Trafiki "feki" akamatwa akila vichwa live

Trafiki "feki" akamatwa akila vichwa live

Tulidaganywa eti "maisha bora kwa kila Mtanzania" , sasa si lazima tujiboreshee maisha yetu sisi wenyewe kama risirikali rimeshindwa! Lol, jamaa ni mbunifu sana mie nimemkubali huyu sajenti feki! Jambo Afandeeee...... !
 
Wala mimi simsikitikii maisha bongo magumu sana!
 
Kuna trafiki mmoja sijui alifanya kosa gani vile! basi akatupwa kijiji cha ndani kinoma,huko zinaingia gari za mapadri tu tena kwa nadra.Basi akawa akiishiwa salio,anajisogeza iringa mjini bila mabosi wake kujua,anaanzisha kituo cha ghafla,anapiga hela then anarudi kijijini faster sana!
 
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar Es Salaam leo limefanikiwa kumkamata askari bandia akiwa amevaa Sare za Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamishina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP Suleiman Kova amesema leo majira ya saa moja na nusu asubuhi wamefanikiwa kumkamata James Hussen mwenye umri wa miaka 45 mkazi wa Kimara Tangi Bovu akiwa amevaa sare hizo huku akiendelea na utapeli wa kujifanya askari wa kitengo cha usalama barabarani.

Aidha Kamanda Kova ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi mara wanapomtilia mashaka askari yeyote na pia kuwaomba wananchi wasikubali kupigwa bao bali kuwataka askari kwenda nao kituo cha polisi pindi wanapokamatwa na makosa.

New+Picture+(2).png

Askari Bandia wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliyekamatwa leo mchana maeneo ya Kinyelezi Mnara, Tabata jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya sare zake mara baada ya kukamatwa. Askari huyu feki amefikishwa kwenye Kituo cha Polisi Stakishari ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa juu yake.

New+Picture.png

New+Picture+(5).png

New+Picture+(6).png
apo cjakupata apo!.
 
Hata mimi nimeipenda sana hii. Nasikia huyu bwana amevuta hela nzuri tu kwa njia hii na ana jumba la kifahari. Ni mbunifu mzuri na anajua ku-take advantage ya system ambayo sio organized. Hili ni funzo kwa taasisi zetu kujipanga au kwa lugha nyingine kuwa organized
 
Hahahahahahaha nimekusoma . Lkn huyu angeachiwa kwa sababu alikua anatafuta ridhiki yake tena alikua anasaidia usalama cha msingi wampeleke CCP moshi akaongeze maujuzi zaidi maana ameonyesha interest ya likazi hili.

Kwa ujumla nakubaliana na wewe kabisa. Wasimchukulie hatua huyu bwana ila wamuwezeshe. Badala ya kumchukulia hatua ni vizuri wao ndio wakajitathmini kwamba wamechemka wapi mpaka mtu akajiamini kuvaa magwanda na kufanya kazi ya kipolisi bila wasiwasi. Mimi nafundisha chuo kikuu, kama anaweza akaja mtu akajifanya mhadhiri na kufundisha na wanafunzi wamuogope kuliko sisi, inakuwa si busara kumchukulia hatua. Badala yake inabidi sisi wahadhiri tujitafakari kujua inakuwaje mtu aje afundishe na apate heshima zote kwa wanafunzi wakati tupo
 
Nadhani amejulikana kwa sababu ya vifungo vya shati lake, huwa vifungo vinakuwa vya silver yeye akazungushia kitambaa cheupe kama kaunda suti za zamani! Hapo lazima wazaee naye...na zile hela alizokusanya kwa siku hiyo zinachukuliwa kabla ya kufikishwa kituoni
 
Kwa ujumla nakubaliana na wewe kabisa. Wasimchukulie hatua huyu bwana ila wamuwezeshe. Badala ya kumchukulia hatua ni vizuri wao ndio wakajitathmini kwamba wamechemka wapi mpaka mtu akajiamini kuvaa magwanda na kufanya kazi ya kipolisi bila wasiwasi. Mimi nafundisha chuo kikuu, kama anaweza akaja mtu akajifanya mhadhiri na kufundisha na wanafunzi wamuogope kuliko sisi, inakuwa si busara kumchukulia hatua. Badala yake inabidi sisi wahadhiri tujitafakari kujua inakuwaje mtu aje afundishe na apate heshima zote kwa wanafunzi wakati tupo
You are all right. Nimependa jamaa hatumii mtutu kupata riziki tena kawashinda hata hawa wanaotuvamia na kutunyang'anya our belongings . Lkn sharia ndio hivo tena wanasema ni msumeno sasa mmmh itabidi auface huo mziki. Halafu nahisi kuna baadhi ya matrafic hii kitu pengine walikua wanaijua , iliwezekanaje mtu wa jinsi hii kufanya kazi na wao wasimjue wala kumshitukia.
 
Hata mimi nimeipenda sana hii. Nasikia huyu bwana amevuta hela nzuri tu kwa njia hii na ana jumba la kifahari. Ni mbunifu mzuri na anajua ku-take advantage ya system ambayo sio organized. Hili ni funzo kwa taasisi zetu kujipanga au kwa lugha nyingine kuwa organized
Umesahau yule mwanajeshi aliyekua analipwa mpaka mshahara , hii scandle nadhani iliibuka miaka ya hivi karibuni.
 
Katika mawazo yake jamaa utrafiki = neema ya rushwa. Vinginevyo asingfanya igizo hilo.
 
Njaa ikikamata kisawa sawa you can do wonders...!!

hahahaaa.......... Kabisaa!!!!! Ukiwa na shida woga wote kwishnehi!!! Waweza fanya vitu ambavyo viko nje ya uwezo wako bila wasiwasi!!!!!!!!
 
Bora hivyo kuliko kuwa jambazi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kama madereva waliopigwa bao na huyu jamaa huko mabarabarani wanamwona hapa nadhani wanatamani wammeze!

By the way, kwani siku zote alikuwa anajitenga peke yake na hasimami na wengine barabarani?
Hii habari ina siri nyuma yake!

Ila jamaa si mhalifu wa hatari kihivyo, maana anaishi kwa hizo buku tatu tatu za wenye magari, huku akiwafanya madereva wafunge mikanda vizuri, magari ya mizigo yasibebe abiria, na kuzuia mizigo haramu na nyara za taifa kutopitishwa barabarani mahala alipo yeye!

Wanatakiwa wampe onyo kali tu na kumwacha aende zake akasaidie familia yake.
Ila amfichue mtu anayeshona sare za jeshi na kutengeneza kofia za polisi huko Uswahilini ili wakomeshe mtandao huo mara moja, pia anaweza kuwasaidia maafande kwa namna nyingi tu.

Interest ya jeshi isiwe kumfunga jela tu raia huyo, wajaribu na kuangalia jinsi ya kusaidiana na serikali kumwonyesha huyo broda namna tofauti/halali ya kujipatia kipato, maana jamaa ameonyesha kimsingi kuwa anapenda kazi.

Binafsi natamani angesaidiwa.
 
Anaonekana kama askari wa ukweli bila wasiwasi wowote. Utafiti ufanyike kujua ni kwa muda gani kafanya utapeli huo bila shaka kipindi hicho hakuwa na shughuli nyingine mali aliyoipata ipigwe mnada na pesa kupelekwa hazina hii haina tofauti na mafisadi waliyoficha hela uswizi.
 
Maisha magumu sana hata sura yake huyo mzee inadhihirisha kuwa amepigika. Lol umaskini hufunza maarifa.
 
Kwa ujumla nakubaliana na wewe kabisa. Wasimchukulie hatua huyu bwana ila wamuwezeshe. Badala ya kumchukulia hatua ni vizuri wao ndio wakajitathmini kwamba wamechemka wapi mpaka mtu akajiamini kuvaa magwanda na kufanya kazi ya kipolisi bila wasiwasi. Mimi nafundisha chuo kikuu, kama anaweza akaja mtu akajifanya mhadhiri na kufundisha na wanafunzi wamuogope kuliko sisi, inakuwa si busara kumchukulia hatua. Badala yake inabidi sisi wahadhiri tujitafakari kujua inakuwaje mtu aje afundishe na apate heshima zote kwa wanafunzi wakati tupo

Ndugu Almuhadith wa alban. Huyu jamaa kwahali yeyote ni mkosefu. Hawezi kugushi na kujiingizia kipato kwanjia ya haramu ya uongo. Ni vyema akapata onyo ili asirudie ndio baadae wampime kama anauweledi ktk kazi hiyo ndio ikiwezekana wamuajiri. Ila wasiwasi ni kuwa ataendelea kuchukua rushwa ambayo ni kosa linalomfanya mtu apate laana ya Mungu.
 
Last edited by a moderator:
Aisee kama mchezo wa kuigiza vile! Binafsi nadhani huo ni ubunifu kwani ili upate pesa lazima uwe jasiri. Umri miaka 45 wakati ule wimbo wa maisha bora kwa kila mtanzamia haujafikia korasi jamaa kahofia uzee bila pesa.
 
Back
Top Bottom