Top 4 richest people in Tanzania 2014

Top 4 richest people in Tanzania 2014

Hata kama hampendi mengi lakin sikuzote laazma tukubaliane nae kwamba serikali laazma iwatengenezee uwezo wazawa na watanzania wote wawe na uwezo wa kumiliki mali zao leo hii naigeria katika sector ya mafuta wapo wanaigeria wengi tu ni matajili wahio nishati ndio sababu kubwa wapo wengi kwenye list ya matajiri.sisi tunayo gesi serikali ingetafuta namana ya kufanya ili watanzaia hata kwa ubia wawe moja wa miliki ya rasilimali zetu.achen mengi aongee cause anajua mengi na anapakusemea na tuheshimu juhudi alizofanya kufika alipofika leo

Serikali imelifanya hilo,inamtaka kila mtanzania akanunue hisa tpdc awe mbia kwenye mafuta na gesi mengi hataki anataka apewe vyake mwenyewe.
 
FISADI ANAYETUMIA KISINGIZIO CHA UTETEZI WA WANYONGE KUZIFANYA CHUKI ZAKE BINAFSI ZIWE NI UGOMVI WA KITAIFA:

Kwa miaka mingi kumukewepo na jitihada za makusudi kabisa zinazofanywa na vyombo vya habari vya IPP kuchafua baadhi ya wizara za serikali, watu binafsi na ofisi za taasisi mbalimbali kwa malengo yao binafsi wanayo yajua wao wenyewe. Ni wazi kabisa hakuna asiyejua chuki binafsi alizonazo mmiliki wa vyombo vya habari na baadhi ya waliokuwa viongozi wandamizi wa serikali, baadhi ya mawaziri ambao bado wanaendelea kuhudumu katika serikali, watu binafsi na baadhi ya viongozi wa dini hususani kutoka dhehebu la kanisa Katoliki. Mmiliki huyu amekuwa akitumia kivuli cha utetezi wa wanyonge kuanzisha vurugu dhidi vya viongozi wa serikali kwa kuaminisha uma kwamba anatetea maslahi ya watanzania. Jambo ambalo hata siku moja halijawahi kuwa na ukweli hata kidogo. Siku zote amekuwa akitanguliza mbele maslahi yake binafsi kwa kigezo cha uzawa, kisha ya serikali na baadaye wananchi wa mwisho. Sote tunafahamu ufisadi aliokwisha wahi kuufanya kwa kivuli cha uzawa kupitia NBC, NICO, Commodity Import Support (CIS), TANPACK Industries Ltd na mengine mengi ambayo hajawahi kuyakanusha hata siku moja zaidi ya kulia lia mbele ya uma kuwa anapakaziwa.

Kama ambavyo iliwahi kutamkwa huko nyuma, historia ya Mengi inamuonyesha kwamba ni mtu anayependa kuanzisha ugomvi katika mambo yanayohusu maslahi yake binafsi lakini unapopamba moto na kuona anazidiwa, hutafuta hifadhi kwa kulia lia na kutaka aonewe huruma na kutaka kuliingiza Taifa zima. Katika kufanikisha hayo, amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari kuwapotosha wananchi ili waone anaonewa au eti anapigania maslahi yao. Hiii ina jidhihirisha wazi kutokana na mlolongo wa ugomvi aliowahi kuuanzisha dhidi ya watu mbali mbali kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe.
a)Alianzisha ugomvi na wamiliki wa vituo vya televisheni vya DTV na CTN mwaka 1994 kwa hofu tu ya kwamba watakuwa washindani wa kituo chake cha ITV na akafika hatua ya kuwazushia kwamba wanataka kumuua, akaufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

b)Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora, Mheshimiwa Wilson Masilingi, baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa Hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima. Katika kudhihirisha jinsi alivyo mtu wa chuki na visasi, kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata hashiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo.

c)Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Mheshimiwa Shamim Khan, kwa kutakiwa afute maelezo katika maji ya kunywa yanayozalishwa na kampuni yake kwamba yalikuwa ya chemchem wakati hayakuwa hivyo, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

d)Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Mazingira, Mheshimiwa Edward Lowassa, aliyemkanya Mengi asitumie nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Mazingira kuwakomoa washindani wake wa biashara kwa kuwazushia tuhuma za kuchafua mazingira na kuvifungia viwanda vyao, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

e)Akaanzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, baada ya kumnasa akikwepa kodi katika uendeshaji wa biashara yake ya bahati nasibu ya BINGO, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

f)Akaanzisha ugomvi na kampuni ya Habari Corporation iliyokuwa inaongozwa na Jenerali Ulimwengu baada ya kufichua habari za jinsi alivyoifilisi benki ya NBC, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

