TRC yasitisha huduma ya safari za treni mikoa 12

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
1705529925230.png

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa kuwa limesitisha kwa muda huduma ya safari za treni kutoka Dares Salaam kuelekea Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Katavi, Kigoma, Shinyanga na Mwanza, pamoja na Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha kutokana na uharibifu wa miundombinu ya reli katika maeneo ya Mazimbu, Kilosa na Munisagara Mkoani Morogoro, Godegode na Gulwe Mkoani Dodoma pamoja na maeneo ya Ruvu junction, Wami, Mvave Mkoani Pwani.

Pia eneo la Mkalamo Tanga kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.“Wahandisi kutoka TRC wanaendelea na matengenezo katika maeneo yaliyoathiriwa na mvua zinazoendelea na huduma ya usafiri wa treni zinatarajia kuanza siku ya Jumanne January 23, 2024 katika reli ya kati

Kuelekea Mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro a Arusha) inatarajiwa kuanza January 29, 2024 baada ya kukamilika uimarishaji wa miundombinu ya reli.

“TRC inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na inawasihi Wananchi kuwa wavumilivu katikakipindi cha matengenezo ili kuhakikisha usafiri unarejea katika hali ya usalama”
 
Per diems za ukarabati zinatengenezwa hapo
 
Back
Top Bottom