Ushauri wa Bure kwa TRA: Anzisheni Program ya Certified Tax Educator (CTE).

lubajaro

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2015
Posts
1,781
Reaction score
1,159
Haya ni maoni na ushauri wangu wa Bure kwa TRA, naomba niwaahauri waweze kuanzisha program Maalum ya Certified Tax Educator (CTE), hii inatokana na Kwamba kwa sasa Watanzania wengi hawana Elimu ya kutosha kuhusiana na masuala ya kodi.

Tukio halisi ni la hivi karibuni lililotokea Dar es Salaam, ambapo wananchi wawili walifikishwa Mahakamani kwa kushindwa kutoa risiti ya EFD kwa wateja waliowahudumia kwa kutoa ya huduma ya kuuza Chipsi ambapo washitakiwa hapo wametakiwa kulipa Faini ya takribani ya kiasi cha Milioni 6 ( Milioni 4 na Milioni 2).

Hii Ina maanisha Kwamba Kuna haja ya haraka Sana Kwa TRA kuweza kuanzisha hii Program kwa kuandaa mtaala utakaosaodia wananchi kupewa elimu kuhusu Kodi.

My Take:
Kulipa Kodi ni jambo la uzalendo wa Kila Mtanzania, na watanzania wanatakiwa kuona Fahari kulipa Kodi kwa Serikali yao, lakini Kodi inayokusanywa inapotumika vibaya kama tunavyosoma ripoti za CAG na kama ununuzi wa Magari ya ya kifahari ya Milioni 600 kwa Wakuu wa Mikoa, na hao hao Wakuu wa Mikoa wanapokuwa wanaenda kukagua Shule na Hospitali wanakuta Shule na Hospitali hazina Madawati na Hospitali hazina Sawa...lakini gari alilokuja nalo Milioni 600. Hivi haya ni matumizi mazuri ya Kodi inayolipwa na wananchi???
 
Haya ni maoni na ushauri wangu wa Bure kwa TRA, naomba niwaahauri waweze kuanzisha program Maalum ya Certified Tax Educator (CTE), hii inatokana na Kwamba kwa sasa Watanzania wengi hawana Elimu ya kutosha kuhusiana na masuala ya kodi.

Tukio halisi ni la hivi karibuni lililotokea Dar es Salaam, ambapo wananchi wawili walifikishwa Mahakamani kwa kushindwa kutoa risiti ya EFD kwa wateja waliowahudumia kwa kutoa ya huduma ya kuuza Chipsi ambapo washitakiwa hapo wametakiwa kulipa Faini ya takribani ya kiasi cha Milioni 6 ( Milioni 4 na Milioni 2).

Hii Ina maanisha Kwamba Kuna haja ya haraka Sana Kwa TRA kuweza kuanzisha hii Program kwa kuandaa mtaala utakaosaodia wananchi kupewa elimu kuhusu Kodi.

My Take:
Kulipa Kodi ni jambo la uzalendo wa Kila Mtanzania, na watanzania wanatakiwa kuona Fahari kulipa Kodi kwa Serikali yao.
Naunga mkono hoja, TRA inayo kitengo cha elimu kwa mlipa kodi, kitu cha ajabu ni hakuna vipindi vyovyote scheduled vya elimu ya mpiga kura kwenye mainstream media zetu, zaidi ya matangazo na vipindi vya special events!, events ni events, public information programs ni vipindi vya kuelimisha umma kuhusu kodi, na matangazo ni matangazo!.

P
 
Nashukuru Legend kwa kuniunga Mkono wazo langu
 
TRA wanatangaza kuvunja rekodi kwa kukusanya mapato harafu mnasema hao walipa kodi hawana Elimu tena..washaurini TRA wapunguze lundo la kodi kwa mtu mmoja ili watu wengi wasikwepe kodi..
Wapunguze kodi za magari ya abiria,mizigo na matumizi binafsi maana huko mbele kukiwa na magari mengi au bidhaa nyingi za miaka ya karibuni ndio maisha yenyewe hayo sio mtu hii 2026 ansingia SBT kununua gari ya 2004 kwa sababu ya kodi na tunaita new model..
 
Back
Top Bottom