TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

Sidhani mkuu. Maana kilio ni hicho tu nchi nzima. Yeye anaharibu vipi?. Anawaambia T.R.A waje huku kitaa watutait kwenye biashara zetu?
Wewe nikuambie kalete kiungo cha albino la sivyo usipoleta nakuua huoni ni sawa nimekutuma kawaue albino then ukate viungo vyao.Ameset malengo ya makusanyo ya kodi na maduhuli la sivyo anatumbuliwa mtu sasa TRA waje wakuchekee?
 
Ni kweli mkuu.
TRA wanatumia mzunguko wa mtaji na inflows kama net profit.
Na wanaikamata hiyo hela huku wakijua kuwa huo ni mtaji.

Wanaua biashara kwa makusudi. Shoka liko shinani. Mti usiozaa matunda utaangushwa tu.
Hizi biashara zinazokufa wao wanaona sifa, hawajui sio muda mrefu wataanza kukosa pa kutoza kodi.
Wanachofanya mpaka nashangaa kama walisoma na kuelimika
 
TRA ifumuliwe isukwe upya ikibidi Takukuru wawachunguze wale maofisa vinara wa kuwafungia watu A/C zao kwani wengi wametajirika kimiliki majumba mali nyingi kwa Rishwa wanazochukua baada ya kuwafungia wafanyabiashara Account zao na biashara zao
Bila shaka Jiwe ndio anawapa kiburi.
 
Lipa kodi mkuu ili serikali ipate fedha ya kujenga barabara, kusomesha watoto bure na kutulipa mishahara.
 
Mfumo wa kodi na sheria ziangaliwe upya, Rais ameonyesha nia ya kuongeza uwekezaji ili kodi iongezeke. Kuna wakati TRA wanaichonganisha serikali na wananchi weledi utumike.
 
Kwa awamu hii mazingira ya biashara si rafiki kwa wafanyabiashara, ni bora kufanya long term investment mpaka waondoke, utawala mwingine uje na kuwe na mkakati wa kukusanya kodi ambao lengo lake si kumkomoa mfanyabiashara bali ni kulipa kodi halali kulingana na sheria za nchi. Nchi zingine wafanyabiashara ni wadau (partners) katika maendeleo lakini hapa kwetu ni kama kuna uadui wa kuviziana.
 
Sasa kampuni za watu binafsi zikifa kwa kubambikwa kodi zisizolipika mtakula wapi?
Wanafikiri kodi itashushwa kama mana. Shida kubwa ni vilaza wa biashara kuingia kwenye hizi taasisi, wakifikiria kutumia mabavu ndio njia ya kufanikisha malengo.
Principle ya kuvuna tunapopanda haiepukiki. Kuna siku watakosa pakukusanya kodi. Muda mwalimu mzuri
 
Kama waliwafungia akaunti hata ile Shule tu inayotoa hisani kwa Watoto Wanyonge wa Kitanzania...TRA siwashangai tena.
Shule?
IMG_20201210_164850_971.jpg
IMG_20201210_164850_971.jpg
 
Hao Tra mnawalaumu bure kabisa, baada ya uwekezaji kupungua na mataifa wafadhili kusita kutoa misaada/mikopo basi hayo ndio matokeo yake na bado huku tunakoelekea hali itakuwa balaa.

Wafadhili wanahofia hatua kali zisipochukuliwa dhidi ya serikali hii basi hakutakuwa tena na uchaguzi ktk nchi hii.
 
Kwa awamu hii mazingira ya biashara si rafiki kwa wafanyabiashara, ni bora kufanya long term investment mpaka waondoke, utawala mwingine uje na kuwe na mkakati wa kukusanya kodi ambao lengo lake si kumkomoa mfanyabiashara bali ni kulipa kodi halali kulingana na sheria za nchi. Nchi zingine wafanyabiashara ni wadau (partners) katika maendeleo lakini hapa kwetu ni kama kuna uadui wa kuviziana.
Nafikiri TRA na viongozi walio juu, hawaelewi mentality ya mfanya biashara.
Ukiipiga kodi faida, hilo linaeleweka.
Lakini ukipiga kodi mtaji, ni kama kugusa mfupa, mtu anafunga biashara mara moja!
 
Back
Top Bottom