Tofauti niliyoiona ya DC na AC

Tofauti niliyoiona ya DC na AC

Ok9

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Posts
4,556
Reaction score
4,169
Kitambo sana nimekuwa na maswali juu ya tofauti ya dc (direct current) na ac (alternate current) .

1.Mara nyingi dc ikisafir umbal hata wa mita 10 na waya mdogo haiwez kUwasha hata taa angali ac inawasha kwa waya huo huo.

2.Dc inaozesha waya kama ni mdogo angali ac haiozeshi.

3. Hasi ukiweka kwenye chanya kifaa husika kinaungua au hakifanyi kaz isipokuwakwa baaadh ya taa while Ac hata ukichangaya N iende L mzigo unapigwa tuu.

4. Ili DC isafir vizuri lazma ipite kwenye waya mkubwa.

5 Je kuna transfomer za kukuza DC?

Je haya ni kwann yapo hivi?
 
kitambo sana nimekuwa na maswali juu ya tofauti ya dc (direct current) na ac (alternate current)
1.Mara nyingi dc ikisafir umbal hata wa mita 10 na waya mdogo haiwez kUwasha hata taa angali ac inawasha kwa waya huo huo.
2.Dc inaozesha waya kama ni mdogo angali ac haiozeshi.
3.hasi ukiweka kwenye chanya kifaa husika kinaungua au hakifanyi kaz isipokuwakwa baaadh ya taa while Ac hata ukichangaya N iende L mzigo unapigwa tuu.
4. Ili DC isafir vizuri lazma ipite kwenye waya mkubwa.
5 je kuna transfomer za kukuza DC?
Je haya ni kwann yapo hivi?
Kitu pekee nilichogundua kutoka kwako ni kwamba unakosa (hauna) elimu ya umeme lakini ni mdadisi, na kwa hili la pili nakupongeza. Kutokana na kukosa ufahamu wa msingi wa umeme (basic knowledge), inawezekana ukipewa majibu ya hayo maswali yako ukayakariri kama yalivyo, lakini mimi huwa sipendi sana kukaririsha, huwa napenda mtu aelewe basics halafu aje awe mbunifu (sio mtundu).
Baadhi ya majibu ya ujumla (siwezi kwenda kiufundi kwa level yako) ni hivi:
1. Ulitakiwa useme POWER uliyoitumia kusafirishia AC ndio ile ile uliyoitumia kusafirishia DC. Theory zinaonyesha DC inasababisha power loss chache kulinganisha na AC, so maelezo yako yanapingana na theory za umeme
2. Hiyo ya kuozesha waya pia ulitakiwa ueleze mazingira yake. Mfano, inawezekana chanzo chako cha AC ulikichukulia kutoka katika socket ya umeme ya TANESCO, wakati labda DC uliichukulia katika battery yako ya nyumbani ambayo inacontain chemicals. Bila shaka unajua battery kama vile za gari huwa zinacontain acid, na hata dry cells huwa zina undergo chemical reactions. Sasa kama hizo kemikali za battery ndizo zilizosababisha waya ukaoza, hapo haustaili kusema DC ndio imeozesha.
3. Unapotumia umeme, ni vyema ukajua aina ya power supply ya load yako; AC au DC. Hata hiyo AC ukiisupply kwenye load iliyotengenezwa kupokea DC, haitafanya kazi au itaunguza kabisa
4. Hakuna ushahidi wa kisayansi unaoonyesha kuwa ili DC isafir vizuri lazma ipite kwenye waya mkubwa. DC ni nzuri kusafirisha kwani inapoteza umeme mchache, ila vifaa vyake ni gharama kubwa ndio maana AC huwa inatumika mara nyingi
5. Transformer linafanya kazi kwa misingi ya changing magnetic field. Kitu kama hicho hakipo katika DC. Hakuna DC transformers, ila kuna DC to DC converters
 
Nashkuru mkuu ila kuna sehemu umejin tofaut na swali

1.nasafirisha dc 10mt from source kwa waya mdogo na taa ya wattt 1 hawaki ila niki change waya niweke mkubwa wa 1.5mm. Unawasha taa vizuri.

2 nimefunga solar ya watt 100. Waya nilitumia ni mdogo baadae nikakuta ndani una kitu kama unga na umekatika.. Nikaambiwa DC ina carbon ndo maana waya umeoza.

