Tour fupi ya shamba langu la greenhouse

Kutokana na hali ngumu ya kifedha kwa wakati huu, watu wengi wamekuwa wakiniuliza ni mazao gani wanaweza lima na yakastawi ndani ya muda mfupi. Wanataka kujua ni jinsi gani wakapata pesa fasta kwa muda mfupi watengeneze kipati. Kusubiri muda mrefu kwa kulima mazao ya muda mrefu wengi hawataki.

Sasa haya ni baadhi ya mazao unayoweza lima ndani ya mwezi ukawa ushaanza uza kwani yatakuwa tayari:

-Chinese
-Spinach
-Matango - Tumia mbegu ya Monalisa. Nunua genuine na si feki. Feki hazioti

Ukilima hivi utakuwa unapata pesa ndani ya muda mfupi
 
Nimekuwa nikipokea simu nyingi sana watu wakiulizia kuhusu ule mfano niliotoa hapo juu kuhusu ni jinsi gani unaweza pata laki saba kwa mwezi. Swali hasa limekuwa likielekezwa kwenye mtaji. Wanaulizia ni mtaji kiasi gani utauhitaji wakati unaanza. Kama eneo lako ushafanya utaratibu wa kupata maji tuseme hauna maji ktk eneo lako ia unaletewa na mkokoteni na kuyahifadhi kwenye pipa, Zaidi ya hapo utahitaji sh. 150,000 ambayo watu wengi wanaweza kuimudu

sijakuelewa hapo Biashara2000 hiyo laki na nusu inajumuisha na mbegu au miche?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unachohitaji ni mbegu na mbegu ndiyo ukiiotesha ktk kitalu ndio utapata miche, hununui miche. Faida ya kilimo utaiona ukitumia elimu na mbegu bora hio pesa inatosha
 
Ngoja nikupe mfano. Tuseme unaishi katika nyumba ambayo kwa upande wa nyuma una eneo ambalo lina ukubwa wa upana hatua tano na urefu vile vile. Hivyo 5 x 5 = 25 square meter. Katika kila square meter 1 unapanda miche 4 hivyo x 25 ni miche 100. Kila mche unakupa kilo 15 yaani sawa na ndoo moja na nusu ya nyanya kwa mwezi. Bei ya shambani ukiamua kufanya mia tano x 15 ni sh. 7,500 kwa kila mche kwa mwezi. 7,500 x miche 100 = sh. 750,000 kwa mwezi. Je kwa miezi nane ya uvunaji itakuaje? 6,000,000. Na hii ni bila greenhouse

Je utaendelea kunyanyaswa na bosi wako ulipoajiriwa na kuendelea kumtajirisha mpaka lini?
Bosi squre mita 25 (5x5) inatoa miche 36 tu na sio miche 100.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wanaulizia huduma ya kupima ph ya udongi ili kujua ni kiasi ganicha mbolea uweke ktk miche yako. Wengi wabataka niwaelekeze jinsi ya kupima ph mwenyewe nyumbani na kujua ni kiasi gani cha mbolea kinahitajika. Faida ya kupima ph inakusaidia usibahatishe vipimo vya mbokea na kufanya miche yako kuungua na kuwa ya njano utadhni yameshanbuliwa na ugonjwa kumbe sio. Sasa kwa anayetaka nimwelekeze anaweza nicheki kwa simu
 
Habarini wanajamvi,
Naomba kueleweshwa ubora kati ya mbegu hizi mbili za zao la TANGO.
1. MONALISA F1
2. DARINA F1

Ipi ni bora zaidi kuliko nyingine. Najua zote zinaweza kuwa bora, ila namaanisha BORA ZAIDI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom