Au na yy kuokotwa toka jalalani? Maana msomi mwenye kuamini kuwa kuvaa mavazi yafananayo na bendera, kuimba mapambio, kushangilia kw sauti kila mara bosi ake anapotoa neno ni dalili za uzalendo, anayefikiria kutajataja majina yote ya rais kila mahala - misikitini, makanisani, mashuleni, mikutanoni...nk. ni uzalendo na sio kujipendekeza, kutajataja idadi ya digirii alizo nazo kila anapohutubia ...nk. hatoshi.Amejiaribia mwenyewe inaonekana jamaa walikuwa na imani nae sana. Ukipewa nafasi ya wizara ya mambo ya nje, wizara ya mambo ya ndani au fedha; kwa mwanasiasa elewa wewe ni potential candidate wa nafasi ya juu in the future kwenye nchi zenye unitary constitution. Na hizo wizara ni senior kweli kasheshe sasa ukimsikiliza Mwigulu the nonsense is beyond me.
Ndo walewale wanaokaa viti vya mbele ili waonekane. Ni balaa kwamba, hapa Tz, unapokuwa na tabia ya kuketi viti vya mbele ili wakuone, kweli unaonekana. Wametoka walikotoka wamehamia huko waliko, kutimiza lengo. Ndo hao wanaomfananisha na kumuita mkuu wa nchi mungu! ...dah!
Ikiwa ni kweli uongozi unafanya maamuzi, mabaya/mazuri kw niaba, basi wanapomkosea Mungu, wanafanya hivyo kw niaba yetu pia! Matokeo, Maendeleo ya Kusadikika ...Mungu tuhurumie