Tofauti ya jehanum na kuzimu

Tofauti ya jehanum na kuzimu

.
downloadfile-27.jpeg


Jr[emoji769]
 
Mshana ngoja Nile nitakuja kuisoma
Nmesoma heading to[emoji4][emoji4]

kelphin kepph
 
Kwa hiyo kwa kuwa kiama bado mbinguni na jehanam ni kutupu hakuna watu. Watu wote wako kuzimu, sio?
kwa hiyo watenda dhambi na wasio na dhambi wanakutana kuzimi wakisubiri kiama wahukumiwe!
 
mkuu haya maelezo yako sipingani nayo nakubaliana nayo asilimia 100
kuna mtumishi aliwahi toa maelezo exactly kama hayo
LAKINI YEYE ALISEMA HIVI ... KUZIMU ZIPO MBILI
KUNA KUZIMU YA IBILISI (KAMA WEWE ULIKUA MTENDA DHAMBI HAPA)
UKIFA UNAENDA KUKUTANA NA NDUGU YAKO ULIEKUA UNAMFANYIA
KAZI. HAPO PIA KUNA MATESO MAKALI SANA LAKINI HAYA NI MATESO
UNAYOPEWA NA IBILISI NA MALAIKA ZAKE .. HAPA NI KABLA
HUJAENDA JEHANAMU AMBAKO KULIANDALIWA MAALUMU
KWAAJILI YA IBILISI . IBILIS MWENYEWE YUPO KUZIMU HUKO
AKISUBIRI KWENDA JEHANAMU KWENYE ZIWA LA MOTO

NADHANI WANAPOSEMAGA MTU APUNGUZIWE ADHABU YA KABURI
NDO INAWAHUSU HAWA NDUGU. (SIJUI SINA UHAKIKA)


KUZIMU NYINGINE NI YA WALIOTUBU NA KUSAMEHEWA KABLA HAWAJAFA.
HAWA WANASTAREHE HUKO WALIPO (IMANI) WANASUBIRI HUKUMU
ILI WAENDE WANAKOSTAHILI

HILI SWALA LIPO KWENYE BIBLIA NIMESAHAU TU MISTARI


NA MUNGU AWABARIKI SANA
Sasa kama tayari washukumiwa kuwa wataenda kula raha(Peponi), kwani wasiende mapema wakati hukumu imeshajua kuwa hawana hatia? Ni sawa na kusema hata mahakama ikikukuta huna hatia hutoki/huachiwi mpaka na Seth au Kabendera nao hukumu zao zitoke. Kama hana dhambi atangulie tu kula raha hawa wengine hata wakitusubiria hakuna shida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali langu ni kwanini wasio na hatia(Waliotubu kabla ya kufa) wasitangulie kula raha mpaka na wao watusubirie sisi ? Ni sawa na mahakama imekukuta huna hatia ila inasema ubaki ndani mpaka Seth au Kabendera hukumu yake itoke. Au kwa kuwa ni mambo ya kiroho
Yes rakini zaidi ya segelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walioko mbinguni sio Binadamu
Kwa hiyo kwa kuwa kiama bado mbinguni na jehanam ni kutupu hakuna watu. Watu wote wako kuzimu, sio?
kwa hiyo watenda dhambi na wasio na dhambi wanakutana kuzimi wakisubiri kiama wahukumiwe!

Jr[emoji769]
 
Wamepumzika kuzimu wakisubiri kiama
Swali langu ni kwanini wasio na hatia(Waliotubu kabla ya kufa) wasitangulie kula raha mpaka na wao watusubirie sisi ? Ni sawa na mahakama imekukuta huna hatia ila inasema ubaki ndani mpaka Seth au Kabendera hukumu yake itoke. Au kwa kuwa ni mambo ya kiroho

Sent using Jamii Forums mobile app

Jr[emoji769]
 
Mshana Jr, kwa kumbukumbu zangu ni kwamba sababu ya yesu kushuka kuzimu ni kwenda kuchukua funguo za kuzimu.
Sio funguo za kuzimu,alikwenda kuchukua funguo za mamlaka ambayo shetani alikuwa nayo,ata katika zile siku arobaini zakufunga kwake shetani alimjaribu kwa kumuonyesha fahari yote ya Dunia nakumwambia iko chini yake. nakutaka asujudiwe ili amkabidhi hiyo mamlaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sometimes huwa siamini haya mambo ila wakati mwingine naamini,kama kweli Mungu yupo na katuumba akijua tutamkosa na kila baya alilitambua kabla ya hata sisi kuwapo basi kwanini akupe adhabu siku ya mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma nikitafuta EVIDENCES zozote au REFERENCES . HAMNA. JF ya miaka hii inapwaya sana. Mtu anaweza akakaa akishashiba akajawa na wahyi au ndoto ambazo zinakuwa kavu akaja akaandika uzi kama ndo facts. Na watu wakakubali tu hivyo hivyo hawajui hata kuhoji.

