TRA, wafanyabiashara wana temper na EFD machines

kimaus

JF-Expert Member
May 10, 2011
565
652
Nimenunua bidhaa za ujenzi za Tsh 210, 000 lakini RISITI YA EFD inasoma total cash Tsh 178, 000 na VAT Tsh 27, 152. Nilipomuuliza mbona mashine yake haitoi risiti sahihi maana 18% ya 210, 000/= ni 37, 800 na risiti yake ilipaswa kusomeka:
cash ni 172, 200
VAT 18% ni 37, 800
Hivyo Total cash isomeke 210, 000 akawa hana majibu.
Kama mtanzania mlipa kodi sikuridhika. Wito wangu kwa mamlaka ya Mapato nchini kukagua mashine hizi, nimegundua maduka mengi ya vifaa vya ujenzi hayana kabisa hizi mashine hivyo kuwepo na mwanya wa ukwepaji kodi kwa kutolipa kodi sahihi.
 
Attachments

  • IMG_20171120_135303.jpg
    IMG_20171120_135303.jpg
    70.5 KB · Views: 131
Inaanza kuingia akilini mwa wananchi sasa,ikikomaa sana kwenye akili zetu ndio inafikia hiyo stage,mnatajana...
 
Kuna watu hawajawahi kuishi mtaani yaani wao wametoka kwa baba wakaamia hostel baada ya hapo wakacheza na rushwa ama kudra za mwenyenzi Mungu wakawa kwenye ajira moja kwa moja, watu hao wengi ni waoga wa maisha na hawajawahi onja uchungu wa kutafuta na isitoshe watu wa namna hiyo wengi hawana majukumu ndio mana akili zao sometym zimejaa upuuzi
 
Mnoko

Jamaa anadaiwa pesa ya pango

Luku

Ada ya watoto

Akiagiza bidhaa kutoka nje
Kodi anayohesabiwa ni kubwa kuliko gharama za bidhaa

Alipe 100% kodi si ataumia na kufunga biashara

Kuweni na huruma basi.khaa hakuna aliyetajirika kwa kulipa kodi 100%
Acha unoko ww lzm ni msukuma
Tayar huyu jamaa ni mchawi. Kwa roho hiyo duh hivi kwa Tanzania hii hii niwe mzalendo wa kulipa kodi ili iweje?
Tayar huyu jamaa ni mchawi. Kwa roho hiyo duh hivi kwa Tanzania hii hii niwe mzalendo wa kulipa kodi ili iweje?
Acha roho mbaya we kijana,Ukiendelea utakuja kuwa mchawi mbaya sana,
Na hawa ndio waTanzania....
 
Tayar huyu jamaa ni mchawi. Kwa roho hiyo duh hivi kwa Tanzania hii hii niwe mzalendo wa kulipa kodi ili iweje?
Kwa hiyo usipodai receipt utanufaika na nini? haujui hiyo yote inaenda kwenye tumbo la huyo ambapo ingeenda kuboresha huduma za jamii.

Akili zingine bora ifike tu mahali muwe mnaazimishwa akili maana naona kuna watu wamewashikia akili zenu. Kwenye ujenzi wa uchumi wa nchi akili kama hizi tunaziita ni za kishenzi kabisa na za kipumbavu. Right ungekuwa unaishi nchi za ulimwengu wa kwanza unakula kifungo cha miezi kadhaa gerezani ukitoka akili imepunguza makengeza.
 
Nimenunua bidhaa za ujenzi za Tsh 210, 000 lakini RISITI YA EFD inasoma total cash Tsh 178, 000 na VAT Tsh 27, 152. Nilipomuuliza mbona mashine yake haitoi risiti sahihi maana 18% ya 210, 000/= ni 37, 800 na risiti yake ilipaswa kusomeka:
cash ni 172, 200
VAT 18% ni 37, 800
Hivyo Total cash isomeke 210, 000 akawa hana majibu.
Kama mtanzania mlipa kodi sikuridhika. Wito wangu kwa mamlaka ya Mapato nchini kukagua mashine hizi, nimegundua maduka mengi ya vifaa vya ujenzi hayana kabisa hizi mashine hivyo kuwepo na mwanya wa ukwepaji kodi kwa kutolipa kodi sahihi.
Hajaiba chochote, labda tu mashine yake haijaonesha total include VAT
178,000 * 1.18 = 210,040
 
Ni ujinga kushabikia mkwepa kodi lakini ni upuuzi zaidi kulaumu wafichuaji wa wakwepa kodi. Pengine inaonesha kuwa watanzania wengi ni irresponsible citizens.

Asante muanzisha uzi kwa kufichua hilo. Niliwahi lizungumzia humu hili suala. Tatizo ni kubwa zaidi ya TRA wanavyoweza kufikiri.
Wafanya biashara wengi hawapendi kutoa risiti na wakiona unahitaji risiti basi wanafanya uhuni wa kupunguza kiasi ama kwa kukuomba wapunguze amount uliyowalipa au wanapunguza bila kukitaarifu.
 
Tuna tatizo sana mkuu hizi akili za kulialia.

Watu hawajui hata watoto wao au wa ndugu zao wanaosoma Msingi, Sekondari hadi chuo wanasomeshwa na kodi hizo hizo. hata wanapopita kwenye lami au barabara za vumbi hawajui ni kodi hiyo. Usalama wao polisi wanapopiga doria usiku ni koodi zao.

Bado nchi hii ina tatizo kubwa sana mbele.
 
Back
Top Bottom