Toyota vx v8

Tonge

JF-Expert Member
May 7, 2010
695
12
Moja ya magari 2 ya ikulu yaliyong'oka tairi.je? Magari haya ya kifahari lini serikali yetu itaacha kuyanunua? Maana kumbe hata kwenye rough road yenyewe hung'ota tairi si agheri tuendelee kununua mkonga nje tu kwa bei nafuu.tubadilike jamani.
 
Attachments

  • gariyarais.jpg
    gariyarais.jpg
    12.8 KB · Views: 598

Hii ngoma ingekuwa kwenye mwendo wa kasi kama wanavyo jiachiaga sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine.
 
Duh noma utakuta gari kama hilo thamani halisi ni 100m ila limenunuliwa kwa 250m au zaidi hii ndio bongo ya Wadanganyika

Lakini uelewe gari kama sita hivi za aina hiyo moja kwenye msafara mmoja ni bullet proof na hiyo bei ya 100m itakuwa sivyo. Hapo weka zaidi ya 200m au kwa ujumla kama ulivyosema 250m for just one piece bro. hiyo gari ni noma. hata waziri mkuu wa Australia haruhusuwi kuitunia hiyo gari.
 
Hata ungetumia gari aina gani ,swala hapo ni kujua kuwa ajali haina kinga jamani,ni kumshukuru mwenyezi na kumuombaili tuendelee kufuata kanuni za utunzaji na uendeshaji wa vyombo vya moto.
 
Hilo gari halifai tena kwa matumizi ya ikulu ngoja waziri mkulo akakope stanbic wanunue aina ingine kwa 500m!wakati mwananyamala hosp wazazi wanalala kitanda kimoja wanne!lukuvi anasema urbanisation ndio tatizo
 
Hata ungetumia gari aina gani ,swala hapo ni kujua kuwa ajali haina kinga jamani,ni kumshukuru mwenyezi na kumuombaili tuendelee kufuata kanuni za utunzaji na uendeshaji wa vyombo vya moto.

Madereva ukumbushwa kuwa kabla ya safari angalia matairi ya gari, nati kama zimelegea, n.k. hata BP wanakuwa na kipindi ITV lakini madereva hawa hawajali kabisa! Sasa huku si kukinga ajali in advance?
 
Katika gazeti la Rai Mwema Ikulu imesema lilipata pancha na si kuchomoka kama picha inavyoonyesha na ndio hilo hilo eti dereva wa rais alisahau kuondoa gear ya 4WD bila ya kujua na kusababisha gari kuwa na mwendo mdogo na kufanya rais aletewe gari lingine..Ama kweli akili za kuambia inabidi uchanganye na za kwako..
 
Mnashangaa Bure Madereva hawa hawajui wajibu wao ndiyo maana hata mkubwa akitaka kupita gari zote zinazuiwa nina wasiwasi hawawezi hata kupishana na magari mengine
 
Katika gazeti la Rai Mwema Ikulu imesema lilipata pancha na si kuchomoka kama picha inavyoonyesha na ndio hilo hilo eti dereva wa rais alisahau kuondoa gear ya 4WD bila ya kujua na kusababisha gari kuwa na mwendo mdogo na kufanya rais aletewe gari lingine..Ama kweli akili za kuambia inabidi uchanganye na za kwako..

Hahaha, inamaana picha inadanganya, gari lilipata pancha? Kweli nchi ya wadanganyika. Kung'oka tairi kwa gari ya ikulu, ukilinganisha gharama halisi ya manunuzi na matengenezo ya haya magari ni kitendo cha aibu.

Ukiambiwa gharama za mwezi za ukarabati, unaweza kupata ugonjwa wa moyo. Lakini ndio hivyo tena, V8 imegeuka imekua bajaji!
 
Hii ngoma ingekuwa kwenye mwendo wa kasi kama wanavyo jiachiaga sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine.

wenye meno wataendelea kula, vibogoyo wataambulia kula kwa macho. wenye rungu wataendelea kupunja wasio na rungu, wasiokuwa na rungu wanaendelea kuonewa tu lakini wananyamaza kimya tu, wenye vyeo wanavitumia wapendavyo, waliowapa vyeo wanahangaika. wenye nafasi wanatibiwa hospitali nzuri, waliowapa izo nafasi wanashindwa kupata hata hospitali yenye garama ya gari moya wanayoendesha hao waliodhaminiwa madaraka. tafakari!
 
Hapo ndio ninapochoka na wabongo wasivyojikubali, kumbukeni marekani wamerudisha magari ya Toyota Kiwandani. Its happen man
 
Songambele;929515]Hapo ndio ninapochoka na wabongo wasivyojikubali, kumbukeni marekani wamerudisha magari ya Toyota Kiwandani. Its happen man[/QUOTE]

jamani kumbukeni ilo ni tatizo la kiufundi Acheni majungu,mbona Marekani wao wamerudisha maelfu ya magari kiwandanani sasa ilo gari la jk kuchoka tairi mshaanza some time's angalieni na matatizo ambayo kwenye gari yanaweza tokea any time
 
Hili gari halikununuliwa jipya ni lazima mtumba kutoka Dubai, ndio maana tairi ilichomoka; na jamaa wametia kibindoni kamisheni kibao!! Gari mpya hazina hicho kipaa cha nyuma!! Wajanja wengi Bongo!!
 
Hii ngoma ingekuwa kwenye mwendo wa kasi kama wanavyo jiachiaga sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine.

bisheni msibishe ngoma ni mtumba,hamna cha marekani kurudisha wala nini.hizi njaa zitatutoa roho.nimesema mara nyingi ikulu kuna wahuni sasa huyu mkulu mpaka atakaposhtukaatakuwa ....... naogopa kumalizia wataniambia niwe mtabiri wa serikali baada ya hayo mambo kutokea
 
duh,ebana hili goma nivipi kuhusu wese?nadhani linakunywa km ngamia,kuna mtu anajua linatumia vipi mafuta maana!"
 
Mh! Mbona Rewyemamu alisema ni pancha? Au ina maana kuwa haelewi maana ya pancha na tairi kung'oka?
 
Back
Top Bottom