TRA Airport JNIA mnatia aibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA Airport JNIA mnatia aibu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Pdidy, Jul 18, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,508
  Likes Received: 5,741
  Trophy Points: 280
  Ukizoea harufu ya rushwa hata mke utatami kumpata kwa rushwa tu.

  Airport kisanga kimoja kikiongozwa na jamaa mmoja aitwae 'Chacha wa TRA'; Kwa kweli kila mmoja ameshindwa kumuelewa.... Egypt Air wanaletaga maji ya sadani.

  Wanaitisha kwenye mizigo then wanaanza kugawa kila box bure kwa kila department za airport. Meneja huyu amefanya hivi zaidi ya miezi kadhaa tangu ianzishwe...na watu wamekuwa wakishukuru kwa kuminimaizi baadhi ya cost za maji.

  Leo maji yakapita kama kawaida box tano ziko wazi wakaja madada wa TRA wakaangalia wakaziachia tena kwa kuomba box moja... gafla baada ya muda akatoka kijana mmoja aitwae Chacha alipoona maji yanagawiwa akakasirika akaanza kukoroma ooh peleka yaliyobaki pale TRA... akambiwa mbona yamepita huko na dada mmoja akatoa 'go ahead'?

  Kama kawaida akang'ang'ana yaende... kufika anawaambia porte bila kujua hakuwa mhusika wa EgyptAir anataka apewe dollar 20 ayaachie akafika mpaka 15usd... hii ni njaa za aibu... wewe mtu hauzi anawagawia na nyie mnachukua maji kweli hii ni haki...? Inatia aibu sana yule mmisri akaamuru zipelekwe ofisini zote na hana hata senti ama ampigie fedha kamili sh ngapi zinatakiwa anaomba aandikiwe na risiti. Hapo kimbembe kikaanza akaona aibu akawaachia...

  Jamani hizi njaa zenu TRA MTAZIACHA LINI? KWA NINI MNATAKA KUISHI KAMA MIUNGU WATU!? WAKUU WA TRA TUNAOMBA MSAADA WENU HUYU KIJANA ANAPITISHA MIZIGO MINGI TU KWA DILI WAKATI MAJI AMBAYO NA YEYE KACHUKUA ANATAKA ALIPWE TUTAFIKA HIVI?
   
 2. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Bahati mbaya siwajui kwa majina, lakini wale jamaa wa TRA pale airport wana njaa kupita kiasi. Utashangaa wanavyokung'ag'ania ufungue suitcase ndogo tu ambayo haiwezi kubeba kitu chochote cha maana.

  Mimi nigeshauri kama ukaguzi ule wa TRA ni kwa nia ya usalama wa nchi, basi waweke scanner ili kukagua mizigo yote inayoingia kabla haijafika kwenye passenger pick up belt ili kuondoa usumbufu wa kusimamisha watu na kuwalazimisha kufungua mabegi hata kama kilichomo humo ni nguo tu.

  Tiba
   
 3. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #3
  Jul 18, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Mlichopaswa kufanya hapo ni kuchukua jina la huyo afisa wa TRA! Hawa jamaa wanajifanya miungu-watu! Sasa basi!
   
 4. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wareaaaa weraaaaaaaaa weraaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa hii ni thithiemuuuuuuu
   
 5. b

  bob giza JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi wale ndo TRA wanaosimamisha watu pale..? kuna siku waliniboa nikawaambia nitawarudia tuu kivingine..lazima niwakamatishe kwa takukuru...

  Bro kashuka pale na vibegi vyake wakamwambia avifungue, wakaanza kumpigia hesabu mwisho wa siku wanamwambia alipe laki 6, bro. mwenyewe hajui kitu akaanza kuhaha kuwabembeleza hata bila ya kuwauliza laki 6 za nn..baada ya muda akawaambia aniite mm nimpe hela, ile naingia pale kuna dada mmoja ananiambia lete laki 6 bro wako apate mizigo yake..nikamuuliza yule dada laki 6 za nn, nikamgeukia bro. nikamuuliza umebeba nn kiasi cha kulipishwa laki 6, yule dada kuona ivo akaniona mm mjanja mjanja akawaita walinzi akawaambia wanitoe nje..jamaa wakaja nikagoma kutoka nikawaambia nataka kujua bro. analipa laki 6 ya nn, jamaa wakanitishia kunibeba mzobe mzobe nikawaambia nitatoka mwenyewe..ila nikamgeukia yule dada nikamwambia utaniona tuu siku nyingine..

