Tofauti ya kung'aa na kujichubua

Meridah Tough

Senior Member
Nov 27, 2017
136
363
Je, kuna tofauti ipi kati ya Kung'aa na Kujichubua? Mimi ni maji ya kunde, sipendi kuwa mweupe lakini napenda kuwa na ngozi nzuri.

Nimeelekezwa kununua mafuta ya Queen Elisabeth kwamba nitang'aa. Najiuliza hii kung'aa si kuwa mweupe kweli.
 
Njia za kung'arisha ngozi mara nyingi zinakuwa ni za asili kama kunywa maji mengi,kupata muda wa kutosha wa kupumzika/kulala,usafi wa ngozi,vyakula n.k

Kujichubua ni kutumia mafuta/chochote katika ngozi ili kuitoa ngozi katika uhalisia wake

Tatizo la mafuta/lotion inategemea imekukubali vipi ili ikupendeze...hiyo queen elizabeth nasikia ni nzuri,lakini wapo watu inawakataa
 
Je kuna tofauti ipi kati ya kung'aa na kujichubua? Mimi ni maji ya kunde, sipendi kuwa mweupe lakini napenda kuwa na ngozi nzuri.
Nimeelekezwa kununua mafuta ya Queen Elisabeth kwamba nitang'aa. Najiuliza hii kung'aa si kuwa mweupe kweli!!
Sio kila mtu,mimi ilinikataa kabisa Ila ndugu yake Ever Sheen alifanya maajabu tangu 2015 mpaka leo
,
 
Kuna ngozi kungaa na kuna kujichubua. Hivyo ni vitu viwili tofauti. Kutokana na hali ya hewa, kushinda juani,upepo nk hupelekea ngozi zetu kufubaa. Ndio ile unajikuta una rangi tofauti tofauti mwilini ie ngozi ya mapaja inakuwa tofauti na ya usoni au mikononi.

Hata utumie mafuta gani ngozi yako haiwezi kung'aa kama haunywi maji ya kutosha, haupati muda wa kutosha kupumzika, una stress, huli matunda ya kutosha, huli mboga za majani, inshort huli balanced diet, unashinda juani na kwenye upepo muda mwingi,huna routine nzuri ya kutunza ngozi yako ila kubwa kuliko ukiwa hauna pesa

Mafuta ni ziada tu, hivyo hapo juu ndio vya msingi zaidi.
 
Totauti ipo Tena kubwa Sana...

Kujichubua ni ile hali ya kubadili ngozi kuondoa ngozi ya juu ..mfano Ukitumia lotion zenye hydroquinone au Mercury tegemea kubadilika kwa ngozi yako na kuisababishia athari hapo baadae.

Kun'gaa hakuchubui ngozi yako zaidi kunafanya ngozi yako kua na mn'garo zaidi ya vile ilivyokua ..unywaji juice wa nanasi..matikiti maji..carrots ..maji kwa wingi..cucumber..ulaji wa tufaa ..kupendelea kunywa green juice ..kutumia mafuta ya Nazi au olive oil hufanya ngozi yako kua na mn'gao wa kipekee.

Waweza itumia queen Elizabeth lakini Kama una ngozi yenye mafuta sikushauri uitumie usoni maana utajuta..

Nakushauri Kama una ngozi yenye mafuta queen Elizabeth pakaa mwilini ..usoni pakaa mafuta ya Nazi changanya na orange/ lavender essential oil.

Au Kama wataka kuapply queen Elizabeth mwili mzima tafuta carrot essential oil changanya...utajipenda my dear.
 
Back
Top Bottom