3 hapo niliface kwenye kuchanganya terminals.
Kwenye DC kuna - na+. Sehem ya - uweke + na + weka -.lazma kifaa kiungue au kisifanye kazi.
In DC kuna N, L& Earth.
Sehem ya N uweke L na sehem ya L uweke N. kifaa kitaendelea kufanya kaz.

4. Kuna STEP UP TRANSFOREMER for DC? AU kuna uwezekano wa kutengeneza?

Talking from experience
 
kitambo sana nimekuwa na maswali juu ya tofauti ya dc (direct current) na ac (alternate current)

1.Mara nyingi dc ikisafir umbal hata wa mita 10 na waya mdogo haiwez kUwasha hata taa angali ac inawasha kwa waya huo huo.

2.Dc inaozesha waya kama ni mdogo angali ac haiozeshi.

3.hasi ukiweka kwenye chanya kifaa husika kinaungua au hakifanyi kaz isipokuwakwa baaadh ya taa while Ac hata ukichangaya N iende L mzigo unapigwa tuu.

4. Ili DC isafir vizuri lazma ipite kwenye waya mkubwa.

5 je kuna transfomer za kukuza DC?

Je haya ni kwann yapo hivi?

MAJIBU YAKO HIVI....

hakuna transformer ya kuDeal na DC. ili DC iweze kushughulikiwa na transfomer ni lazima ipelekwe kwenye AC kwanza ndio ichakatwe then irudishwe kwenye DC. Hivyo DC inakuwa INVERTED (Kwa kutumia Inverter) to AC then inachakatwa na transformer.

KWANINI TRANSFOMER HAICHAKATI DC?

Kwa sababu transfomer inategemea MAGNETIC FIELD CHANGES ili kusafirisha umeme kutoka COIL ya primary kwenda COIL ya secondary. Kwa ufupi iNVERTER circuit inachofanya ni kuubadilisha huu mkondo mnyoofu kuwa na frequency, yaani DC inaVunjwa vunjwa katika vipande vidogo vidogo , na kusafiri haraka hata ka.

Badala ya DC kuwa hivi ___________ inakuwa hivi -----------------

sasa hayo mapengo yanayotengenezwa ndiyo yanayoleta MAGNETIC FILDS CHANGES katika Coils za Transformer.
 
Nashkuru ymollel kwa majib mazur ya no 5
 
Last edited by a moderator:
Kuhusu swali namba 3.

AC haina chanya wala hasi. Waya zote 2 zinapokezana , waya A ukiwa chanya basi Waya B unakuwa hasi. Na waya A ukiwa hasi waya B unakuwa chanya. Yote hayo yanafanyika kwa haraka haraka kwa kasi ya mara 60 hadi mara 50 kwa sekunde moja. Na hiyo ndio inaitwa frequency (50-60Hz).

Vifaa vingi vinatumia AC kwa sababu AC nirahisi kuchakatwa, kuliko DC. Na endapo utatumia DC kwenye kifaa chenye Transformer , basi transofmer itaungua kwa sababu DC haina frequency hivyo hakutakuwa na magnetic changes kwenye coil ya transfomer ,

Badala yake kutakuwa na steady/constant Magnet na pia kiasi kikubwa chanumeme uliobaki utabadilishwa kuwa nishati ya joto ambapo joto hilo likizidi transofmer itaungua.
 
Well mkuu nimevuna vingi.
Ni kwa nn wanasema DC ngumu kuliko ac.? While AC appliance zina transformer ambayo inachange AC - DC?
 
Labda cha kuongezea ndugu Kapwila ni ivi Dc haiwezi ku transformed katika different voltage or current level Ndo mana hatuitumii ktk kusafirisha umeme masafa ya mbali kwani Current itakuwa kubwa na kupelekea kuhitaji cables zenye cross sectional area kubwa kwa ajili ya kubeba current hio kubwa ila kwa AC unaona namna cable zilivyondogo ambazo zinabeba power kubwa nini kinafanyika Transformer inakuza voltage kitendo ambacho kitaipunguza current but power will remain constant kama tukipunguza current na kukuza voltage hivo itatupelekea kuwa na conductor zenye ukubwa kidogo ambazo zitabeba high voltage low current na kupunguza line losses kwa mantiki hio tutapeleka umeme mbali kabisa
 
Uko sawa na investigation zangu.
 
Last edited by a moderator:
Kuhusu swali namba 3.

