TRA wagonga hodi kwa Wakulima

Hawa TRA wanapoelekea sasa ni too much, watu wataogopa kufanya kila kitu nchi hii mbona uchumi utakufa kabisa, na pesa zao wataondoa benki.

Serikali wanavyofanya ni unyan'ganyi, mnawatisha sana hawa watu.
Watu walishaanza kutopeleka pesa zao benki.
 
Naamini huo mlango waliogonga hodi TRA, kuna namna, maana matukio haya ni machache sana nchi hii. Japo kisheria ni wajibu kulipa kodi katika kila pato halali, yaani pato litokanalo na kazi halali.

Subiri tuone mwenendo wake.
 
Kuna Jambo lipo hapo, anza na barua inasema wamepata habari kule Mang'ora ndipo yule jamaa yupo, anza hapo na huyo jamaa, kama hujanielewa cjui sasa.
 
Uganda wanajaribu kujiokoa na serikali ya kifascist wakati Mtanzania yeye yuko busy kulia lia badala ya kuchukua hatua!
1098760.jpg
 
Ieleweke tu kwamba hakuna jiwe litasimama bila kugeuzwa....

Jamani mimi nadhani kila mtu ana wajibu wa kulipa kodi.
Mimi ni mfanyakazi, sifanyi majadiliano na mtu ili nikatwe kodi au nisikatwe, nakutana na PAYE kwenye salary slip yangu kama taarifa tu.

Kwa mantiki hiyo kila mtu bila kujali anafanya shughuli gani anawajibika kulipa kodi, kikubwa asionewe bali iliyo ya kaisali ampe kaisali".

Kuna msemo maarufu unaosema ''wewe mfanyakazi, umejenga nyumba hii kwa mshahara gani, gari n.k". Sasa mimi huwa najiuliza, hao wanaofanya hivyo, hufanya kwa mapato gani? Je hayo mapato huwa yanalipiwa kodi kama wafanyavyo waajiriwa? Je hizo biashara na kilimo biashara(not small scales) wanalipa kodi na kuwalipa wafanyakazi wao haki stahiki?

Ni vema tutafute majibu ya maswali haya kabla ya kuwalaumu TRA. Japo na TRA kupitia machapisho haya wajitafakari kama wanatenda haki, sawa sawa na maadili ya kazi zao.

Unaweza kuisingizia serikali kwa kisingizio cha kutoza kodi, lakini kumbe unatekeleza majukumu yako kwa hila, hapo uwe na uhakika LAANA ISIPOKUPIGA WEWE ITAMPIGA MWANAO AU MJUKUU WAKO.
 
Hii haiwezi kuwa sawa, unamtoza mkulima kodi kisa anamiliki mashamba? Kwa nini wasimsubiri kipindi atakapovuna na kuyauza hayo mazao. Hii maana yake ni kwamba unamtoza mkulima kodi baadaye utamtoza mfanyabiashara atakayenunua na kusafirisha hayo mazao, yaani kodi juu ya kodi jambo ambalo litapelekea bei kupanda kwenye masoko. Ni kama mnavyofanya kwa wafanyakazi, mnawatoza kodi kwenye mishahara yao (PAYE) halafu wakienda kununua vitu na huduma wanalipa pamoja na VAT.
 
Hii haiwezi kuwa sawa, unamtoza mkulima kodi kisa anamiliki mashamba? kwa nini wasimsubiri kipindi atakapovuna na kuyauza hayo mazao. Hii maana yake ni kwamba unamtoza mkulima kodi baadaye utamtoza mfanyabiashara atakayenunua na kusafirisha hayo mazao, yaani kodi juu ya kodi jaambo ambalo litapelekea bei kupanda kwenye masoko. Ni kama mnavyofanya kwa wafanyakazi, mnawatoza kodi kwenye mishahara yao (PAYE) halafu wakienda kununua vitu na huduma wanalipa pamoja na VAT.
Wakati nchi nyingine au kufuatana na sera za vyama mbadala, hayo hayapo na huduma utapata
 
Mkuu hivi unawafahamu wakulima kweli?Wakulima huuza mazao yao wakati mwingine yakiwa bado shambani.Hao wanaotunza stock ya mazao ni wafanya biashara au wachuuzi wa mazao.Mfano kule Kahama kuna wafanyabiashara wakubwa wanama godown ya kuhifadhi mpunga hata miaka mitatu wakisubiri bei ipande.

Wakulima wengi hawawezi kuwa na uwezo huo wa kuvumilia bei ipande
Mwenzako kataja makundi mawili.
 
Ni sehemu gani kwenye sheria ya kodi shughuli za kilimo zimetajwa kama ‘exempt’ activities kwenye kulipa kodi?

Lipeni kodi sio kila kitu kulalamika, hakuna tatizo lolote kwenye hiyo barua.

Usipolipa kodi jamaa wakikubaini that’s what happens, sasa mtu kama huyu analalamika kitu gani wakati anaonekana kajitakia.
 
Kama ni shamba la uwekezaji na kuna wafanyakazi walioajiriwa,huyo mwekezaji anastahili kulipa kodi kwani litakuwa linaingiza mapato.

Halafu issue ya kodi hata mkulima anatakiwa kulipa kodi ili mradi tu awe anaingiza mapato.

Hapo nipo pamoja na TRA.

Wajitahidi kutoa elimu ya kutosha ya kodi na kubuni vyanzo rafiki vya kodi ili tuinue uchumi wetu.
Huku ni sawa na kukamua ng'ombe maziwa bila huduma yakinifu. ( Utatoa damu mwisho wa siku)
Mkulima huyu amejengewa mazingira Bora ya kilimo?
Anapatiwa masoko?
Mpunga mpaka Sasa upo maghalani Bei ni sawa na kipindi Cha mavuno, serikari haishughuliki na chochote.

Wakulima wengi ni wadogo wadogo hawana hata uwezo wa pump ndogo za maji ili kumwagilia, Sasa hivi wanaangalia mawingu.

Alafu unataka kumtoza ushuru kwa kipato gani, kwa huduma gani anazopata toka serikalini?
 
Back
Top Bottom