Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Kero yangu ni kuhusu matumizi mabaya ya barabara kwa hawa wenzetu waliojuu ya sheria..askari(polisi na na baadhi ya Jwtz).

Utakutana nao njiani wametanua tena njia unayopita wewe na wanakuja speed hukuwakikuamrisha uwapishe,mbaya zaidi hata wakiwa kwenye private cars zao. Utakuta hawana hata emergency yoyote wanawahi kazini hadi saa zingine wanasababisha ajali katika kuwakwepa wao. Hii inakera sana kwasababu sote tunataka kuwahi makazini na majumbani pia.

Ustaarabu na kuzingatia sheria barabarani ni swala la muhimu sana...sio wengine wanaovertake kwenye mataa tena taa nyekundu na Traffic police wanamuacha kisa askari mwenzao. Tunakwenda wapi? Tunajenga Taifa la aina gani?

Halafu baadae tujetujiulize tumerogwa na nani,wakati tabia mbovumbovu kama hizi tuliziruhusu wenyewe.
 
Kuna vishoka pale TRA kijitonyama kitengo cha leseni za udereva.Yaani ni rushwa tupu inaendepea Kwa wafanyakazi wa TRA.

MTU mmoja ana kuwa na karatasi za leseni kama 30, anazipitisha Kwa trafic bank lessen inatoka hapo halo. Ila walala hoi unaambiwa njoo wiki ijayo au mtandao upo chini
 
Hapa Geita bwana kuna watu ni miungu watu hasa Geita District council kwa idala ya sekondary kuna afisa elimu mmoja anaitwa George Opiyo huyo bwana ni Mungu mtu kwa sababu anahitaji walimu wamuabudu ndio wapate haki zao.

Ni maarufu sana kwa kuwahamisha watumishi kinyemela bila utaratibu maalumu na pasipo kuwalipa fedha za uhamisho, kwa kutumia mgongo wa ukaguzi wa vyeti kuna badhi ya waliimu amewaingiza katika sakata laa vyeti Fake kwa ku_edit matokeo ya nakala za vyeti alivyokuwa amekusanya mwalimu ili akaguliwe na kumkusanyia nakala zilizo badilishwa matokeo.

Jambo hilo lilimpelekea mwalimu Fredrick wa shule ya sekondary Kamuhanga kusimsmishwa kazi kwa kigezo cha kua na vyeti fake na khali ana vyeti kamili na baada ya kuvipeleka baraza la Mitihani walithibitisha kua vyeti vyake ni halali kabisa ila walipokea nakala za vyeti zilizo badilishwa matokeo.

Kibaya zaidi pamoja na raisi kupinga uwepo wa wanafunzi wenye mimba mashuleni pamoja na uwepo wa wanafunzi hewa kuna jambo moja bado hajalikumbuka.

Kuna mradi ambao anauendesha afisa elimu idala ya sekondary kwa Geita vijijini kwa kushirikiana na baadhi ya wakuu wa shule mfano ni Headmaster wa shule ya sekondary Senga bwana Magoma Komesi.

Kuna mpango wa kuwachukua na kuwasajili wanafunzi walio kosa elimu ya sekondary au walio jifungua na kuwachanganya na wanafunzi wa kawaida darasani.

Hali hii imepelekea kuwepo kwa msongamano mkubwa sana katika madarasa kiasi ambachoi mwalimu anae ingia kufundisha katika nadarasa hayo ina mlazimu kua kama mchungaji ane hudumu katika kanisa lililo jaa waumini.

Hatukatai uhuru wa mtu kupata elimu, lakini hii isiathili shughuli za ufundishaji na ni vema wanafunzi wa aina hiyo wasichanganywe na wanafunzi wa kawaida kwa sababu wengi wao ni watu wenye familia na wanatofautiana kwa kiwango kikubwa katika umli na wanafunzi wa serikali
 
Tunao utamaduni wa kutawalana ambao unaainisha kuwasilsha kero kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi juu lakini bado tumeendelea kuona wananchi wakisimamisha misafara ya viongozi hasa Rais na waziri mkuu ili kutoa kero zao na wakati mwingine kuvamiwa mikutano yao kwa mabango yenye kero mbalimbali.