AC haina chanya wala hasi. Waya zote 2 zinapokezana , waya A ukiwa chanya basi Waya B unakuwa hasi. Na waya A ukiwa hasi waya B unakuwa chanya. Yote hayo yanafanyika kwa haraka haraka kwa kasi ya mara 60 hadi mara 50 kwa sekunde moja. Na hiyo ndio inaitwa frequency (50-60Hz).

Vifaa vingi vinatumia AC kwa sababu AC nirahisi kuchakatwa, kuliko DC. Na endapo utatumia DC kwenye kifaa chenye Transformer , basi transofmer itaungua kwa sababu DC haina frequency hivyo hakutakuwa na magnetic changes kwenye coil ya transfomer ,

Badala yake kutakuwa na steady/constant Magnet na pia kiasi kikubwa chanumeme uliobaki utabadilishwa kuwa nishati ya joto ambapo joto hilo likizidi transofmer itaungua.

Mzee wa Fiscalization
 
Well mkuu nimevuna vingi.
Ni kwa nn wanasema DC ngumu kuliko ac.? While AC appliance zina transformer ambayo inachange AC - DC?

Ni rahisi sana ku-Deal na AC kuliko DC. kwa mantiki hiyo ni rahisi pia kupunguza ama kuongeza umeme ulio katika mfumo wa AC. Simply kwasababu Transformer zinafanya kazi na AC moja kwa moja bila kuhitaji uchanganuaji wowote.

Kifaa kinachopokea AC lakini kinahitaji DC ili kufanya kazi , kinakuwa na RECTIFIER inayobadili AC kuwa DC , lakini baada ya AC kupunguzwa na transformer.

Kwa mfano; Subwoofer inapokea AC ~220V , lakini kiasi kinachohitajika na subwoofer ni DC -- 24V.

Kitakachofanyika, AC ~220 V itapokelewa na transformer, itapoozwa hadi AC ~24V , itapitishwa kwenye RECTIFIER na itabadilishwa kuwa DC-- 24V , itapitishwa kwenye Filter (Capacitor) ili kunyooshwa na kuelekea kwenye components zingine kama vile Voltage regulators, etc etc
 
Ongera kwa kujitahidi, kwa kifupi, 1.hakuna umeme unaoozesha waya, hizo ni waya feki 2. Ukubwa wa waya hutegemea kiasi cha mzigo na umbali. Hakuna transformer ya DC kama wachangiaji wengine walivyo sema.
 
Kitu pekee nilichogundua kutoka kwako ni kwamba unakosa 6(hauna) elimu ya umeme lakini ni mdadisi, na kwa hili la pili nakupongeza. Kutokana na kukosa ufahamu wa msingi wa umeme (basic knowledge), inawezekana ukipewa majibu ya hayo maswali yako ukayakariri kama yalivyo, lakini mimi huwa sipendi sana kukaririsha, huwa napenda mtu aelewe basics halafu aje awe mbunifu (sio mtundu).
Baadhi ya majibu ya ujumla (siwezi kwenda kiufundi kwa level yako) ni hivi:
1. Ulitakiwa useme POWER uliyoitumia kusafirishia AC ndio ile ile uliyoitumia kusafirishia DC. Theory zinaonyesha DC inasababisha power loss chache kulinganisha na AC, so maelezo yako yanapingana na theory za umeme
2. Hiyo ya kuozesha waya pia ulitakiwa ueleze mazingira yake. Mfano, inawezekana chanzo chako cha AC ulikichukulia kutoka katika socket ya umeme ya TANESCO, wakati labda DC uliichukulia katika battery yako ya nyumbani ambayo inacontain chemicals. Bila shaka unajua battery kama vile za gari huwa zinacontain acid, na hata dry cells huwa zina undergo chemical reactions. Sasa kama hizo kemikali za battery ndizo zilizosababisha waya ukaoza, hapo haustaili kusema DC ndio imeozesha.
3. Unapotumia umeme, ni vyema ukajua aina ya power supply ya load yako; AC au DC. Hata hiyo AC ukiisupply kwenye load iliyotengenezwa kupokea DC, haitafanya kazi au itaunguza kabisa
4. Hakuna ushahidi wa kisayansi unaoonyesha kuwa ili DC isafir vizuri lazma ipite kwenye waya mkubwa. DC ni nzuri kusafirisha kwani inapoteza umeme mchache, ila vifaa vyake ni gharama kubwa ndio maana AC huwa inatumika mara nyingi
5. Transformer linafanya kazi kwa misingi ya changing magnetic field. Kitu kama hicho hakipo katika DC. Hakuna DC transformers, ila kuna DC to DC converters
Khaa!! Chief Hiyo namba 2 inawezekana kabisa, labda maelezo yake ndiyo hayajaeleweka. Njia moja wapo ya kuzuia kulika/kutu kwenye metalic structures ambazo zipo kwenye mazingira ya maji, chumvi na hewa ya oksijeni kama mabomba, reli, meli au hata majengo yaliojengwa kwa metali ni matumizi ya umeme wa dc. Kinachofanyika ni kulazimisha kitu unachokilinda na kutu ni kukifanya kiwe hasi (cathode) zaidi kisha kuhamishia uharibifu huo kwenye kitu (anode) kingine ambacho ni rahisi kukibadilisha kikiharibika. Kumbuka electolysis kwenye kemia ya form1. Huu mfumo unaitwa cathodic protection :mvutaji:
 
Ongera kwa kujitahidi, kwa kifupi, 1.hakuna umeme unaoozesha waya, hizo ni waya feki 2. Ukubwa wa waya hutegemea kiasi cha mzigo na umbali. Hakuna transformer ya DC kama wachangiaji wengine walivyo sema.
Khaa!! Kiongozi ukienda deep utakuja kuona umeme wa dc unaozesha waya. Kuoza kwa wire ni kupata kutu au kupungua (decaying) kwenye upande wa chanya. Ndiyo maana wire za dc huwa ni flexible copper na huwa nyembamba na nyingi au zinakuwa tinned copper. Jikumbushe ionic movement/reaction kwenye metal ukipitisha umeme wa dc 😎
 
  • Thanks
Reactions: me1

Yaaap hicho nlicho kiona maana hata nyayq nzuri za DC ni hizo zenye ndogo ndogo nying kwa ndan na huuzwa ghal sana .
Huwa sio kama hizi za AC za wiring
 
Chopper kwa DC inafanya kazi sawa na Transformer kwa AC ila tofauti ni kwamba Chopper haziwez kutransform power.
 
Kiongozi umenichanganya hapokwenye kutransform power. Sijaelewa 😎
 
Ngoja nitulie nikuze knowledge yangu ya electronics hapa
 
Uzi umesahaulika....
 
Kitu pekee nilichogundua kutoka kwako ni kwamba unakosa (hauna) elimu ya umeme lakini ni mdadisi, na kwa hili la pili nakupongeza. Kutokana na kukosa ufahamu wa msingi wa umeme (basic knowledge), inawezekana ukipewa majibu ya hayo maswali yako ukayakariri kama yalivyo, lakini mimi huwa sipendi sana kukaririsha, huwa napenda mtu aelewe basics halafu aje awe mbunifu (sio mtundu).
Baadhi ya majibu ya ujumla (siwezi kwenda kiufundi kwa level yako) ni hivi:
1. Ulitakiwa useme POWER uliyoitumia kusafirishia AC ndio ile ile uliyoitumia kusafirishia DC. Theory zinaonyesha DC inasababisha power loss chache kulinganisha na AC, so maelezo yako yanapingana na theory za umeme
2. Hiyo ya kuozesha waya pia ulitakiwa ueleze mazingira yake. Mfano, inawezekana chanzo chako cha AC ulikichukulia kutoka katika socket ya umeme ya TANESCO, wakati labda DC uliichukulia katika battery yako ya nyumbani ambayo inacontain chemicals. Bila shaka unajua battery kama vile za gari huwa zinacontain acid, na hata dry cells huwa zina undergo chemical reactions. Sasa kama hizo kemikali za battery ndizo zilizosababisha waya ukaoza, hapo haustaili kusema DC ndio imeozesha.
3. Unapotumia umeme, ni vyema ukajua aina ya power supply ya load yako; AC au DC. Hata hiyo AC ukiisupply kwenye load iliyotengenezwa kupokea DC, haitafanya kazi au itaunguza kabisa
4. Hakuna ushahidi wa kisayansi unaoonyesha kuwa ili DC isafir vizuri lazma ipite kwenye waya mkubwa. DC ni nzuri kusafirisha kwani inapoteza umeme mchache, ila vifaa vyake ni gharama kubwa ndio maana AC huwa inatumika mara nyingi
5. Transformer linafanya kazi kwa misingi ya changing magnetic field. Kitu kama hicho hakipo katika DC. Hakuna DC transformers, ila kuna DC to DC converters
DC TO DC converter?
 
Back
Top Bottom