Treni Lagonga Daladala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Treni Lagonga Daladala

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumbalawinyo, Feb 9, 2010.

 1. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Na Mwandishi Wetu

  Taarifa zilizotufikia sasa hivi zinaeleza kuwa, basi moja la abiria (daladala) ambalo namba zake hazikuweza kupatikana mara moja, limegonga treni na kwamba mtu mmoja (mwanaume) amefariki dunia.

  Ajali hiyo imetokea eneo la Davis Corner, Tandika Yombo jijini Dar es Salaam.

  Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kufafanua kuwa watu 26 wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Temeke kwa matibabu!
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,097
  Likes Received: 716
  Trophy Points: 280
  UDHAIFU WA SHERIA...!
  sheria ilisema inapotokea ajali itakayohusisha TRENI...inakuwa mtu,baiskeli, gari,daladala ndo limegonga treni....!
  hata kama mtu amekufa mtu huyo hustakiwa kwa kosa la kuigonga treni.....!
  I ONCE SAID.......THE LAW IS BLIND....!
  T542 ALR
   
 3. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mkuu rekebisha title ya thread....nijuavyo treni haligongi ila linagongwa! Pole zangu kwa wafiwa & Majeruhi
   
 4. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Niliwaambia juzi wakati nachangia hoja ya ajari ya Dar - Arusha iliyouwa watu zaidi ya 30 nikasema madereva wana upungufu wa akili - kama si hivyo basi ni uzembe wa kipumbafu.

  Mi nasema hawa madereva wanaosababisha ajali wasipokufa basi wawe kundi moja na wauwaji wa kutumia silaha. wafungwe maisha au miaka 30 na kazi ngumu.

  Jamaa linapewa ishara lisimame, yeye akaamua kuchomekea trein kama alivyozoea kuchomekea magari siku zote- jamani vifo vingine vya kujitakia hivi.
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 41,889
  Likes Received: 37,104
  Trophy Points: 280
  hiii ni athari ya kujua kwingi.
  Over speeding jumlisha bangi matokeo yake ndio haya.
   
 6. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  ha ha ha we umeona kwanza daladala lenyewe hapo break itoke wapi?
   
 7. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 655
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hivi hili gari ni la zege au bati mbona kama limevunjika?
   
 8. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kumbe humu ndani kuna watu wasio na busara, gari likikatika brake dereva ana kosa gani, kuna mtu anapenda kupata ajari, ktk ajari hii, unaambiwa pale hakuna alama yoyote na wala hakuna mshika kibendera kuashilia trane, na kila wakati ajari za magari na trane utokea pale pale.

  Hoja hapa ni hizi sheria zetu, haiwezekani mtu agonge trane, trane inapokuja bila kupiga honi na hakuna taa nyekundu kuashilia ujio wa trane, basi isomeke kuwa trane imegonga mtu, ila kama vyote hivyo vimefanyika iwe kinyume chake.
   
 9. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kila mara unapotoa thread kuwa makini na kichwa cha habari unachotumia ili kisiwachanganye wasomaji. Hii habari niliisoma jana kuwa daladala imegonga treni.

  Poleni wafiwa maana maisha haya siku hizi ukitoka nyumbani asubuhi na kurudi salama jioni ni kushukuru Mungu maana ajali za barabarani zinatisha kama sio kilema basi haupo kabisa, kila kuchicha afadhali ya jana. Wana Jamii Tumuombe sana Mungu kama FL1 alivyotushauri.

  Tutayaweza mambo yote katika Yeye atutiaye nguvu; na katika mambo yote tumkiri Yeye naye Atayanyoosha mapito yetu.
   
 10. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Wewe ushawahi kuendesha gari? Gari linakatika brake kwa sabubu zipi na kwa nini? na kwa nini likatike hizi brake ghafla? unajua njisi braking system ilivyo na invyofanya kazi? HUJUI na ndiyo maana unatetea uzembe wa hawa watu? jaribu kufikiria scenario ya ajali siyo ukukurupuke na hoja zako za brake.

  Hata kama hakuna alama yoyote lazima kama dereva uwe na caution, na kama kibao kinachokwambia eneo hili speed ni 60km/h hakipo wewe ukifika hapo unawenda tu speed 120km/h then unajiita dereva? na je yule dereva wa daladala hakujua kuwa pale kuna kivuko cha Reli?

  Ni sawa na mtu unaenda speed 120km/h anashindwa kukata kona then tyre ya mbele ndani upande wa kona ilipo inapasuka au gari inamshinda inapinduka anasema ni bahati mbaya - shame

  usitete ujinga - ningekuelewa ungeniambia gari lilikuwa bovu sana kiasi kwamba system zake nyingi hazifanyi kazi na ilikuwa makosa hata kuwa barabarani na ndiyo chanzo cha ajali - brake zitoke wapi ukiangalia hizo picha?

  Sheria za driving zinasema wazi kuendesha gari bovu pia ni kosa- tetea tena madereva wako.
   
 11. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  bwana wee, jamaa ananishambua eti brake zake zilikatika ndiyo maana akagonga train - duh
   
 12. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Naona wewe hujawahi hata kuendesha hata baiskeli, unapotaka kuvuka reli ni lazima uwe kwenye speed vingine uwe kwenye namba moja, bila hivyo gari linazimika, pia tumezoea kama kuna trane inakuja, ni lazima awepo mtu wa kuashilia hilo au taa nyekundu, kama vyote hivyo hakuna unalazimika kupita kasi, vinginevyo gari linazimika, ndio maana magari mengi ugongwa kwenye reli kwa sababu ya kupitisha magari yao slowly na hatimaye kuzimika,

  Hoja bado iko pale pale, TRL wana makosa na wao ndio wamegonga gari, sio gari limegonga trane, na mtoa hii thread yuko sahihi na heading yake maana ndivyo tukio lilivyotokea.
   
 13. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,824
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Sawa, Nimeshaliona gari lako lililogonga train -
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...