Kama hujajenga pitia hapa usifanye makosa kwenye wiring yako

Hondelo

Senior Member
Nov 13, 2017
155
238
Uhakika wa nishati ya umeme katika nyumba ni jambo muhimu kila mmoja anafaham hilo; Tunajua namna gani nishati hii imekua sio ya uhakika wakati mwngne, kwa kuzngatia hilo nikupe wazo wakati unajenga nyumba yako kukabiliana na hiyo hali ili isikuletee usumbufu siku za mbeleni.

Kuna namna mbili unaweza kuzitumia;
1. Kama vifaa vyako vinatumia mkondo mnyoofu (DC) basi utahitaji kusuka wiring ya solar itakayojitegemea tofauti na ile ya umeme wa kawaida (AC), hapa maana yake kuanzia taa itabidi ufunge mbilimbili kila chumba, moja ya umeme na moja ya solar , kwa upande wa vifaa kama redio, TV n.k, hakikisha unapokinunua kifaa husika kina mfumo wa DC na AC,, siku hizi vifaa vingi viko hivo ni wewe tu kuchagua.

Katika mfumo huu utahitaji ku install power station (battery, charge control n.k) karibu na mahali ambapo vifaa kama TV &Radio na vifaa vinavyohitaji current nyingi vitakapokaa.

Pointi kubwa hapo ni kwamba umeme wa mkondo mnyoofu hupotea kwa wingi kwa sababu husafiri katika voltage za chini kwa hivo current huwa kubwa hivo kupelekea umeme mwingi kubadilishwa kuwa joto kutokana na ukinzani wa vipitishi(conductor).

Kwa hivo inatakiwa distance kati ya chanzo na kitumiaji kuwa ndogo sana as well as possible huku ukitumia waya nene zisizo na ukinzani mkubwa kama shaba.

Hasara ya hii design ni kwamba kwanza mpangilio wa power station unaweza kukuhaibia mwonekano wa sebule yako mfano, kwa Sababu kitu kama TV kinakaa katka sebule na kwa sababu hakutakiwi kuwepo umbali mrefu kati ya chanzo na hiyo TV yako basi itabidi battery na vifaa vyake vikae hapohapo sebuleni (utakua umenielewa) lakini kama utaona una namna unaweza ku design vitu vkakaa poa ni wewe tuu.

Hasara ya pili huu mfumo unatumia gharama kubwa wakati ufanisi wake ni mdogo. Nimeshasema utahtajika kununua mfano taa ziwepo za kujitegemea tena zikiwa katika wiring ya peke yake, lakini pia swala la upotevu wa umeme kutokana na kanuni ya Power loss haitakwepeka japo utakua umepunguza pakubwa (hata siku moja nishati haiwezi kusafiri pasipo kupotea ila kwa hii design kiwango cha upotevu kinakua kwa kiwango kikubwa).

Hasara ya tatu, ikiwa utatumia Lead acid battery (hizi znazotumia sulphuric acid kama electrolyte) zinapojaa huwa zinatoa hydrogen na oxygen katika process wanayoita (gassing) sasa mfano charge control ipate hitailafu battery ita overcharge kupelekea over gassing ikitokea chanzo chamoto basi faham hydrogen ita react na oxygen kwa kuwaka (italipuka).

2. Njia ya pili ni ya kutumia wiring ileile ya umeme wa kawaida (AC) na kila kitu kitabaki katika hali yake. Utakachofanya hapa ni mara baada tuu ya kufunga power station yko ya sola utahitajika kuwa na inverter ambayo kazi yake itabadili umeme wa DC ule wa sola kuwa AC na ku step up voltages at the same time.

Hapa umeme wetu ukishabadilishwa kuwa AC na hiyo inverter ina maana tunaweza kuutumia kwa matumizi ya kawaida bila kuhitaji vifaa special vya DC wala nini. Utakachofanya kuuingiza umeme huo kwenye mfumo wa wiring ya nyumba yako utaupeleka kwenye main switch kupitia kwenye kifaa kinaitwa Change over switch hiki kinachukua input ya TANESCO na ile kwenye inverter yetu lakini inatoa output ya mojawapo kati ya hizo source mbili, yaani kama TANESCO imekata utainonyeza let say unaipeka juu ndio upande wa inverter na ukiipeleka chini ina disconnect inverter na kuunga TANESCO and vice versa.

Faida ya huu mfumo hauhitaji wiring ya kujitegemea, haihitaji chanzo kukaa karibu na vitumiaji (kwa hyo unaweza hata kuitengea sehem yke nje huko au stoo) haitaathiri mwonekano wa chumba chako kama sebule hivi.

pia upotevu wa umeme si mkubwa kama ule wa mwanzo kwasabab hapa umeme utasafiri katika voltage kubwa (230V) badala ya (12V) zile za mwanzo kwa hivyo current ztakua kidogo tuu.

Napendekeza zaidi huu mfumo wa pili.

Ahsante!
 
Tafadhali nieleweshe kuhusu ule umeme wa backup Yaani, kunakuwa na back up ya umeme ukikatika unaweza kutumika kwa masaa 12.

Hapa sizungumzii solar. Naomba elimu
 
Tafadhali nieleweshe kuhusu ule umeme wa backup Yaani, kunakuwa na back up ya umeme ukikatika unaweza kutumika kwa masaa 12.

Hapa sizungumzii solar. Naomba elimu
Nunua inverter charger combination na battery,, wakati umeme upo huwa inafanya kazi kama charger kuchaji battery then umeme ukikatika unai switch upande wa inverter inaaza ku draw umeme ktoka kwa battery ku step up na ku amplify,, so utakua umeepukana na habari ya solar panel ila battery lazma iwepo,, na ukubwa au capacity ya battery ndiyo ita determine masaa ya huo umeme kuwepo pindi TANESCO imekata
71qNX8kkbRL._AC_UF894%2C1000_QL80_.jpg
 
Nunua inverter charger combination na battery,, wakati umeme upo huwa inafanya kazi kama charger kuchaji battery then umeme ukikatika unai switch upande wa inverter inaaza ku draw umeme ktoka kwa battery ku step up na ku amplify,, so utakua umeepukana na habari ya solar panel ila battery lazma iwepo,, na ukubwa au capacity ya battery ndiyo ita determine masaa ya huo umeme kuwepo pindi TANESCO imekata View attachment 2539373
gharama zikoje

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
gharama zikoje

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Inategemea masaa unayotaka umeme uwepo baada ya TANESCO kukatika,, sambamba na hilo nyumba yako ina consume umeme kiwango gani ( vifaa vyako kama vnatmia umeme mwingi au kdogo na muda utakaotaka vi operate) so ukijua hlo fundi atakushauri uchkue battery ya ukubwa gani na hiyo inverter charger combination ya ukubwa gani na mwisho utajua vinagharimu pesa ngapi,, vlevle brand za hvo vifaa hutofautiana ubora na gharama pia, mwisho location inategemea uko wapi sio kila mahali bei ztafanana mkuu
 
nina nyumba ya vyumba vitatu tv,2 kubwa za inch 70 na inch 50,friji 2 na ac 3 basi

nataka inayoweza survive kwa walau masaa 12

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
nina nyumba ya vyumba vitatu tv,2 kubwa za inch 70 na inch 50,friji 2 na ac 3 basi

nataka inayoweza survive kwa walau masaa 12

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Kikawaida hivyo vyote inapaswa ujue wattage zake,, huwa zmeandkwa Kam zntmia kias gan,, so utajumlisha mfano TV ni 120W + TV 90W + FRIDGE 180W + A/C 500W n.k.... ukipata details hzo inakua rahisi ku design back up yako iweje,,

SASA KURAHISISHA HILO NKUULIZE TUU KWA WASTANI HUWA UNATUMIA UNIT NGAPI PER DAY (24hrs), then ntatumia experience hiyo kukadiria ukubwa wa back up itakayokufaa,,,( kuzisoma details zke kwenye chombo husika mara nyingne huwa hazko direct km ni watts ngapi unakuta wameweka Voltage na current ambapo unatakiwa ufanye calculation kujua wattage zake kitu ambacho sio kla mtu anajua hayo mambo)
 
kwa mwezi natumia umeme wa 40k ukizidi sana 50k

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Naomba uniambie uhalisia wa kitu hiki... Free flywheel energy, hii ikoje? Kuna uhalisia kwenye hili?
 
kwa mwezi natumia umeme wa 40k ukizidi sana 50k

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Utahtajika kununua dry battery (lead acid battery) tatu za N200 kila moja, Inverter charger combination ya KW3 (3000W) na change over switch kwa ajili ya kuingizia umeme wako (back up) kwenye main switch yako,,, zaid ya hpo ni waya ambazo si kias kikubwa na gharama ya fundi,, nipivokutajia unaweza kwenda dukani ukauliza utajua inagharim kias gan
 
Hivyo vitu gharama yake ni ~ 1m Tsh, mimi ningependa kujua pia nikihitaji na solar hapo ya matumizi kama hayo gharama yake ikoje? Pia ustahimilivu wa solar upoje, inaweza kukaa miaka mingapi kabla ya kubadilishwa ? Naweza kutumia Solar kama mbadala wa TANESCO kwa nyumba kubwa kwa nia tu long time ku save cost, is it cost effective in a long run au tuendelee na Tanesco tu ?
 
Umeme wa solar nikikupigia hesabu utakimbia,, that's why unaona jua linawaka kila mahali lakin power station za solar ni chache sana then huwa znahtaji back up ya diesel generator,, hyo ni kwa level ya grid ya taifa so hata ukija kwako itoshe tuu kusema umeme jua unagharim mno tulia tuu na tanesco ndugu,,
 
Naomba uniambie uhalisia wa kitu hiki... Free flywheel energy, hii ikoje? Kuna uhalisia kwenye hili?
Flywheel haina maajabu zaidi ya kuwa lenyewe ni gurudum lenye mass kubwa kuwezesha ku store mechanical energy temporary wakati engine inapokua katika mapigo yasiyo ya power,,,, lakin pia kufanya ile mechanical output kuwa smooth (kuondoa ma gap kati ya pigo la power na mapigo ya exhaust & input,,, kwa lugha nyepesi flywheel ni sawa na CAPACITOR katika electronics,, kikubwa uelewe hili dude halizalish nishati yoyote ila linahifadhi kwa matumizi ya muda mfupi ya injini au popte unapoona imetumika,,

Mpaka sasa hakuna ugunduzi rasmi kuthibitisha uwezekano wa free energy machine,, kilichopo ni nadharia tuu so ukiona zile fake videos YouTube ni kutafuta views tuu,,

Iko hivii unaposema free energy flywheel/generator/motor maana yake hiyo machine itazalisha nishati bila kuhitaji input yoyote km ilivo kwa diesel generator au steam turbine, windmill, solar cells kwamba hivyo vyote huhitaji aina Fulani ya nishati alafu kazi yake ni kuibadili kuwa umeme au kimakanika au joto n.k.. wakati kimsingi hata katika mchakato wa ubadilishaji huo wa nishati huwa kuna upotevu kwa namna mbalimbali hivo output huwa sio 100% Yani lazma itakua chini ya hpo tuu,,
 
Umeme wa solar nikikupigia hesabu utakimbia,, that's why unaona jua linawaka kila mahali lakin power station za solar ni chache sana then huwa znahtaji back up ya diesel generator,, hyo ni kwa level ya grid ya taifa so hata ukija kwako itoshe tuu kusema umeme jua unagharim mno tulia tuu na tanesco ndugu,,
Kiongozi, tunaomba estimation ya umeme wa jua kwa majumbani tu, mfano nyumba inayotumja umeme wa 150,000Tsh kwa mwezi, 414.5 unit. Nahitaji investment ya kiasi gani ili nitumie umeme wa solar na Tanesco iwe ndio umeme mbadala ?
 
Back
Top Bottom