Binafsi huwa ninawakubali sana wale wanaolalamika kivitendo na sio kuishia kwenye maneno tu, so nakupa tano kaka kwani umeshout kwa vitendo.
Tukirudi kwenye website, naomba kutoa mchanganuo wangu kwa milengo ifuatayo.
1. Tabia
Kitu cha msingi kwenye tovuti yoyote ni kufahamu culture ya wasomaji, kwani sisi kwenye IT huwa tunasema IT doesn't matter ila kinachomatter ni jinsi gani utaweza kufikisha tekinolojia kwa watu rasmi, kwa tabia ya Watanzania (nikiwemo mimi) huwa sipendelei tovuti yenye contents zilizokithiri, kwa tovuti yako, ni dhahiri imejaa contents nyingi mno ambapo ni lazima mtu aachwe hewani.
Naweza sema kuwa na contents nyingi sio tatizo bali mpangilio (structure) ya mpangilio ni tatizo. Kwenye lugha ya website huwa tunasema watu huwa hawasomi bali huscan hivyo website visibility ni kitu muhimu mno. unatakiwa kuzingatia mambo haya.
-mtu ajue nini website inafanya kwa jicho la kwanza (Kwa tovuti yako haijajitofautisha na ile ya mwananchi.co.tz)
-Kutumiamultimedia (Kwenye tovuti yako umetumia text nyingi mno)
- Social media integration ( watu wanapenda kujiachia, so kwa kuona rafiki zake wa FB basi inaongeza attensio yake kusoma)
-Rangi lazima ziwe na maana husika,na zinazovuta. Rangi kwenye tovuti yako haziashilii utanzania (ulichofanya ni kucopy na kupaste rangi zao, masanja anaweza kukutengenezea video ya kopi na pesti (hehe) na vilevile hazipo kwenye Multimedia colors za website design. Unaweza kugoogle rangi za website na matumizi yake.
-Epuka kuwa kama wao, ni kosa kufanana na website fulani, kwakuwa user huwa hawasomi, akiscan na kugundua inafanana na web fulani basi ataasume inafanana kila kitu na kuondoka. Kwenye website yako umetumia very default template bila ya customization kubwa, na inafanana mno na tovuti nyingi za media za Tz.
2. Technology. Kama ambavyo nimewahi kuelezea kwenye mafundisho yangu ya joomla kuwa, kikommo cha joomla ni wewe mwenyewe. Hivyo joomla inakuwezesha kutengeneza website ya level nyingine. Ukiangalia kwenye tovuti yako, vitu almost vyote ni basic, sijaona advanced extension au extension yoyote special kwa ajili ya multimedia. Hivyo itakuwa ngumu mno kumshawishi administrator wa TBC1. Kama mimi ndiye Webmaster wao, ningekuuliza, what's special in your website??
3. Usalama.
Kwa sasa tunazungumzia Joomla 3.0, ila kwenye tovuti yako umetumia 1.5 ambayo haina tena maboresho tangu joomla 1.5.26. Haishauliwi na ni hatari kuona bado watu wanatengeneza tovuti kwa kutumia joomla 1.5. Hivyo hii ni dole chini nyingine. Unaweza kuona kwa urahisi just kwa kwenda
- Administration
...naendelea kwenye thread nyingine...