Bahi, Dodoma: Treni iliyokuwa ikitoka Dar kuelekea bara imepata ajali. Majeruhi na vifo vyaripotiwa

Abby Newton

JF-Expert Member
Nov 12, 2017
656
1,000
Nimepigiwa simu na mpwa wangu ambaye ni miongoni mwa abiria walionusurikana, kuwa treni iliyokuwa ikitoka Dar - Kigoma imepata ajali kilometa chache kutoka stesheni ya Dodoma.

Inasemekana watu kadhaa wamejeruhiwa na inadaiwa watu 3 wamepoteza maisha.

Naomba wahusika wafuatilie.

======
UPDATES:

10:05pm

Ajali ya treni iliyokuwa inatokea Dar kwenda Bara imetokea muda wa saa moja kasoro, Maeneo ya Zuzu Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Kati na Itiga. Taarifa za awali ni kwamba watu 25 wamejeruhiwa. Vifo hadi sasa ni Vitatu ambavyo ni Mfanyakazi mmoja wa treni na abiria wawili.

Shirika la reli limepeleka Mabasi kubeba abiria na Majeruhi na Wanapelekwa Dodoma kupata huduma ya kwanza hospitali ya General.

Abiria wote wanapelekwa Manyoni sababu kuna Treni ya abiria saa sita inatokea bara. Kwasababu haiwezi kupita sehemu ya ajali, abiria watapanda hiyo Treni iliyokuwa ikitoka bara kwenda Dar. Itageuzia manyoni na abiria Waliokuwa wanaenda Dar watapanda mabasi ambayo yamekwisha andaliwa.

Mvua imenyesha sana, kuna uwezekano kuna makalavati yamekatika.

Ajali ilipotokea ni Km 40 kutoka Dodoma.

Taarifa zaidi zinafuata.

Zaidi, soma:


PICHA:

418DE065-8533-429C-9A8E-296367A2CC00.jpeg
4703E327-7FA6-490D-905C-71401420354B.jpeg
E29A1EF6-C278-4E52-8C12-C771AF904EAC.jpeg

EFECB064-7A15-4A21-B851-25CC9466C6CD.jpeg
F17BB55B-87C8-4D6C-8EE6-9E46705BF602.jpeg
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,645
2,000
Nimepigiwa simu na mpwa wangu ambaye ni miongoni mwa abiria walionusurikana, kuwa treni iliyokuwa ikitoka Dar - Kigoma imepata ajali kilometa chache kutoka stesheni ya Dodoma. Inasemekana watu kadhaa wamejeruhiwa japo hakuna taarifa rasmi ya vifo. Naomba wahusika wafuatilie.
Haina muda wala siku! Je, umewajulisha trafiki na faya?
 

Stephen Chelu

Verified Member
Oct 31, 2017
5,402
2,000
Ngoja tusubiri taarifa rasmi, ila hata mimi nimesikia taarifa hiyo dakika chache zilizopita.
 

Mapico

JF-Expert Member
Apr 17, 2019
458
1,000
Poleni sana kwa waliofikwa na majanga haya .
msimuhusishe Magu na hili chanzo yaweza kuwa uchakavu wa miundo mbinu au uharibifu wa njia za Reli kwa kuiba vyuma na nondo.

Mungu azilaze mahali zinapohusika roho za marehemu
 

KAWETELE

JF-Expert Member
Dec 11, 2015
529
1,000
Duuuh.. leo tarehe 2.

Hivi hii reli ya kati mbona Majanga saana ..... naona hii SGR ilipaswa kwenda huko..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom