ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,048
- 49,731
Naunga mkono haya mabadiliko ya Sheria ila nasema Bado Kuna haja ya kuwepo na kikosi kazi Cha TRA.
Kwa nini jambo la Kodi linaonekana ni hiari hapa Tanzania? Mathalani sijadai Risiti Kwa makubaliano na muuzaji akanipunguzia TRA watanikamatia wapi ikiwa vikosi kazi vimefutwa?
Serikali acheni siasa kwenye mambo ya msingi,hakuna anaependa kulipa Kodi eti Kwa hiari ili iwaje?
Tumefika mahala Kwa Sasa ukionekana unadai Risiti dukani Watu au muuzaji anakushangaa,unauliza Risiti ya nini? Nani akukmate Sasa kama huu ndio utaratibu wa Kuendesha Nchi basi tunaelekea kubaya.
Mwisho kama imeshindikana kuwafanya watu watoe na kudai Risiti basi Kodi zitozwe na mzalishaji Ili kusiwepo na kudai Risiti huku Kwa mnunuzi wa mwisho.
===
WAUZAJI WASIOTOA RISITI KUTOZWA 20% YA THAMANI YA MZIGO
Mamlaka ya mapato nchini TRA imewataka wananchi kuendelea na desturi ya kutoa na kudai risiti licha ya sheria kupunguza adhabu ya faini kwani serikali ina uwezo wa kubadilisha pia.
Akizungumza baada ya kukutana na washauri wa kodi, Chamaz Siriwa ambaye ni afisa usimamizi wa kodi msaidizi TRA amesema mabadiliko ya sheria imetoa nafuu kwa muuzaji na mnunuzi ambaye hatatoa na kudai risiti.
Amesema kutokana na kubadilishwa kwa sheria 15 za kodi na kuna maeneo ambayo mambo ni mapya hivyo washauri hao wanapaswa kufahamu ili wakaelimishe wafanyabiashara.
Aidha kwa kwa upande wa adhabu kwa wale ambao Hawatoi risiti Sasa sheria inaelekeza atozwe asilimia 20 ya thamani ya mzigo au Milioni 1.5 na kwa asiyedai risiti atozwe asilimia 20 ya kodi iliyokwepwa