g)Akaanzisha ugomvi na mfanyabishara Yusuf Manji ambaye kwanza walikuwa wakigombea uendeshaji wa mchezo wa bahati nasibu, na baadaye akajenga chuki naye binafsi kwa sababu tu alifanikiwa kuusuluhisha mgogoro wa Yanga ambao Mengi ulimshinda, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

h)Akaanzisha ugomvi na Mheshimiwa Adam Malima ambaye alihoji Bungeni jinsi Mengi anavyotumia vibaya vyombo vyake vya habari kwa kutangaza habari za kujitukuza binafsi zaidi ya hata vinavyotangaza habari zinazowahusu viongozi wa kitaifa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

i)Akaanzisha ugomvi na mfanyabiashara Tanil Somaiya baada ya kumuona kijana huyo aliyekuwa wakala wa kuuza bidhaa za viwanda vyake Mengi (kabla ya kuviua mwenyewe), ameweza kujiimarisha na kupata mafanikio makubwa ya kibiashara hata kumshinda yeye Mengi, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

j)Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Lawrence Masha, kwa kuja na madai ya kutaka kuhujumiwa, akataka kuufanya ni ugomvi wa nchi nzima.

k)Akaanzisha ugomvi na Ndugu Rostam Azizi, baada ya kuona kwamba amekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, na aka ufanya ni ugomvi wa wa nchi nzima.

l)Akaanzisha ugomvi na vijana wajasiliamali wa kikundi cha Zecomedy kisa baada ya wao kugundua ana wanyonya kwenye maslahi yao kupitia mkataba wa kipuuzi aliokuwa nao dhidi yao hali iliyo pelekea wao kuvunja mkataba na kujiunga na TBC.

m)Akaanzisha ugomvi na Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Mbarawa Makame baada ya serikali kupitisha azimio la kubadili mfumo wa matangazo kutoka analojia kwenda digitali ambapo alikuwa akishinikiza watanzania wakatae kwa lengo la yeye mwenyewe kujinufaisha binafsi.

n)Ni huyu huyu Reginald Mengi amekuwa akipiga vita ya chini kwa chini kuhakikisha Tanzania haipati katiba bora kwa malengo yake binafsi na huu ni mpango mkakati anao uratibu kwa kushirikiana na UKAWA na baadhi ya balozi za kutoka nchi ya wahisani ambazo haziitakii mema nchi yetu.

o)Baada ya kuona malengo yake pamoja nay a UKAWA hayatimii akaanzisha kampeni ya hadharani kuhakikisha bunge hilo lina simama mara moja kabla ya muda wake. Hali hii ilipelekea kukemewa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge hilo maalumu Mhe Samweli Sita ambapo sasa kaanzisha ugomvi binafsi na waziri husika kwa kuhakikisha hapati nafasi kwenye vyombo vyake vya habari.

p)Na kama hiyo haitoshi, akamfadhili Ndugu Said kubenea akafungue kesi mahakamani ili kusimamisha Bunge maalumu la katiba. Na bado penyewe wakashindwa.

q)Baada ya kugaragazwa mahakamani sasa amegeuka kuwa mfadhili mkuu wa NYERERE Foundation ambayo inatumiwa kama kivuli cha kuhakikisha waliokuwa wajumbe wa tume ya katiba wana ipinga hadharani katiba pendekezwa.


r)Na siku za karibuni kaanzisha ugomvi mkali na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo baada ya kuona harakati zake za kutaka kupewa vitalu vya gesi bure kwa kigezo cha uzawa kugonga mwamba. Amesikika mara zote akitoa maelekezo maalumu kwa wahariri wa vyombo vyake vya habari kuhakikisha wana mwandika vibaya Prof. Muhongo mpaka ang’oke wizarani.

HITIMISHO:
Watanzania tuna haja na kila sababu ya kujiuliza mara mbili mbili juu ya uhalali wa mtu huyu kuamua kutumia kigezo cha utetezi wa wanyonge (uzawa) kwa minajili ya kujinufaisha yeye binafsi, familia yake pamoja na washirika wake. Ni vyema pia tuendele kujiuliza uwapi uhuru wa vyombo vya habari kama wamiliki wa vyombo vya habari wanashinikiza kuandikwa habari wanazozitaka wao hali inayo tunyima fursa watanzania haki ya kupata habari kwa usawa. Ni vyema pia tujiulize uwapi uhalali wa mmiliki huyu anayejifanya ni mzalendo ilihali ana wanyanyasa wafanyakazi wake kwa kutowapa maslahi yao kama wanavyostahili. Sasa umefika wakati watanzania tuseme hapana. Kamwe hatuwezi kukubali hili na tunatoa wito kwa serikali kuchukua hatua kali dhidi ya mmiliki huyu ambaye amekuwa akichochea vurugu na kuivuruga serikali pasipo sababu. Pia tunatoa wito kwa watanzania kupuuza ujinga na upuuzi unaofanywa na mmiliki huyu katika kuhakikisha nchi hii inakosa amani kwa maslahi yake pamoja na genge lake la wahuni.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
 
Ngoja niwakumbushe Mengi alianzisha ugomvi na Kinje Ngombare Mwiru kisa Jackline Ntuyabaliwe akawa anamuandika vibaya kijana wa watu mtafutaji kuhusu parking za ubungo mpaka jiji wamechukua lkn wamechemka pia kagombana na Kusaga na Ruge wa clouds kisa watangazaji kuhama kwake na kuhamia clouds kufuata maslahi pia kamgombanisha Lady Jay Dee na clouds bure bila sababu pia kagombana na Madame Ritta ndo maana bongo star seach mmeiona mwaka huu kisa Madame Ritta baada ya kuona kachuma vya kutosha akaona akimwage kibabu ndo kimemaind na kwenda kumtibulia Madame Ritta kwa Wafadhili
 
Wakuu Mengi ana biashara gani?METL kajipaisha tuu hana chochote wakati Bakhresa ana viwanda malawi,rwanda,uganda,msumbiji
 
Hao watatu waliotajwa ukiacha Mzee Mengi ni wanauza dawa za kulevya, deal za kifisadi, bakhresa anaingiza sukari anazoita za viwandani anauzia watu mtaani

Huyu dalali , mwizi aliyeshindikana , kila siku anagombana na mawaziri apewe upendeleo, angekuwa na vigezo asingekuwa anapiga kelele kila siku, wenzake wanapiga kazi, yeye anahangaika na miss tanzania na uzee wote
 
4. Reginald Mengi - 560 million us dollars,number 44 in Africa

3. Said Salim Bakhresa - 575 million us dollars, number 43 in Africa

2. Mohammed Dewji - 800 million us dollars,number 31 in Africa(Youngest richest African among top 50 African richest people)

1. Rostam Azizi - 0ne billion us dollars,number 26 in Africa


Source: Africa Ranking.
Ranking Interesting Facts About Africa

Sorry ni kwa mwaka 2014,nimekosea title, Moderator fanyieni marekebisho.

Aisee halafu huyo na.4 kuna jamaa alikuwa anakomaa daily hapa kwamba ana vipesa vya juice! watu wana dharau! Wengine kama siyo ka mgao ka Ruge 1m usd wangekuwa wanaisikia tuu.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja niwakumbushe Mengi alianzisha ugomvi na Kinje Ngombare Mwiru kisa Jackline Ntuyabaliwe akawa anamuandika vibaya kijana wa watu mtafutaji kuhusu parking za ubungo mpaka jiji wamechukua lkn wamechemka pia kagombana na Kusaga na Ruge wa clouds kisa watangazaji kuhama kwake na kuhamia clouds kufuata maslahi pia kamgombanisha Lady Jay Dee na clouds bure bila sababu pia kagombana na Madame Ritta ndo maana bongo star seach mmeiona mwaka huu kisa Madame Ritta baada ya kuona kachuma vya kutosha akaona akimwage kibabu ndo kimemaind na kwenda kumtibulia Madame Ritta kwa Wafadhili
weka evidence siyo kuongea tu
 
Wakuu Mengi ana biashara gani?METL kajipaisha tuu hana chochote wakati Bakhresa ana viwanda malawi,rwanda,uganda,msumbiji

Mkuu hizo ni facts,wamethibitisha bank accounts zao,viwanda,mashamba au ardhi,hisa,majumba nk wakavitathmini hadi kuandika,hajiandiki mtu,kama ingekua hivyo kila mtu angejipaisha mkuu. Huwezi kudanganya hapo.
 
That is the point...Uzawa my foot...
Nchi haiwezi endelea kwa kuwa wabaguzi...we have to be proud na yeyote anayeitwa mtanzania tajiri no matter ni wa asili gani...mwisho wa siku tunachotaka ni kodi na ajira...

Watu wanatumia neno uzawa vibaya kutafuta upendeleo ambao hauna msaada kwa mtanzania wa kawaida (zaid ya familia zao)...
1420391963271.jpg
Thank you
 
Mengi ndiyo tajiri namba moja kwa sasa hapa bongo
 
Ina maana mimi katika hiyo list sipo?haiwezekani
 
Wewe unaesema ni waarabu na wahindi ni muongo.Hao ni watanzania tu,huko watabaki ktk asili yao tu.Usipende ubaguzi usio na maana wewe.Hata marekani matajiri wakubwa wengi wanaasili ya israel lkn husikii wakinasibishwa na huko.Nyie mnaongoza kwenye ufisadi serikalini na kuibia nchi mabiliono ya fedha sio kwenye orodha zilizotukuka kwa uingizaji vipato halali.Chunguza Richmond,EPA na ESCROW nyie ndio mmeshika nafasi ya kwanza mpaka ya mwisho.Hahahaaaaaaaaaa!!!!
 
Back
Top Bottom