Katika maandishi ya kitaaluma au ujengaji hoja huwa kuna reference. Kuna rejea. Wewe hujatumia Kuran wala Biblia. Ila umewaza ukawaandikia watu ambao nao sababu hawapendi kuwaza wanapokea kama ilivyo.

Hii ni shida.
Unajuaje mtu hawezi enda kuzimu? Unajuaje mtu anayekufa anakuwa kuzimu?
Hivyo hamna tofauti ya mtenda mema na mtenda maovu wote wakifa wanaenda kuzimu?
Huko wanafanya nini?
Wanaishi maisha gani?
Uthibitisho wa hayo yote ni nini?

Kama Shetani yupo kuzimu muda huu na wanaokufa wakiwa wametenda mema wanaenda kaa naye kuzimu? Wakifanya nini?

Kuna watu huwa wanakula kirahisi matango pori unayowalisha Mimi sipo hivyo. Nisaidie hayo maswali then tupeane darsa hapa.
 
Habarini wapenzi wa jukwaa hili....tulipoteana kidogo lakini naamini kila mmoja wetu ana siha njema...nawaombea afya tele na furaha pia

Wengi wetu kama si kwa uchache basi kwa wingi tunachanganya matumizi ya haya maneno mawili...JEHANUM NA KUZIMU
haya maneno mawili yako kiroho zaidi, kiimani zaidi japo ukiyachukua kwa tafsiri nyingine mbadala yanazungumzika kiuhalisia

JEHANUM ni motoni...kwamba wale wote wafao wakiwa na dhambi na hawakutubia makosa yao wanaenda kwenye moto wakatupwe huko kwenye kila aina ya tabu mateso na ukatili wa aina zote....Lakini kiuhalisia wafu hawajafika jehanum bado wako kuzimu wakisubiri hukumu
KUZIMU sio JEHANUM ,kuzimu ni kaburini...ni sehemu wakaapo wafu ni makazi ya muda wakati wa kusubiri kiama na hukumu kuu....kuzimu no lango na mapito ya wafu kuelekea jehanum au peponi
Waendao kuzimu ni wafu,huwezi kufika kuzimu kama wewe si mfu...waendao kuzimu wana nafasi ya kurudi (sio duniani), waendao jehanum hawarudi....anayekwambia alifika kuzimu na kurudi si mkweli ,huyo alifika mpaka langoni lakini hakuingia ....kwa maneno mengine wanasema alichungulia kaburi....
Kwenye imani ya Kikristo kuna maneno yanasema hivi....AKAFA AKAZIKWA AKASHUKA KUZIMU....siku ya tatu akafufuka (dhana ya kurudi toka kuzimu)akapaa mbunguni (hakurudi na kukaa duniani)
Huwezi kufika jehanum bila kupitia kuzimu...hiyo ndio ya kuelekea motoni hivyo huwezi iruka abadan!...Kama ilivyo tafsiri ya wengi mbingu ni juu ,kuzimu ni chini....lakini jehamun iko pande zote ,haikwepeki ,haikimbiliki....unaweza kukwepa kwenda mbinguni lakini sio jehanum na njia ya kufika huko ni kupitia kuzimu tena ukiwa mfu [emoji1562][emoji1562][emoji1562][emoji1562][emoji1562]weird phenomenon...

Tunapofanya ibada za kuwaombea wafu ili wasiende motoni bali peponi zile ni ibada tu za faraja na kuzuia roho hizo za wafu zisitangetange(dhana ya jehanum) bali zibaki kaburini (dhana ya pepo).... ...Ndugu zetu waliotangulia wako kwenye pepo na jehanum za muda tuu kwakuwa kiama bado....na kwa tafsiri ya hakika...kuzimu kupo na jehanum ipo...milki ya kuzimu ipo na milki ya jehanum ipo....na vitu viwili tofauti japo vinafanana kwakuwa tu kiasili chake ni WAFU
Umeanza tena
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom