hawaamini mpaka wakiona kitu kimetekelezwa
Wakiamua kutoajiri wala kuboresha huduma za jamii na mambo mengine na hela zote wakaelekeza huko,baadhi ya mambo watafanikiwa ila wajue tu wakiumiza watu 2020 itakula kwao.
 
Back
Top Bottom