Nimeonelea huenda litakuwa wazo jema nifungue uzi huu ili watu mbalimbali waweze kuorodhesha kero zao na viongozi wetu watakaolengwa na kero hizo wawe wanapitia humu mara kwa mara kuokota hili au lile linalowahusu na kulitatua kabla halijawa agenda ya kwenye mabango.

Karibuni wote, bali kero za kisiasa hapa sio mahala pake; hapa tuweke kero za kijamii na kiuchumi pekee kusukuma kurudumu la maendeleo.
 
ccm.jpg



Kero zangu nazimwaga kwa hao jamaa wa lumumba na wabunge wao hadi ngazi ya serikali ya ccm police ccm waache kutumia nguvu kuwaelimisha watanzania.ccm wametuingiza gizani hadi leo vijana awana ajira,walimu mateso,wafanyakazi mateso raia mateso hospital hakuna dawa,wanapitisha mikataba bila kusoma yaani pyuuu, huyu baba sisonje Mungu anamuona


Swissme.
 
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais, Waziri mkuu na Watanzania kwa ujumla:-
(1)kwa nini tunawaacha watu wachache wakipandikiza UKABILA, UDINI na UKANDA bila kuwakanya kwa namna ambayo hawatathubutu tena kurudia maneno hayo?
 
MHESHIMIWA Rais, naomba unipe Cheo cha UPOLISI japo kwa wiki moja tu ili niweze kufanya kazi moja tu. Kazi hiyo ni hiyo ni kumshikisha adabu mtu yeyote ambaye atathubutu kutoa LUGHA CHAFU, UCHOCHEZI, kauli zinazochochea UDINI, UKABILA na UKANDA.
Lakini pia nitamshikisha adabu yeyote ambaye atuthubutu kusambaza kauli za mtu aliyetajwa hapo juu.
Naamini mara nitakapomtia mikononi mwangu mtu /watu wa namna hiyo kwa hakika HAWATARUDIA TENA KUYATAMKA MANENO KAMA HAYO.
Mungu ambariki Rais Magufuli na serikali yake.
 
Kuna mtandao wa wezi unaoanzia dodoma kuelekea arusha na moshi .konda au dereva anampakia mtu anaejua ni mwizi na akifika babati anaingiza gari sehemu ya chakula anakojua yeye na hapo mwizi anachukua mali za abiria. ..hili lilinipata mimi tar 25 march nimepanda gari la shabiby na nilikata tkt ya mwisho no 50 nikapanda gari konda akaniambia begi langu niliweke kwenye buti nikamuambia lina laptop akaniambia shauri yako ..nikaweka begi la nguo tu.tulipofika babati wakapeleka gari kwenye hotel inayotizamana na stend hapana nafasi kubwa ya parking chini wamejaa wapigadebe na wafanyabiashara ndogondogo .nikaacha begi ndani ya gari chini ya siti nikafunika na kanga nikashuka..niliporudi begi halipo nikamfuata konda nikakuta yupo na mmiliki wa hotel.nilipomuambia silioni begi wakanijibu kuwa kuna mtu kakufuatilia toka dom ndio kakuibia ..nikarudi kwenye bus nikawauliza abiria mmoja kasema aliona mtu kaingia kapekuwa mabegi 2 kabla hajaingia kwenye siti yangu na kulichukua begi.na akasema amemfaham .nikarudi kwa konda na dereva kuwajulisha nikawaomba wanionyeshe kituo cha polis nikaripoti ..walichofanya waliacha hata ule msosi wakaingia kwenye bus while nawasubiria wanipekleke polis wakageuza gari nilipoingia wakaanza safari mbio kuelekea arusha nikawaomba wanionyeshe polis wakasema nawachelewesha wakaenda kanma km 2 nikatafuta namba ya trafic moshi nikampigia kumuomba muongozo akaongea na dereva kuwa tukifika polis post ya magugu tukatoe taarifa.tulifanikiwa kurepoti polis magugu na kusearch kwenye bus but nikawaambia polis magugu wamhoji abiria aliyeona befi likichukuliwa na walimhoji..mwisho gari liliondoka konda akinidhihaki... nikarudi babati nikaenda kufungua jadala la kuibiwa hadi leo sijapata vitu vyangu na sijui hatima yangu na wale wenye bus wanaendelea kutamba na mama mwenye hotel ananishihaki kwenye simu. Niko tayari kulisimamia na kuhojiwa ili nipate haki yangu nnaomba mheshimiwa rais na mamlaka yake husika wanisaidie kuipata haki yangu mamlaka husika wanazungusha tu.kama nilimlipa mwenye gari pesa ya kunisafirisha anapaswa kunitake care hadi nifike salama mimi na mali zangu maana anaejua kuna mtandao wa wizi ni wao basi wanapaswa kujulisha abiria .tumeshuka kwenye bus konda na mawakala walikuwepo mlangoni je anaingiaje mtu kwenye gari ambae hahusiki au ambae hawamtambui ?anajiaminije bila kuwa wanashirilkiana? Mimi naomba mnisaidie nipate haki yangu jamani miezi mitano inapita bila kujua ninafanyaje ni mimi raia mwema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jipu uchungu nimeliona hospitali ya Mwananyamala kitengo cha maabara watu wanaanza kupewa huduma saa tano. Na wakati wafanyakazi wanafika ofisini saa moja wao ni stori tu na kuacha wagonjwa wanaendelea kuzidiwa....

