kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,319
- 12,622
Bei ya mafuta imepanda sana, mishahara ni midogo sana na bidhaa zote sokoni zimepanda kwa kila mtu duniani wakiwemo hata polisi traffic.
Polisi wanazidisha ugumu wa hali hii kwa njia ya kutafuta makosa kwa wenye magari na wasafirishaji wa abiria na mizigo, hali inayosababisha gharama kubwa za usafiri na usafirishaji mijini na barabarani. Ukiendesha gari lazima uwe na hela ya askari barabarani, kwanini iwe hivi?
Wanatekeleza ukatili huu kwa njia zifuatazo.
1. Wanaanza msako wa magari yenye kasoro ndogondogo na madeni ya kubambikia ambayo hayalipwa kuanzia asubuhi kabisa wakati ule watu wanawahi kwenda kazini. Jambo hili linachelewesha watumishi, wafanyabiashara, wanafunzi, wasafiri wa mikoani na wagonjwa kufika kwa wakati waendako.
2. Kuwapiga fine madereva au kudai kitu kidogo ili kuwasamehe. Makosa yenyewe ni hata ukikosa triangle moja kati ya mbili, mkwaruzo kwenye gari.
3. Kujificha vichakani na kupiga picha kwa kificho magari yaendayo spidi na kurusha picha hizo kwa wenzao mbele ambao watakudai kitu wakuachie uendelee na safari yako, wanakuchelewesha njiani bila sababu za msingi. Yaani nililipishwa kitu kidogo kwa spidi ya mwendo wa km 54/hr. Njia zote za kwenda mikoani zimejaa viota vya kujifichia askari hawa wasioonekana njiani.
3. Pikipiki za maguta, bodaboda, kirikuu na gari za mizigo wanatembea roho juu kwenye nchi Yao wenyewe, askari wanaondoka na faida yote unayotarajia kuipata kwenye mzigo huo. Huu ni wizi sawa na wizi mwingine TU.
4. Watoto wanachanganyikiwa, shuleni wanafundishwa kuwa taa nyekundu simama, lakini wanapofika barabarani sio hivyo, traffic wanaruhusu magari kwenye taa nyekundu na kusimamisha kwenye taa ya njano na kijani, hadi inakuwa kero.
Ugumu wa maisha unazidishwa na hawa watu bila sababu za msingi. Wanaichonganisha serikali na raia wake, ili maisha ya mpiga kura wa kawaida yawe magumu sana.
Mama yetu tusaidie hili pia.