TRC yasitisha safari za treni kutoka Dar es Salaam Kwenda bara kutokana na mvua zinazoendelea

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa kuufahamisha umma juu ya kusitishwa kwa huduma ya usafiri wa treni ya abiria inayotoka Dar es Salaam kuelekea mikoa ya bara (Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Tabora, Mwanza, Mpanda na Kigoma) kuanzia tarehe 28.03.2023.

TRC imesitisha utoaji wa huduma kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali nchini na kupelekea daraja kusombwa na maji kati ya stesheni ya Godegode na Gulwe, wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

Huduma ya treni inatarajia kurejea siku ya Alhamisi tarehe 30.03.2023.

WhatsApp Image 2023-03-28 at 21.36.01.jpeg
 
Tunaangaika na treni hadi leo. Mvua kidogo treni haifanyi kazi. Radi kidogo tanesco wanazima umeme. Tungeamua kujenga njia 3 kwenda na 3 kurudi dar dodoma leo tungekua tunafurahia matunda

Jiji tu la Dar ikinyesha mvua linaanza kunuka mvundo.
 
Hata daraja la kwenye barabara pia linaweza kuzolewa na maji
 
Back
Top Bottom