Tour fupi ya shamba langu la greenhouse

Huu uzi nimeugundua juzi,kutokana na umuhimu wake + haja ya moyo wangu nimesoma/pitia michango yooote. Sijawahi kuta uzi wenye page 10+ nikasoma zote lakini kwa uzi huu nimethubutu.

Hakika nimefaidika lakini napaswa kufika katika shamba darasa kujazia pale palipo baki,sasa hivi ni saa kumi kasoro ikifika asubuhi tu nakupigia simu mkuu.
 
Unapata tango zaidi ya ishirini kwa mche sasa piga hesabu eka moja inaweza accomodate miche 1000 na angalia bei ya tango mtaani kwenu ni ngapi. Bei ya shamba ni sh 300 so zidisha mara idadi ya tango kisha idadi ya miche urajua kwa mwezi unapata pesa ngapi maana mbegu hii ya monalisa ni ya mwezi

Hapa najibu swali la trojaan hapo juu
miezi gani mizuri kulima matango Dar..kutoingiliana na Yale yanayotoka mikoani...
 
Ngoja nikupe mfano. Tuseme unaishi katika nyumba ambayo kwa upande wa nyuma una eneo ambalo lina ukubwa wa upana hatua tano na urefu vile vile. Hivyo 5 x 5 = 25 square meter. Katika kila square meter 1 unapanda miche 4 hivyo x 25 ni miche 100. Kila mche unakupa kilo 15 yaani sawa na ndoo moja na nusu ya nyanya kwa mwezi. Bei ya shambani ukiamua kufanya mia tano x 15 ni sh. 7,500 kwa kila mche kwa mwezi. 7,500 x miche 100 = sh. 750,000 kwa mwezi. Je kwa miezi nane ya uvunaji itakuaje? 6,000,000. Na hii ni bila greenhouse

Je utaendelea kunyanyaswa na bosi wako ulipoajiriwa na kuendelea kumtajirisha mpaka lini?
vipi kuhusu changamoto zake?
 
Natumaini mnaendelea na shuguli za kulijenga taifa kwa namna moja au nyingine.

Wakuu mliokwisha anza/mlioacha na mnaoendelea kulima kwenye greenhouse ingependeza mtupe feedback ni wapi mumefikia, pia itawasaidi wakulima wengine
kupata mwelekeo zaidi wa maamuzi yao au kufanya marekebisho kadhaa.

Ni changamoto gani mmezipata hadi kutengeneza faida au hata kuachana na ulimaji huo.

Greenhouse yako inatosha kuzalisha kiasi kinachotakiwa na soko lako? Unazalisha hadi bidhaa zinabaki au zinakwisha na bado soko linahitaji?

Soko lako au wananunuaji wako ni watu gani, had mtumiaji wa mwisho? Wananunua kwa bei uliyoamua?

Ili kutengeneza faida kubwa, Je bidhaa/produce yako unazalisha mwaka mzima au unalengeshea kipindi cha bei ya juu tu? Au unabadilisha mazao tofauti tofauti?

Ili kutengeneza faida kubwa, unalima kwenye greenhouse na nje kwa pamoja?

Kwa walimaji wa greenhouse, umeweza kufaidika kiasi cha kurudisha gharama ulizotumia kuanzisha greenhouse?

Usahuri wako na maoni kama unao/unayo.

Asanteni sana.
 
vipi kuhusu changamoto zake?

Nategemea unauizia changamoto za kilimo kwa ujuma hasa kwa kiimo cha waz yaani bila gh. Kwanza eewa kuwa kilimo ni biashara km biashara ingine yoyote. Km unategemea itakuwa ni biashara yenye hangamoto chache u isiyonayo kabisa utakuwa unajidanganya. Naisha ni kupambana hakuna kitu chenye thamani ambacho unakipata kirahisi ktk maisha hivyo km unataka kuingia ktk kilimo usiogope hangamoto sababu hata ktk maisha ukiamua kutofanya chochote bado pia pana hangamoto

Challebges za kiimo hiki zinategemeana na aina ya zao na eneo unapolimia kn mara nyingi ni watu kulima bila kuwa na elimu ya kiimo matokeo yake kupoteza muda na pesa zao na kuishia kukichukia kiimo, kilimo wazi kutegemeana na eneo ulipo km hutunzi mazao yako na kwakuwa unatumia mbegu zenye uzao mkubwa kuna uwezekano ukawa unaibiwa mazao yako usiku, mbolea na madawa feki yamejaa sokoni, wakulima kutokujua magonjwa na wadudu waharibuo mazao, kutopata maji ya kutosha ya umagikiaji, nk

Lkn unatakiwa kukaza moyo na kulima, waliofanikiwa ktk kiimo ni wale tu wasioogop na walio tayari kujaribu. Jaribu sasa utasubiri fanya uliyoyapanga hadi siku gani?
 
Bw. Ngamba umeuliza swali zuri sana, ni swali ambalo watu wengi wamekuwa wanapenda sana kufahamu. Kwa bahati ambayo sio poa wakulima wengi na wale ambao wana mpango wa kulima imekuwa vigumu kwao kupata info sahihi ntalijibu katika vipengele viwili

Mbegu hizi special kama Heirsloom, Corazon, Anna F1, Julia, Carson, Memoneta na n.k zina shelf life kubwa tu na zimeboreshwa kutoka katika nchi za ulaya zenye baridi na zilikuwa maalumu kwa ajili ya kupandea kwenye greenhouse. Sasa waafrika tunafoji na kuamua kuzitumia huku afrika ndio maana wakulima wengi wanalalamika zinawatesa zinashindwa kuvumilia hali ya joto ndio maana zinalimwa Arusha na Nairobi angalau penye kaubaridi

The kick ni kuwa hazikubali nje ya greenhouse yaani kulima kilimo cha wazi. Hii inanyima fursa kwa watu wasio na uwezo wa kifedha wa kujenga gh kushindwa kufanya kilimo cha kisasa na kufanya wakulima wa kawaida kubaki na zile mbegu za kawaida mfano Tengeru na Tanya

Mbegu ambayo mi nawashauri watu waitumia ndio ambayo mie naitumia. Hii imeboreshwa kutoka nchi ya ulaya ambayo iko karibu na bahari ya med. ambalo ni eneo lenye kiwango angalau cha joto. Baada ya hapo ililetwa afrika kusini kuboreshwa Zaidi. Pia ikajaribiwa ktk nchi za afrika ktk gh na kilimo cha wazi. Mbegu hii unaweza ilima ndani ya gh na kilimo cha wazi km ilivyo kwenye hiyo video yangu hapo juu na inavumilia ukame na jotohivyo ni nzuri kwa mikoa yote ya tz

Hapa hujaitaja aina ya mbegu unayotumia wewe.....pls inaitwaje?
 
Nimeona hili pia, sijajua changamoto iko wapi kwa wakulima wenzangu wa huu mfumo, sie wa Kilimo cha ardhi isiyofunikwa tunaendelea kupambana na jembe.
"Kama unataka mali utaipata shambani"
Green houses kibao zinatelekezwa..sijajua shida ni nn..jiran yangu ametelekeza GH yake...!Kila la heri wakulima
 
Nimeona hili pia, sijajua changamoto iko wapi kwa wakulima wenzangu wa huu mfumo, sie wa Kilimo cha ardhi isiyofunikwa tunaendelea kupambana na jembe.
"Kama unataka mali utaipata shambani"


Kwakweli pambaneni kila la heri..nadhan mazao Gh Ni aghali pia..mfano nyanya yy alikua anauza sado 12000🙆..naona kaitelekeza mwaka wa 4 huu
 
Kwakweli pambaneni kila la heri..nadhan mazao Gh Ni aghali pia..mfano nyanya yy alikua anauza sado 12000..naona kaitelekeza mwaka wa 4 huu
Production cost ziko juu hasa kwa small scale producers hivyo compensation yote unaifanya kwenye mauzo ndiko mkwamo hutokea, kwanini mbongo anunue nyanya za buku tano kwako wakati zinauzwa jero soko la mkulima kitaa?
Shukrani mkuu.
 
Kuna watubwanataka lima pilipili mbuzi wananiuliza sana habari zake lkn mimi aizifahamu sana kwani sijazilima lkn nasikia watu wanazilima Dae nadhani zinakubali. Mnaweza tfuta humu kina posts na thread za hiyo kitu jf
 
Mhhh sijui nna ukata wa matukio flani au nini ili nimependa sauti ya mwenye video🙈🙈
 
Nataka hiyo huduma ya kupimiwa udongo ili tulime kisasa km vidro ya shamba lako inavyoonyesh. Tuna wakulima wengi tu huku mvometo wanahitaji hiyo huduma
 
Back
Top Bottom