  Mwisho wa siku wamemtoa bro euro 190 na laki 2 afu wakamwandikia risit ya laki 2, zile euro 190 wakala..nilimaindi sana nikiwa pale nje..nishawaripoti kwa washkaji wa takukuru, nasubiri bro siku anavokuja tena niwawekee mtego..yule dada naapa lazima azishike za moto, si anajuifanya anapenda mkwanja??

  Hatajua siku wa la saa..yaani lazima nimtie jamba jamba mpenda rushwa mwanahizaya mtoka pabaya yule..inaniuma sana..
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nafikiri sasa umefika wakati kuwa na kitengo maalum IKULU cha kulalamikia mambo kama haya. Ninasema hivi kwa sababu, ukiripoti polisi bure, TAKUKURU bure yaani hakuna anayejali kwani ni network ambayo inashirikiana katika kuharibu uchumi na sifa nzuri kwa Tanzania. Ule msemo wa kwamba mambo madogo kama haya hayahitaji Attention ya rais umepitwa na wakati sasa. Obama kila siku anasoma barua 10 kati ya 40,000 zinazotoka kwa wananchi wa nchi yake. Nafikiri kukiwa na influence ya IKULU straight watu wanaweza ku-behave kama tu network hii haihusiani na IKULU na ninaamini hivyo. Kuna mambo mengi sana CCM inaweza kuyafanya na kujihakikishia support kubwa ya wananchi mojawapo likiwa hili la watu kutofuata maadili ya kazi zao na uonevu.

  Niliishawahi kusimamishwa pale JKNIA karibu saa moja wakitaka nifungue sanduku langu lililokuwa na nguo zangu wakati wazungu wanaachiwa wapite kwa raha zao. Niliwaambia sifungui kitu kama wanataka wanikamate wakanihoji faragha halafu wajiandae kunilipa kwa usumbufu. yaani hasira zilinipanda kama si kuwa mtu mwenye subira unaweza rusha ngumi kwa uchungu. Yaani nimepitia nchi zenye security ya hali ya juu halafu mnaning'ang'ania nifungue bag langu. Mwisho eti wananiomba hela ya maji nikawaambia mkitaka maji nipo tayari kuwanunuliwa maji ya betri mnywe au maji ya kuwapofusha macho yenu.

  Nakumbuka wakati wa Nyerere usalama ulikuwa tight sana lakini rushwa za wazi hazikuwa kama ilivyo sasa, yaani sasa hivi system yote kuanzia TISS wanaofanya kazi pale mpaka wafagiaji wote wapo kwenye network moja, sasa ikifikia hapo basi ni dhahiri ofisi ya mkuu wa nchi inatakiwa iwe na mkono wake pale. Mtu akiomba rushwa leo kesho anapewa barua ya kupelekwa Tandahimba kuwa mshauri wa mgambo, yaani tuhuma tu ziwe ni sababu tosha kuwahamisha hawa jamaa maana kuwafukuza itakuwa harsh, na ukikamatwa unachukua ni kufukuzwa na prosecution. Hatuwezi kuwa tunafanya kazi kwa kuoteana ni lazima mtu uwe na reasonable suspecion kabla ya kumchukua mtu na kumuweka chini ya ulinzi ndipo upate ruhusa ya kufungua mzigo wake.

  Wakati wa kuondoka napo, jamaa wa scan wanaomba kwa nguvu uwaachie chenji za kitanzania zilizobakia, yaani pale hapafai kabisa. Ninajua wakuu wa nchi na viongozi wao hupitia VIP Lounge, lakini kama kweli tunataka kuondokana na uchafu huu na tamaa zisizo za msingi za watu tunaowapatia dhamana ya utendaji basi kuna haja ya kujichanganya ili uone nchi inavyoenda si kusubiri uletewe taarifa na wana network. Uongozi si kuwa na preveledge bali kuhakikisha kuwa usawa na haki vinachukua mkondo wake. Inafika wakati mtu akiataka kuja Tanzania anajishauri kwanza japo ni nchi yake anayoipenda sababu ya usumbufu unaoandaliwa kwa makusudi na hawa jamaa wanaojiona wao ndiyo Tanzania kuliko mtu yeyote yule.
   
