Tofauti ya Dini katika mapenzi

Tofauti ya Dini katika mapenzi

Kwangu mie nikipendana na wa dini tofauti na yangu nabadili tu kwa ajili yake kama akitaka

Huwa naamini Mungu ni mmoja
Mungu wa waislam na Mungu wa wakristo na mungu wa budha sio sawa,usijitoe ufahamu kisa ndoa
 
Katika haya maisha nimeamini kuwa watu huzaliwa waliwa very pure, innocent na bila ubaguzi wowote ila jamii ndio huwabadilisha kwa kuwalisha mawazo ya kibaguzi.

Imagine leo huyu dada anaacha penzi ambalo ni la uhakika ili tu kuwafurahisha wazazi wake au jamii yake bila kujijua.

Mwisho wa siku hiyo yote inageuka kuwa tatizo ambalo hata halikutakiwa kuwapo.
Kuna watu wazima hawataki kutumia Ubongo wao kabisa,wao akili zao zote wameziweka kwenye maandishi ya Dini mwisho wa siku wanaonekana Kama kituko fulani hivi kwa Jamii!!
 
Kuna watu wazima hawataki kutumia Ubongo wao kabisa,wao akili zao zote wameziweka kwenye maandishi ya Dini mwisho wa siku wanaonekana Kama kituko fulani hivi kwa Jamii!!
Kwaiyo...kushikilia msimamo wa dini nikuwa kituko katika jamii... BASI NA IWE HIVYO
 
Katika haya maisha nimeamini kuwa watu huzaliwa waliwa very pure, innocent na bila ubaguzi wowote ila jamii ndio huwabadilisha kwa kuwalisha mawazo ya kibaguzi.

Imagine leo huyu dada anaacha penzi ambalo ni la uhakika ili tu kuwafurahisha wazazi wake au jamii yake bila kujijua.

Mwisho wa siku hiyo yote inageuka kuwa tatizo ambalo hata halikutakiwa kuwapo.
Sio kuwafurahisha wazazi... Bali Ni imani yangu Mimi binafsi hainiruhusu.....Mafundisho yangu yangu ya dini yanakataza
 
Mapenzi Ni mazuri Sana, unakutana na mtu mnapendana unaona kabisa yaani penzi Lina flow bila hata nguvu ya ziada.
Lakini tatizo Dini. Unaona kabisa Dini Ni kikwazo, Mimi katu Siwezi badili Dini yangu. Mwenzangu analazimisha nibadili...

Naona penzi langu tamu,zuri na maridhawa linakaribia mwisho. Inasikitisha Sana. Swali nimeulizwa, kwanini uliacha penzi lichipue namna hi Kama ulijua tangu mwanzo kuwa halina future. Jibu ninalo ila kapuni.
Kwani unamfuata Mungu yupi anayeruhusu zinaa?
 
Nyenyere tunakujua wewe Ni mtu wa Mungu..Hebu tuambie huko kwenye wokovu Ni ukamilifu?..Huko kwenye kumjua Mungu Ni kwa watakatifu?

Maana ya kutubu Ni Nini?..Usipende Sana kuona boriti za wenzanko.
 
Don't compromise your faith for any thing.
Religion first always and forever.
BTW hakuna ndoa ya muislamu na mkristo.
Hapa ndo huwa tunakosea..family is always first

Huo ujinga wa religion first Ndomaana baadhi ya dini baba anamuua mtoto wake kisa ameacha dini...madness and barbarianism
 
Pole sana Dada..ni wachache sana wanaojitambua kiimani na wakawa tayari kufanya maamuzi kwaajili ya ya imani na sio mapenzi.
Ukikuta mtu kaingia kwenye mapenzi na mtu tofauti na imani yake halafu baadaye anasema kwani Mungu si yuleyule jua huyo ni mtu hatari sana...ingawa anaweza badirika wakati fulani..probably..
Lakini endapo umempata mwenzi tofauti na imani yako na ukatumia muda kwa siri kunifunza na kujua juu ya imani yake na ukaielewa vizuri not hear say (sio perception uliyopandikizwa juu ya hiyo imani noo..but yale uliyojifunza kwa kina na kwa unyenyekevu)..utafanya2 maamuzi sahihi ..ukiamua kumfuata Unamfuata kwa kuwa una hakika bila ya shaka kuwa naenda au nimepata njia sahihi au mwanga fulani kuliko awali.

Na kwa vyovyote vile Utakuja kuipenda mno hiyo imani na kuwa muumini mzuri na mwaminifu zaidi ya uliowakuta sababu tuu umeijua hiyo imani vyema.

Ukitazama hata baadhi ya mabishano ya kiimani katika jamii zetu simply ni kwa sababu wengi hawazijui vizuri imani zao wanazoamini ingawa wao wanaamini kuwa wazijua...na pia hawajui kabisa juu ya imani ya wanayebishana naye zaidi ya kusikia kusikia na kuambiwa negativity ya hiyo imani..na vifungu au viushahidi viwili vitatu vya kuokoteza ili kuhalalisha anachokipinga dhidi ya imani nyingine.

Kama watu wengi wangekuwa na tamaduni za kujifunza imani za wengine kama njia ya kuongeza Elimu tuu...religious knowledge..Duniani tungeishi kwa upendo na kuheshimiana sana sana.

Hata kama baada ya kujifunza hizo imani kwa kina za wenzetu na kuona kuna mapungufu basi namna ya kusaidiana na kuelimishana Ingekuwa ni ya upendo mno mno wala dharau..kiburi..jeuri..majigambo visingekuwepo bali hekima na akili ingetawala na busara kuamua kwa adili kila tuzungumziapo mambo ya imani na wale tunaotofautiana nao.

Kwa sababu wengi wetu mbali ya kwamba tumejifunza sana labda mpaka tukakielewa tunachokiamini na kuwa ndio sahihi kuliko anachoamini mwingine...
Lakini ukweli unabaki pale pale..unaamini katika Dini yako kwa sababu za kijiografia tuu..ungezaliwa kule lazima ungejikuwa wewe ni muislam..au ungezaliwa kule automatically ungekuwa mkristo no matter what au umejifunza dini yako kiasi gani.

So why malumbano ya Din I????
Nakushauri uamue juu ya imani yako au yake kwa kuwa umejifunza zote mbili..nyingine kwa kuzaliwa automatically ukaijua kupitia malezi na nyingine kupitia incidence ya mahusiano au ulishaijua vyema kabla.sio kwa kusikia kupitia dini yako ilivyokufunza hapana bali uliijua wewe mwenyewe kwa kunifunza juu yake.

Muoane au msioane bado mtaheshimiana..kuliko kikwazo cha dini kikamfanya mmojawapo adharau hata imani nyingine zote kupitia malumbano yenu yaliyosababishwa na mapenzi.

Wote wawili mlikua hamzijui kabisa kabisa hizo imani zenu mnazoziamini ndio maana mliamua mkiwa na akili timamu kuwa uzinzi ndio jambo la kwanza kwenu...halafu unasema kupitia uzinzi ndipo mapenzi yakachanua mpaka kuanza kuhisi au kuamua juu ya nia ya kuishi kama wanandoa..ni ajabu sana sana.

Huu msimamo wa kiimani mlio nao ungeanza kabla hata hamjaanza mahusiano yeyote..mmeshatiana mihuri isiyofutika mioyoni na rohoni mwenu eti ndio mnashtuka leo.

Kama tunazo imani na tunaziamini kweli na tupo tayari hata kufa kwaajili4 hiyo ziwe zinatufanya tuamue mapema na kwa wakati sio baada ya dhambi..

Best wish katika safari yako ya kumpata mwenzi wa maisha...
Samahani samahani mniwie radhi kwa lecture ndefu tena isiyo na maana..

Nawaombeni radhi nyote mliokwazwa nami...
Well said mkuu.
 
Back
Top Bottom