Mtu amepima toka jana lakini kumpa tu majibu yake asubiri hadi saa tano ndo waanze kutoa majibu....wao na stori tu ofisini
sIKU NYINGINE UKIENDA PIGA PICHA. HALAFU NENDA KAWAHOJI. THEN OMBA KUONANA NA SUPERVISOR WAO.
TUKIWAJIBIKA WOTE TUTASAIDIA
 
Habari za kazi ndugu zangu naomba wote wenye KERO/KESI za ardhi ambazo zinasababishwa na Wanasiasa(Viongozi wa kisiasa)wale wakuchaguliwa na wakuteuliwa.

TUKUTANE hapa na kusema KERO zetu na kutaja maeneo ambayo ipo hiyo KERO...... mimi naanza na DODOMA

1.KIKUYU KUSINI(Diwani anagawa mashamba ya wananchi)

2.NDACHI NA NARA(wananchi wameambiwa wamejenga maeneo ya Mwekezaji)

3.CHANG'OMBE(Mwenyekiti wa mtaa amegawa viwanja na kuwaruka baadhi ya wamiliki na kuwapa wageni/wasio wakazi wa eneo husika)

Karibuni tuchangie ili kufahamiana na wataalamu waje na ushauri wa Kitaaluma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
4. TARIME, MARA (Mwaka 2013 mgodhi wa North Mara ulifanya tathimini ya ardhi kwenye eneo linalozunguka mgodhi huo na kukata kata mazao na vitega uchumi vingine vya wananchi hao, lakini ni miaka 4 sasa hakuna aliyelipwa, cha kushangaza DC wa TARIME haeleweki kichwa kipo wapi maana kila akiitisha mkutano haonekani na akionekana huja na majibu ya kukatisha tamaa wananchi)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
4. TARIME, MARA (Mwaka 2013 mgodhi wa North Mara ulifanya tathimini ya ardhi kwenye eneo linalozunguka mgodhi huo na kukata kata mazao na vitega uchumi vingine vya wananchi hao, lakini ni miaka 4 sasa hakuna aliyelipwa, cha kushangaza DC wa TARIME haeleweki kichwa kipo wapi maana kila akiitisha mkutano haonekani na akionekana huja na majibu ya kukatisha tamaa wananchi)

Sent using Jamii Forums mobile app
Poleni sana kero zetu ndo wimbo wetu wa kudumu na chanzo cha kura zetu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kero kubwa kuliko zote ni kwanini maeneo yasiyopimwa wananchi wasiamriwe kuachia ardhi ili barabara zipanuke. Unakuta mtu ana eneo kubwa lakini kaachia kanjia kupita gari moja tuu hata pa kugeuzia hakuna wakati kaweka uzio wa miti na ndani ana eneo kubwa.

2. Bei ya kupata hati miliki kwa dsm sasa inafikia mpaka milioni 10. Je wahusika hawatambui kwamba kiwango cha mishahara kinazidi kuporomoka kwa makato makubwa ya HELSB, WCF sasa hizi hati si tutasikia kwa wahindi na waarabu na matajiri wengine. Hakuna sababu ya kuweka bei ya hati kuwa juu. Kama wanasafisha kuhusu ufisadi kila sehemu waweke bei za kizalendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom