Trafiki "feki" akamatwa akila vichwa live

Trafiki "feki" akamatwa akila vichwa live

umeonaeee, ana zaidi 45. hongera kwa ubunifu trafic feki
 
Huyu jamaa ni bonge la mjasiamali,Ningekuwa nipo magogoni ningemwachia HURU mara moja badala ya kukomaa naye huku waliopeleka pesa USWIS wakiachwa.
 
hata hivyo nembo ya polisi kwenye kofia yake ni feki? na aliipataje
 
Huyu ni mjasiriamali aisee, hizo idea ndio zinatakiwa-anatumia uoga na udhaifu wa madereva kuishi mjini. Dah bonge la idea sio mchezo...I tell you hatafungwa

Katumia fursa vizuri !sasa jiulize Kama wa nguo nyeupe kaweza kupeta je?wa nguo za kaki itakuaje?
 
hii inadhibitisha kuwa jeshi la polisi limezidi kwa rushwa mpaka watu wanatamani wawe askari polisi ili wapige hel akupitia rushwa...
 
Mmemsahau yule binti alyeidai ni mtoto wa aliyekuwa RPC wa Dar Bw Gewe ambaye alikutwa chumba cha upasuaji hospitali ya Dodoma "akiwa kazini kama daktari wa upasuaji" huku akiwa kwenye sare? Mwingine baadaye alikamatwa Bugando. Kwa polisi hao ni wengi mno. Kwanza hakuna polisi hata mmoja anayefukuzwa kazi anarudi kijijini wanabaki mjini hasa Dar kutapeli watu.
 
Kuanzia leo nikikamatwa na Police nauliza ID yake kwanza maana kila sehemu kuna watu feki
 
Nadhani Kova alitakiwa awaambie wanachi wawe wanawaulizia vitambulisho maaskari, kabla hawajakubali kuhojiwa nao...
Kama aliweza kupata sare za polisi, sidhani kama angeshindwa kujipatia pia na kitambulisho. Nakubaliana na msemo huu kuwa 'Tanzania ni zaidi na uijuavyo'!!
 
maisha yamemchapa, mpaka kudiriki kujifanya polisi feki ili kupata fedha za kujikimu sio mchezo, maisha kwa wengine ni magumu mno.
Hizi zote ni athari za kutoa ahadi zisizotekelezeka JK aliahidi ajira zile milioni ambazo hadi leo hamna kitu mtu maisha yamempiga anaikimbiza hela ya kula akaamua LIWALO NA LIWE huo ni ubunifu.
 
Hongera kwa ubunifu wake jamaa inaelekea kazi hii ameifanya kwa muda mrefu sana je hiyo lamp (red) ameipata wapi kama hana ushirika na baadhi yao wampeleke mafunzo arasimishwe rasmi
 
Kaweza kuwa na kofia, uniform na kijaketi stashindwa kuwa na kitambulisho? Cha msingi ni wale wanaokamatwa kukubali kwenda kituoni ndo mwisho wa mchezo lkn ukitaka shortcut basi unamsaidia mtanzania mwenzio aliyebuni mradi

Inasemekana kaka yake ambaye ni marehemu alikuwa Askari wa barabarani nadhani aliamua kurithi hadi uniform...
 
1157708_4912487384603_756531407_n.jpg
 
Kama ningekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi huyu jamaa ningempa kozi fupi na kumpa hiyo kazi rasmi kabisa kwasababu inaonekana anaiweza na anaipenda na yuko smati kuliko waliopo kazini kihalali.
 
maisha yamemchapa, mpaka kudiriki kujifanya polisi feki ili kupata fedha za kujikimu sio mchezo, maisha kwa wengine ni magumu mno.

Aisee hii ndo bongoland kweli kadri maisha yanavyozidi kuwa magumu watu nao wanangalia namna ya kutoka! hii nikiboko inawezekana huyu anatafuta unga wa uji wa watoto mngetukamatia nahao wa madawa ya kulevya na wanaotorosha wanyama.
 
Back
Top Bottom