Tanga: Gari la Wanafunzi(Coaster) lagonga Treni, Mtu mmoja afariki, 19 wajeruhiwa

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
13,142
6,947
Kwa walioko jijini Tanga, watujuze kwa kiurefu kuhusu coaster ya wanafunzi iliyogonga treni maeneo ya Gofu.

Mtupe taarifa kwa urefu ikiwa ni za uhakika
====

maiyanga1, anasema;
"Ni kweli ajali imetokea, coaster iklikuwa imebeba wanafunzi wanaenda kwenye mpira shule ya Masechu, majeruhi wapo Bombo, hakukuwa na kifo eneo la tukio."

HABARI KAMILI
Mtu mmoja amefariki na wanafunzi 19 kati ya thelathini wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kwenda kucheza mpira kuligonga Treni eneo la Gofu jijini Tanga.

Kamanda wa polisi mkoani Tanga SACP Edward Bukombe amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

IMG-20190315-WA0002.jpg

IMG-20190315-WA0003.jpg
 
Mtu mmoja amefariki na wanafunzi 19 kati ya thelathini wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kwenda kucheza mpira kuligonga Treni eneo la Gofu jijini Tanga.

Kamanda wa polisi mkoani Tanga SACP Edward Bukombe amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
 
TRC acheni ulimbukeni, mnagonga magari ya raia kwa makusudi kisa sheria inawalinda, siku wananchi wakiwachoka na kuanza kuchoma moto hizo scrap metal sijui mtamlaumu nani, be responsible please!
Rail crossing hazina automated gates zinazofunga treni ikikaribia na kufungua treni ikishapita, hakuna taa kuzuia magari kwenye railway crossing, hata wale washika vibendera nao mmeshindwa? Wauwaji wakubwa!
 
Hizi ni sheria tumerithi toka kwa "mabeberu" na sisi tulivyo mazumbukuku tunaziendekeza. Ni kama tunavyohalalisha dereva wa mwendokasi kugonga bodaboda!
 
Mambo ya ajabu kabisa, hapa dar tu hakuna signal wala zile automated boom zinazofunga na kufungua treni inapokaribia, mambo ya ajabu sana, yani kama tuko enzi za ukoloni tu..

TRC wanalo la kutuambia kwanini tunajenga reli ya kisasa huku reli nyingine haina vitu muhimu, je hiyo sgr itadumu kweli au itakuwa kama miundombinu ya brt
 
Back
Top Bottom