Sumbalawinyo
JF-Expert Member
- Sep 22, 2009
- 1,282
- 247
Na Mwandishi Wetu
Taarifa zilizotufikia sasa hivi zinaeleza kuwa, basi moja la abiria (daladala) ambalo namba zake hazikuweza kupatikana mara moja, limegonga treni na kwamba mtu mmoja (mwanaume) amefariki dunia.
Ajali hiyo imetokea eneo la Davis Corner, Tandika Yombo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kufafanua kuwa watu 26 wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Temeke kwa matibabu!