Tetesi: TRA kuja na 'Inheritance Tax',mdau nini maoni yako

Uongozi wa juu wa TRA huko katika hatua za mwisho kuanza mchakato wa ukusanyaji maoni juu aina mpya ya kodi itakayoanza kutumika mapema mwakani.

Kodi hiyo mpya itakuwa inawataka wanufaika wote wa urithi kulipa kodi ya asilimia 15, pamoja na hilo TRA pia hiko kwenye mchakato mwingine kama huo ambao hutawaka pia watu wote wanaopokea zawadi zinazozidi thamani ya mil tano(mil 5) pia kulipa kodi ya asilimia 15 ya thamani ya zawadi hiyo.

Bila shaka hili litakuwa pigo linguine kwa vibopa wanaohonga bongo movies magari maana itawabidi kuongeza asilimia 15 ya serikali juu yake.

Nini maoni yako?
Ni wazo zuri kabisa lakini mapato yake yatumike kwa usahihi kwa kuzingatia sheria za kibubu cha umma tulizojiwekea wenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaaaaa hii nchi bwana... Utitiri wa kodi haina maana kwamba ndo makusanyo yatakuwa mazuri..... Me nadhani ni vizuri serikali itafute namna nzuri ya kukusanya hizi kodi zilizopo.... Sina hakika ila sidhani kama hata kwa kodi zilizopo, serikali inakusanya 50%. Mtaongeza kodi hiyo ya urithi wakati Property tax imewashinda, VAT ndo usiseme, importy/ export duty imewashinda... Na kodi nyingine nyingi ambazo zimewashinda kukusanya!!!
Kodi zilizikuwepo hazikusanywi hata kwa 30%. Kwa sababu TRA hawana resources na willingness kufanya hivyo.
 
Hao TRA wanaopendekeza suala hilo hawajui wao ndio watakapokufa wataacha mali za billions? Wao ndio wanaowapa watoto wao nyumba, magari na cash worth mamilioni? Waje kuonesha mfano wasije wakatumia loopholes!

Ushauri wangu, kila mmoja wetu anayemjuwa ofisa wa TRA basi aje kutowa taarifa endapo atakapotowa zawadi inayopita threshold ama atakaporithiwa. Kujipendekeza kwengine kunaathiri maisha ya watu kwa generations! Yes, hizi kodi zipo huko ughaibuni, lakini walijipanga na kujiwekea mifumo mizuri kabla ya kuyafanya haya mambo!
 
Uongozi wa juu wa TRA huko katika hatua za mwisho kuanza mchakato wa ukusanyaji maoni juu aina mpya ya kodi itakayoanza kutumika mapema mwakani.

Kodi hiyo mpya itakuwa inawataka wanufaika wote wa urithi kulipa kodi ya asilimia 15, pamoja na hilo TRA pia hiko kwenye mchakato mwingine kama huo ambao hutawaka pia watu wote wanaopokea zawadi zinazozidi thamani ya mil tano(mil 5) pia kulipa kodi ya asilimia 15 ya thamani ya zawadi hiyo.

Bila shaka hili litakuwa pigo linguine kwa vibopa wanaohonga bongo movies magari maana itawabidi kuongeza asilimia 15 ya serikali juu yake.

Nini maoni yako?
corrupt kama uliwahi isikikiza hituba ya nyerere, ukiona serikali inandama mpaka machinga alipe kodi hiyo ni corrupted government, kama wewe ni muhenga utaifahamu hiyo hotuba, kwa tz yetu hata wakatae wananchi wao watalazimisha tu, mifuko ya jamii ni hiari wao wanalazimisha na mwisho wa siku mlengwa hapati chochote

nitakuunga mkono pale utakapoacha chuki, ubaguzi na visasi
 
wacha tunyooshwe kwa maendeleo ya taifa
kwa akili yako kabisa unadhani nchi itaendelea kwa kumnyonya mwananchi wake tena mnyonge, biko peke yake hupewi m20, tra wanachukua 18% sasa mambo gani hayo

nitakuunga mkono pale utakapoacha chuki, ubaguzi na visasi
 
Naona michango ya harusi, mazishi na pesa ama Mali ya kuposea zitatozwa kodi. Tanzania itakuwa taifa la kwanza duniani kwa utozaji wa kodi.
mbona tayari mkuu

nitakuunga mkono pale utakapoacha chuki, ubaguzi na visasi
 
kama viwanda wameshindwa wanavyodai awamu ya 5 ni ya viwanda basi tz ina eneo kubwa sana waanzishe kilimo cha kitaalamu hapo nina uhakika pesa itaingia lukuki

nitakuunga mkono pale utakapoacha chuki, ubaguzi na visasi
 
Sijui kama habari ina ukweli kiasi gani, ninachoweza kusema TRA wasiwe wavivu wa kutafuta vyanzo vya mapato
Kuna maeneo mengi sana yakifanyiwa kazi hayahitaji ongezeko la kodi nyingine

Kwa mwendo wa kuongeza kodi, michango ya harusi akina mama kubeba mimba na misiba ipo siku itatozwa kodi licha ya kwamba tayari ina ''kodi''
 
Back
Top Bottom