Kinachwauma wadau wengi hasa wadogo wadogo ni kodi kukusanywa kwenye penalties na sio mapato
Nakupa mfano:
HUYO MWENYE SHAMBA HUENDA AKAWA NA SUPERVISOR MMOJA NA WAFANYA KAZI WATATU kila mmoja anamlipa 50,000 kwa mwezi.
Kodi ya SDL inatakiwa kulipwa na mwajiri mwenye wafanyakazi wanne, ila wafanyakazi wa mashambani wako excluded (direct shamba boys) ila sio supervisor. Kitakachomkuta ni hiki:
Mishahara 4 x 50,000= 200,000
SDL tax ( 200,000-150,000)x 4.5%=2250
Kimbembe kinaanzia hapa: 2250 x 12 (mwaka)=27,000
Penalty 225000 x 12= 2700,000
Hiyo nimekupa hesabu ya SDL kwa mwaka mmoja, interest inategemea BOT rates. Sasa imagine miaka kumi hajalipa.
KINACHOWAUMA WADAU NI KODI KUBWA KUWA INALENGWA NJE YA FAIDA.
Penalty ya 2,700,000 kwa kushindwa kulia 27,000.
Yaani wakukute kuna kikorokoro kidogo let say with hold tax ya 8000, yaan ulilipia professional service flan tuseme miaka 5 iliyopita ukasahau au ukaacha kulipa hiyo kodi ya zuio 8000 maana yake ni 8000 x interest ya BOT
MZIKI WA PENALT 225000 X 12X 5=13500,000....
ALL IN ALL TULIPE KODI ila nao watunzi wa sheria za kodi wajitadhmini
Kwahiyo aliyeandikiwa hiyo barua ni mnyonge ausio!? Acheni ushabiki wa kijinga; tembelea Mang'ola uwaone mabwanyenye. Utaratibu wa wenye mashamba makubwa kulipia kodi ya mapato upo siku zote, na ukifuatilia barua hiyo anapewa maelekezo ambayo alitakiwa kuwa ameyatekeleza kabla ya hiyo notice.
Anyway, lazima tulipe kodi ili tuweze kujitegemea; endeleeni kutegemea ubeligiji.