miezi gani mizuri kulima matango Dar..kutoingiliana na Yale yanayotoka mikoani...Unapata tango zaidi ya ishirini kwa mche sasa piga hesabu eka moja inaweza accomodate miche 1000 na angalia bei ya tango mtaani kwenu ni ngapi. Bei ya shamba ni sh 300 so zidisha mara idadi ya tango kisha idadi ya miche urajua kwa mwezi unapata pesa ngapi maana mbegu hii ya monalisa ni ya mwezi
Hapa najibu swali la trojaan hapo juu
vipi kuhusu changamoto zake?Ngoja nikupe mfano. Tuseme unaishi katika nyumba ambayo kwa upande wa nyuma una eneo ambalo lina ukubwa wa upana hatua tano na urefu vile vile. Hivyo 5 x 5 = 25 square meter. Katika kila square meter 1 unapanda miche 4 hivyo x 25 ni miche 100. Kila mche unakupa kilo 15 yaani sawa na ndoo moja na nusu ya nyanya kwa mwezi. Bei ya shambani ukiamua kufanya mia tano x 15 ni sh. 7,500 kwa kila mche kwa mwezi. 7,500 x miche 100 = sh. 750,000 kwa mwezi. Je kwa miezi nane ya uvunaji itakuaje? 6,000,000. Na hii ni bila greenhouse
Je utaendelea kunyanyaswa na bosi wako ulipoajiriwa na kuendelea kumtajirisha mpaka lini?
vipi kuhusu changamoto zake?
Hata na Biashara2000 mwenyewe atupe mrejesho of what transpired and of what is going on now!Mulioweza kufuata mafunzo ya Biashara2000 mutupe mrejesho wa kilimo kwa njia ya kisasa tafadhali.
Hakika mkuuHata na Biashara2000 mwenyewe atupe mrejesho of what transpired and of what is going on now!
Bw. Ngamba umeuliza swali zuri sana, ni swali ambalo watu wengi wamekuwa wanapenda sana kufahamu. Kwa bahati ambayo sio poa wakulima wengi na wale ambao wana mpango wa kulima imekuwa vigumu kwao kupata info sahihi ntalijibu katika vipengele viwili
Mbegu hizi special kama Heirsloom, Corazon, Anna F1, Julia, Carson, Memoneta na n.k zina shelf life kubwa tu na zimeboreshwa kutoka katika nchi za ulaya zenye baridi na zilikuwa maalumu kwa ajili ya kupandea kwenye greenhouse. Sasa waafrika tunafoji na kuamua kuzitumia huku afrika ndio maana wakulima wengi wanalalamika zinawatesa zinashindwa kuvumilia hali ya joto ndio maana zinalimwa Arusha na Nairobi angalau penye kaubaridi
The kick ni kuwa hazikubali nje ya greenhouse yaani kulima kilimo cha wazi. Hii inanyima fursa kwa watu wasio na uwezo wa kifedha wa kujenga gh kushindwa kufanya kilimo cha kisasa na kufanya wakulima wa kawaida kubaki na zile mbegu za kawaida mfano Tengeru na Tanya
Mbegu ambayo mi nawashauri watu waitumia ndio ambayo mie naitumia. Hii imeboreshwa kutoka nchi ya ulaya ambayo iko karibu na bahari ya med. ambalo ni eneo lenye kiwango angalau cha joto. Baada ya hapo ililetwa afrika kusini kuboreshwa Zaidi. Pia ikajaribiwa ktk nchi za afrika ktk gh na kilimo cha wazi. Mbegu hii unaweza ilima ndani ya gh na kilimo cha wazi km ilivyo kwenye hiyo video yangu hapo juu na inavumilia ukame na jotohivyo ni nzuri kwa mikoa yote ya tz
Green houses kibao zinatelekezwa..sijajua shida ni nn..jiran yangu ametelekeza GH yake...!Kila la heri wakulima
Nimeona hili pia, sijajua changamoto iko wapi kwa wakulima wenzangu wa huu mfumo, sie wa Kilimo cha ardhi isiyofunikwa tunaendelea kupambana na jembe.
"Kama unataka mali utaipata shambani"
Production cost ziko juu hasa kwa small scale producers hivyo compensation yote unaifanya kwenye mauzo ndiko mkwamo hutokea, kwanini mbongo anunue nyanya za buku tano kwako wakati zinauzwa jero soko la mkulima kitaa?Kwakweli pambaneni kila la heri..nadhan mazao Gh Ni aghali pia..mfano nyanya yy alikua anauza sado 12000..naona kaitelekeza mwaka wa 4 huu
Nataka hiyo huduma ya kupimiwa udongo ili tulime kisasa km vidro ya shamba lako inavyoonyesh. Tuna wakulima wengi tu huku mvometo wanahitaji hiyo huduma
WeweMhhh sijui nna ukata wa matukio flani au nini ili nimependa sauti ya mwenye video🙈🙈