Kama hujawahi kuendesha hizi gari tano, KAJITAFUTE!

Bemendazole

JF-Expert Member
Nov 14, 2020
2,352
5,871
1. Suzuki Carry
Hii inaingizwa kwenye list kutokana na ubora wa engine yake. S. Carry ni gari ambayo engine yake iko very robust. Inachanganya kwa upesi sana. Huwa naifananisha engine hii kama engine ya piki piki ya mashindano iliyofungwa kwenye gari.

2. Mitsubishi Pajero Mini
Ukishasikia gari inaitwa Pajero basi lazima iwe vizuri kwenye hivi vitu viwili; stability na braking systsm.
Pajero mini ni gari ambayo iko stable sana hasa kwenye bara bara za vumbi. Ina uwezo mkubwa sana wa kusimama. Inaweza kutoka spidi 80 hadi 0 ndani ya umbali wa mita mbili

3. Isuzu D Max
Kuna mtu aliwahi kusema, kwa kuwa Isuzu wamejikita katika kutengeneza Magari makubwa basi ni rahisi sana kwao kutengeneza magari madogo. Dmax iko vizuri katika mifumo yote. Ina suspensio nzuri, gear knob na brake ziko smooth, taa ina mwanga mzuri na wa kutosha. Inafaa sana kwa safari ndefu na hata za usiku

4. Toyota IST
Ukiipata ile yenye 1500 cc, huhitaji tena kuwa na v8. Highway inafanya vizuri sana. Iko stable kwa spidi kubwa. Unaweza tembea 160 bila wasi wadi wowote.

5. Range Rover
Hapa nadhani Range inajizungumzia yenyewe. Ukiendssha Range rover, gari zingine utaziona kama 'taka taka'. Kwanza ina nguvu kubwa, ina suspension nzuri na bara barani iko vizuri.

6. Nissan Hardbody (bonus track)
Hii inaingizwa kwenye orodha kutokana na uwezo wake rough road. Ukiwa na hii gari, huwezi kuelewa kukwama kwenye matope ni kitu gani. Ina 4 wheel drive pamoja na diff lock, pia ina uwezo mzuri wa kukimbia na kutoa upinzani kwa gari nyingi bara barani.

Ukiipata yenye Turbo, maisha umeyapatia.
 
Nimepiga trip mbili na IST ya 1.5 AWD Mwanza to Moshi... bwana hutu tugari hutu tunafunguka mpaka unaogopa mwenyewe
 
Kwamba nikaendeshe Suzuki carry ili nionje injini tamu?! Am I a test driver?

Sio kila mtu ana hobby na magari wengine simu, wengine safari n.k
 
Back
Top Bottom