 7. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2010
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huwa wanatazama na mtu mwenyewe mkuu, Wengine huwa tuna pita tena wakiwa wana jichekesha chekesha wakijiua ni vya moto. Kuna mzungu mmoja aliwa koromea na kumwambia jamaa mikono yako michafu huwezi gusa vitu vyangu..!!!!!!!
   
 8. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,885
  Likes Received: 20,965
  Trophy Points: 280
  mi sijawahi kusimamishwa hapo JKNIA......ila nishasimamishwa mara moja nje ya TZ na kuambiwa nifungue sanduku langu....tupe trick mzee ili tusisumbuliwe.....
   
 9. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,508
  Likes Received: 5,741
  Trophy Points: 280
  ANAITWa hosea chacha
   
 10. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,508
  Likes Received: 5,741
  Trophy Points: 280

  mpendwa usiombe kila trick zingine utakimbia ukifungua mabegi
  usifikiri wanapita hivi hivi,....utayaweza..wakiwaona hao wanaona
  wametokea mwanza ama arusha ...wewe ukifika unaonekana
  umetoka nje....ooohhh uliza wanaopita madawa utahisi mashine zimefungwa
  kumbe....@#$%^^&anyway tusimalizie
   
 11. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2010
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Trick ni jinsi ulivyo.!!
   
 12. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,893
  Trophy Points: 280
  Mkuu, una maana tuwe tunavaa suti kila tupitapo pale? wengine tumezoea casual wear
   
 13. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,885
  Likes Received: 20,965
  Trophy Points: 280
  mkuu,fafanua,hivi nilivyo.....JKNIA nimepita bila kuulizwa......SCHIPOL[AMST] nimesimamishwa na kuulizwa maswali mia.....HEATHROW nimepita bila kuulizwa chochote.....je naenda nabadilika kila airport??
   
 14. n

  nndondo JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Hivi hapa tunaweza kuja na solotion za nguvu badala ya kuleta hadithi ya Ikulu kwenye kutatua swala gumu ama la rushwa wakati wao wenyewe wala rushwa wakubwa? hebu tujaribu kuondoa mgando wa fikra na kuchemsha bongo mimi ungeniambia dawa nia walau kupiga polisi hata kama hawatafanya kitu ili mradi kutoa taarifa ama kuandika kwenye media ningekuelewa IKULU TENA MBONA UNATURUDISHA NYUMBA
   
 15. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Trick nyingine, jamaa wakianza kukuongelesha wewe badili ligha ongea English.
  Mara moja watakuacha uende zako.
   
 16. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu pale SCHIPOL huwezi kupita hivi hivi na hasa ukiwa ngozi nyeusi labda uwe na bahati ya mtende. Lakini wale jamaa angalau unaelewa kwamba wanatafuta madawa ya kulevya na vitu kama hivyo ingawaje hata na wazungu nao wanabeba hayo madawa ingawaje wao wanaachiwa kupita tu. Sasa kwanini TZ tunasimamishwa na TRA? Mimi nikiombwa kufungua begi langu na kikosi cha kuzuia madawa ya kulevya sina tatizo hata kidogo!! Lakini hawa jamaa wa TRA na njaa zao, kwa kweli wanaboa.

  Tiba
   
 17. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,885
  Likes Received: 20,965
  Trophy Points: 280
  kusimamishwa airport za wenzetu ni randomly[ingawa nakubali racism kidoogo ina-nafasi]........lakini JKNIA ni njaa tu ya hao waungwana maanake mwisho wanaishia kukuomba hata $10.........always nasafiri casual[jeans-tshirt-sneakers] siku nyingine nasimamishwa siku nyingine sisimamishwi na SIJAWAHI KUSUMBULIWA JKNIA!!!!!!!
   
 18. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2010
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mpaka umeulizwa maswali Mia hiyo ndege haijakuacha tu mkuu? na ukiona umeulizwa ma swali mia umeonekana ndivyo sivyo ..Jinsi unavyoonekana kutetemeka tetemekwa kwa woga wa kupanda ndege lazima uulizwe maswali mengi..!!!
   
 19. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #19
  Jul 19, 2010
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu "jinsi ulivyo" sio suti kwani suti zimejaa hata kwa makonda wa dala dala...!!
   
 20. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,885
  Likes Received: 20,965
  Trophy Points: 280
  lol.......sio mgeni wa safari hadi kutetemeka.....nilikuwa transit for more than 5 hrs..........at least umefafanua unavyoonekana maanake wengine wanafikiri ni mavazi.....body language wenye kujua kazi yao wanaitumia vizuri.
   
Loading...