Tetesi: TRA kuja na 'Inheritance Tax',mdau nini maoni yako

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,465
20,211
Uongozi wa juu wa TRA huko katika hatua za mwisho kuanza mchakato wa ukusanyaji maoni juu aina mpya ya kodi itakayoanza kutumika mapema mwakani.

Kodi hiyo mpya itakuwa inawataka wanufaika wote wa urithi kulipa kodi ya asilimia 15, pamoja na hilo TRA pia hiko kwenye mchakato mwingine kama huo ambao hutawaka pia watu wote wanaopokea zawadi zinazozidi thamani ya mil tano(mil 5) pia kulipa kodi ya asilimia 15 ya thamani ya zawadi hiyo.

Bila shaka hili litakuwa pigo linguine kwa vibopa wanaohonga bongo movies magari maana itawabidi kuongeza asilimia 15 ya serikali juu yake.

Nini maoni yako?
 
kama ni gari unlikata mara mbili kisha linaungwa tena mawazo ya kipumbavu teh teh

ila kwakweli hizi kodi hizi? ndio best option ya kuinua uchumi wetu?
wajikite ktk kuanzisha miradi itakayo pelekea tuuze bidhaa nje ya nchi vinginevyo haya mambo ni kuzidi kudidimizana tu
 
Uongozi wa juu wa TRA huko katika hatua za mwisho kuanza mchakato wa ukusanyaji maoni juu aina mpya ya kodi itakayoanza kutumika mapema mwakani.

Kodi hiyo mpya itakuwa inawataka wanufaika wote wa urithi kulipa kodi ya asilimia 15, pamoja na hilo TRA pia hiko kwenye mchakato mwingine kama huo ambao hutawaka pia watu wote wanaopokea zawadi zinazozidi thamani ya mil tano(mil 5) pia kulipa kodi ya asilimia 15 ya thamani ya zawadi hiyo.

Bila shaka hili litakuwa pigo linguine kwa vibopa wanaohonga bongo movies magari maana itawabidi kuongeza asilimia 15 ya serikali juu yake.

Nini maoni yako?
Hizo 15% so wachukue hukohuko kwenye makinikinia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona michango ya harusi, mazishi na pesa ama Mali ya kuposea zitatozwa kodi. Tanzania itakuwa taifa la kwanza duniani kwa utozaji wa kodi.
Kama ilipiga Acacia faini ya dola Bilioni 190 ambayo imeingia kwenye Guinness World Record unategemea watanzania watalipa kodi ngapi.
 
Kuna nchi yoyote inayokusanya kodi kama hizo?
Pamoja na wingi wa kodi lakini pia wabuni namna ya kumfanya mtu alipe kodi kwa hiari. Mojawapo ya njia hizo ni tax credit zinazotoa upendeleo kwa walipa kodi kwenye baadhi ya huduma na kuwapunguzia privilege wasiolipa kwa maksudi.
 
Nasubiri mpaka waipitishe rasmi ndio nije kutoa maoni yangu.

mafisadi hayana rangi
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom