Mtutuwandei
JF-Expert Member
- Jun 28, 2022
- 1,891
- 2,562
Ambao hawana mauzo ya 12m kwa mwaka ni wachache Kariakoo. Hata wauza matunda.Ukweli mchungu
Ambao hawana mauzo ya 12m kwa mwaka ni wachache Kariakoo. Hata wauza matunda.Ukweli mchungu
Tungeweza kuja na system kama India. Ambapo Wameweka System za Mauzo POS yenye Digital EFD (VFD) Ambayo inafaida nyingi na imeondoa changamoto na migogoro baina ya India Tax man na wafanya biashara.Hii VFD ni safi sana na inatibu matatizo mengi sana yaliyokua yakipigiwa kelele na watu kwenye EFD.
Hii inakua ni kama web based system ambayo unaweza kuitumia kwa simu janja ama computer na wewe muuzaji unakua na acount yako ambayo ndio imebeba taarifa zako.
Hiiutakua unaweka details za bidhaa unayouza details za mteja na namba yake ya simu au email kisha anatumiwa risiti hiyo. Kama utapenda print out za hardcopy basi unaweza kuunganisha na printer ndogo ya hizo karatasi za risiti na ukatoa risiti kama kawaida.
KWA NINI WAFANYABIASHARA WENGI HAWAZITAKI?
Hizi hazina janja janja za kudanganya kwenye records kama zilivyo hizi EFD ambapo muuzaji huweza kufanya cheating ya idadi /bei ya bidhaa. Pia kwenye EFD muuzaji huweza kufanya udanganyifu wa kutoa rusiti ya bei halisi lakini mashine isiweke records husika hivyo inakua ni rahisi kutoa risiti hewa.
NINACHOJIULIZA MIMI.
Serikali imeruhusu kutumika kwa huu mfumo lakini sioni hao TRA wakiupigia chapuo huu mfumo sijui ni kwanini , lakini kama serikali ikitaka ku'maximize hikihiki kidogo na hawa hawa wanaoiba basi huu mfumo ni sahihi kabisa maana upo smart na ni gharama nafuu kuutumia ukilinganisha na EFD.
Najua kwa watanzania tulivyo tutakuja kuulalamikia huu mfumo kuwa hatuna hela ya kununulia bando ili tuutumie😂😂😂😂.
Kiufupi ndio namna huu mfumo ulivyo, very smart, reliable and effective
Kuna mwaka mmoja TRA ilibuni mradi mmoja wa kufanya Watu kupenda Kudai Risiti za EFD wakiwa na furaha na Bashasha na walitangaza Ata Tender ili wafanye hilo, lakini alikufanyika japo Tender ilitangazwa na watu walibid- Inatakiwa wafufue hili , na lenyewe pia litaongeza ukusanyaji mapatoYap, unaandika kwa vile upendavyo, hata ukitaka kulist bidhaa kwa idadi yake inakubali. Kimsingi endapo serikali inataka kukusanya vizuri na kupunguza ujanja ujanja basi waweke shart hili kwa wateja wote wapyaa wanaohitaji EFD tutaona matunda yake. Ila nina wasiwasi kuwa wanufaika wa EFD wakakwamisha huu mfumo
Wale hawakukwepa kodi bali alikuwa anafanya dhuluma akiona akaunti ya mtu imenona basi yeye na kikosi chake wanatafuta sababu ya kumuangushia jumba bovu ili wagawane zile pesa au kama hataki wanamfungulia kesi ya uhujumu uchumi.Kwahyo nikikwepa kulipa kodi 2022, mwaka 2025 nisidaiwe ???
Alichokuwa akifanya jiwe akiona akaunti ya mtu imenona basi mwenye hiyo akaunti atatafutiwa sababu ili aporwe hela zake na wengine,jamaa lilikuwa dhuluma na jizi hatari.Samuel Eto mchezaji wa zamani wa Cameroon na timu kadhaa za ulaya majuzi amefunguliwa kesi ya ukwepaji kodi uliofanyika miaka zaidi ya 10 iliyopita.
Tunatamani maendeleo ya wenzetu ilhali bado tunaendekeza na kushabikia fikra za kiumama umama na kiubwete ubwete
Kuwa na TIN kunamkatisha vip mtu tamaa ?Sasa wanasema vijana wajiajiri wakimaliza chuo alafu wanakutana na Mambo mengi kama haya,,yanakatisha tamaa kiukwel
Una geto kaliii
Nani atalipa kodi kwa hiyari yake? Hata huyo wa serikalini kodi huwa inafyekwa juu kwa juu lakini angeachiwa kulipa mwenyewe asingekwenda.Wamegundua kosa lao?
Hata hivyo hangaya si alisema hataki kodi za dhuruma na kwamba anataka watu waachwe walipe kodi kwa hiari yao?
Acha kutisha watuKama hufikishi 12m Kwa mwaka ondoka Kariakoo.
Na mashine ya efd jeKuwa na TIN kunamkatisha vip mtu tamaa ?
Jaribu hii kutoka AMBWENE KONZO LIMITED inatumika zaidi ya miaka mitatu sasaDah hivi hii VFD inakuwaje?
zama zimebadirika, unaweza kuwaza kwenda kukaba au kuiba.Si Panya Rodi wataongezeka?
Unatumia simu Yako ya mkononi kutoa risiti bossDah hivi hii VFD inakuwaje?
Bado wengi tu hawana, na hawatoi efd. Naona bii efd pengine hufatiliwa kwa wenye maduka makubwa sana. Ni kama hili jambo kwa kariakoo limeshindikanaTRA wamesema yeyote afanyaye biashara Kariakoo amepewa siku 15 toka siku ya Tangazo awe na TIN na EFD