Land cruiser VX V8 ni ndege ya chini aisee! Ndiyo maana viongozi hawataki kuyaachia

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Land cruiser vx v8 hii gari isikie tu!

Hii ni ndege ya chini!
Ukionja hii gari unaweza ishauri Serikali kuwe na leseni maalum kwa madereva wa hizi gari maana ni ndege ya chini wallah!

Nahisi ndiyo maana ilibatizwa Ushangingi maana ni kweli VXV8 ni shangingi la njia siyo uwongo!

Na ukitaka kuielewa vizuri panda kwenda safari ndefu ndiyo utajua TOYOTA HAPA ALITULIZA KICHWA.

Uraibu wa hii gari ni viongozi wachache sana wakiafrika wanaweza kukubali kuushinda ili waachane kununua magari Haya ya gharama kubwa!

Zote zipo fiti ila hii land cruiser vx v8 2022 ni kiboko yao!

Ni gari bomba sana, very comfort, stable, luxury, High speed tolerance, sensor of crush, music system, massaging seat, sleeping sensor and much more!

Napata ugumu kukuelewesheni hii ya 2022 ilivyo bora na bomba ila kama kuna mtu yuko karibu na Mwigulu Nchemba anayo moja bado mbichi kabisa unaweza kuitizama ni mashine!

Land cruiser vx v8 inasifa moja kuu! INAOMBA NJIA MUDA WOTE!

Tunawalaumu bure viongozi wanavyopita pyuupyuupyuu huko barabarani siyo wao! Bali ni land cruiser vx v8 ndivyo inataka mambo hayo!

Naomba Mungu anijalie na mimi siku nimiliki yangu!

Toyota-land-Cruiser.jpeg
 
Watakuja wazee wa magari ya magharibi ei k ei ant-japanese

Lakini nikuulize utamu huu ni kwamba umesoma tu au umeipanda na kama umeipamda, ushapanda ma BMW x6, vipi g wagon za bwana benz? Je hata nissan patrol ushapanda?
Hao wote wanakuja kufeli kwenye rafu road, land cruiser vx v8 inafiti kote, lami hadi shamba pori kwa pori ambako BMW na wengine ni kuku wa kizungu!
 
Vxr v8 ni habari nyingine.

Huwa najiuliza kwanini Serikali nyingi za kiafrika viongozi wanapenda hiki chuma, ni habari nyingine.

Hata viongozi wa Ulaya wanatamani wangekuwa wanatumia Toyota sema kwa unafiki wa kuonyesha uzalendo unakuta wanalazimika kupanda magari ya kampuni zao.
 
Vxr v8 ni habari nyingine.

Hua najiuliza kwa nini serikali nyingi za kiafrika viongozi wanapwnda hiki chuma, ni habari nyingine.

Hata viongozi wa ulaya wanatamani wangekua wanatumia Toyota sema kwa unafiki wa kuonyesha uzalendo unakuta wanalazimika kupanda magari ya kampuni zao.
Ndiyo maana watu wanalogana ili wasipigwe chini kudadeki hii ni ndege!

Yaani hii gari hata dereva tu anasahau shida za dunia kwa muda!
 
Back
Top Bottom