Ajali, Dar: Watu 2 wajeruhiwa baada ya Lori lililobeba Soda kugongana na daladala maeneo ya Mabibo

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,408
2,000
Watu wawili wamejeruhiwa vibaya baada ya kutokea ajali iliyohusisha Lori lililokuwa limebeba soda, mali ya Kampuni ya Coca-Cola kugongana na basi la abiria (daladala) katika maeneo ya Mabibo Gereji jijini Dar es salaam asubuhi ya leo, jumatano Oktoba 2, 2019.

Taarifa zinaeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya breki kwenye lori hilo hivyo kusababisha dereva kushindwa kulimudu...!
IMG_20191002_090707_443.jpeg
IMG_20191002_090724_266.jpeg
IMG_20191002_090741_656.jpeg

******

Watu wawili wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea eneo la Ubungo Extenal baada ya gari ya kampuni ya Cocacola kuacha njia na kuigonga daladala aina ya Coaster iliyo na namba za usajili T 665 DLP.

Ajali hiyo imetokea leo asubuhi Oktoba 2, 2019 wakati gari hilo lililokuwa limebeba shehena ya soda likielekea Tabata huku daladala hiyo ikielekea Ubungo.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Juma Juma amesema kabla ya ajali hiyo kutokea, gari la Cocacola lilikuwa limeongozana na gari lingine la mizigo ambayo yote yalikuwa yakitokea Ubungo.

“Yalikuwa yakienda sambamba sasa walipofika katika eneo hili, aliyekuwa upande wa kushoto alihamia upande wa kulia ghafla, sasa dereva wa gari ya Cocacola ili kukwepa kumgonga alilazimika kupanda ukingo wa katikati ya barabara na gari lilihama hadi upande wa pili.”
“Ilipofika huko kwa bahati mbaya coaster iliyokuwa inapita iligongwa upande wa dereva akabanwa miguu pamoja na abiria mmoja,”

“wengine ndiyo hivyo kupata mishtuko lakini walitoka wazima. Waliokuwa wamebanwa walinasuliwa na kikosi cha uokoaji na kukimbizwa hospitali

Kwa upande wake Nassor Abdul amesema kama dereva wa lori angekuwa mwendo mkali ingekuwa ni ajali ambayo huenda ingetoa uhai wa watu wengi.

“Lile gari lina nguvu, lingeweza kuisukuma Costa na kuangukia katika mtaro mkubwa uliopo pembeni ya barabara huenda nalo lingeangukia juu yake unafikiri nini kingetokea ashukuriwe tu Mungu,” amesema Abdul

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ambaye pia alishuhudia wakati juhudi za kuwanasua watu hao zikifanyika pamoja na uondoaji wa magari hayo katika eneo la barabara alipopigiwa simu kuulizwa kuhusu tukio hilo alijibu kifupi “Niko kikaoni.”

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Mussa Taibu alipotafutwa, simu yake ilipokelewa na msaidizi wak huku akibainisha kuwa yupo kikaoni hadi saa 11 jioni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom