Tetesi: TRA kuja na 'Inheritance Tax',mdau nini maoni yako

Hata tukusanye kodi kiasi gani, kama maamuzi yetu yataendelea kuwa ya hovyo kama ilivyo sasa, hakuna tutakachojenga. Maana kodi yote ya urithi ya miaka 5 inaweza kuishia kulipa faini ya mahakama ya samaki wa Magu. Makusanyo ya kodi nyingine kama ile ya nyumba inaweza kuishia kukomboa ndege. Mfuko wa kutunzia pesa unatobolewa na maamuzi ya pupa.
 
Mambo haya sio ya kuudhi, ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi
Mimi nipo kijijini, makusanyo ya kodi mnayaelekeza kujenga ma flyover huko mijini kwa mabilioni!

Huoni kuwa jambo hili linaudhi!?

Wangenunua trekta kwa kila kijiji si wangekuwa wametusaidia sisi wakulima wa mashamba madogo kuepuka kuchelewa msimu wa mvua huku village?

Inaudhi!!
 
Hahaaaaa hii nchi bwana... Utitiri wa kodi haina maana kwamba ndo makusanyo yatakuwa mazuri..... Me nadhani ni vizuri serikali itafute namna nzuri ya kukusanya hizi kodi zilizopo.... Sina hakika ila sidhani kama hata kwa kodi zilizopo, serikali inakusanya 50%. Mtaongeza kodi hiyo ya urithi wakati Property tax imewashinda, VAT ndo usiseme, importy/ export duty imewashinda... Na kodi nyingine nyingi ambazo zimewashinda kukusanya!!!
 
Kodi haijawahi kuuacha utawala wowote salama. Margaret Thatcher aling'oka sababu ya Kodi, Mapinduzi ya Marekani yalisababishwa na kodi. Kodi ni jambo jema lakini lina limits zake wana kijani wenzangu.
 
Back
Top Bottom