Tofauti kubwa kati ya Mbowe na Tundu Lissu

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,490
11,660
Freeman Mbowe
Mbowe kwa upande wa akili. Hana. Ila anajitahidi wakati mwingine kuonesha ana busara. But angekuwa na akili na busara angekuwa mwanasiasa mzuri zaidi. Kuna kipindi sababu ya kukosa akili anakosea steps.

Mfano:
Suala la kusema alivamiwa akapigwa kuvunjwa mguu halikuwa na ukweli. Ilikuwa ni performance ambayo haikuwa na tija. Alichemka sana ktk hilo. Alianguka kwa sababu ambazo anazijua si kupigwa. Ifikie hatua tuwe wakweli tu.

But kuna kipindi anakuwa na utulivu flani mzuri. Ila bado kuna kipindi anakurupuka sana. Jana hakuweza ichambua kisomi hotuba ya Mh. Rais akakimbilia ku conclude kukatisha tamaa juhudi za Rais kuwa wakutane. Nadhani alipaswa kutulia. Kutafakari.

Tundu Antipas Lissu
Ana akili sana. Anaweza jenga hoja. Anajiamini. ila anakosa Busara na si mwanasiasa mzuri. Matamko yake huwa yanaonesha ana utoto/ujana mwingi sana. Hafikirii kabla ya kutamka. Anatamka anakuja fikiria baadaye.

Mfano:
Aliyoyaongea baada ya kifo cha Magufuli yalionesha utoto, kukosa busara n.k hata kama aliumizwa sana na Utawala ule kipindi hiki ndo angeweza kujichukulia credit kwa kuongea kama mtu aliyekomaa, but akaanza kupita akifanya sherehe na kutukana. Huo uli kuwa ni utoto.

Ukosefu wa Busara. Jambo ambalo linaonesha ana immaturity katika siasa na nini cha kuongea. Shida kubwa ya Lissu ni kuwa na mihemko. Rejea kauli ya kuwa Nyerere ali.... Kwenye bunge la katiba. Hakupaswa anene hayo. Anahitaji kujifunza nini cha kuongea na wakati gani.

Tundu Lissu angejifunza kwa akina Mandela, Lowassa n.k

Mbowe aambiwe wakati flani ni vizuri kunyamaza aonekane ana busara kuliko kuzungumza. Na anapotaka kuzungumza anapaswa aangalie nini cha kuzungumza.
 
Hivi unaposema mtu hana akili sijui hata una maana gani? Mtu ambaye ametoka familia bora kabisa na yenye utajiri luluki toka kipindi kabla hatujapata uhuru wa Tanganyika, mtu ambaye ni mfanyabiashara mwenye utajiri wa kutosha, Mwenyekiti Taifa wa CDM, mtu ambaye alikuwa mbunge kwa muda mrefu na hata kuwa KUB, unathubutu kunasema hana akili!?
 
wewe boya kabisa watu wenye akili huwa wanaona fursa na kutumia mtu ni investor wa ndani na nje unathubutu kusema hana akili? pili hakuna mwadamu ambaye ameumbwa hana akili utofauti ni namna ya kuzitumia elewa hivyo
 
Tangu lini Nyumbu wakamtakia mema rais Samia hadi wampangie cha kufanya?
 
Hangaikeni na mzee wa MIGA mtetezi wa mashoga.
Mashoga ni watu hawakushushwa toka mbinguni ni watoto, ndugu, jamaa zetu hawakuzaliwa hivyo wengi wao walifanyiwa ukatili utotoni, tuwafundishe, tuwaelimishe juu ya Mungu na kuwaombea wabadilike kama wewe ni mtu mzima hutamcheka kilema maana hata kesho yako hujui mwanao au ndugu yatakayompata unaweza kumcheka shoga leo kesho mwanao akawa mvuta bangi au madawa ya kulevya
 
Hapo kwenye ushoga sijui hawa jamaa walitaka kulipeleka wapi hili taifa.

Some time na mshangaaga sana Mboe sijui alifikiri nini kumruhusu mzee wa MIGA kugombea urais yule mtu hafai kuwa kiongozi mkuu wa nchi anamihemko na misifa ya kijinga sana.
 
Mashoga ni watu hawakushushwa toka mbinguni ni watoto, ndugu, jamaa zetu hawakuzaliwa hivyo wengi wao walifanyiwa ukatili utotoni, tuwafundishe, tuwaelimishe juu ya Mungu na kuwaombea wabadilike kama wewe ni mtu mzima hutamcheka kilema maana hata kesho yako hujui mwanao au ndugu yatakayompata unaweza kumcheka shoga leo kesho mwanao akawa mvuta bangi au madawa ya kulevya
Sasa unawaambia nini waliotaka kuuhalalisha.
 
Sina lengo la kukukosoa sana, ila nataka tu nikuambie, kwanza akili ni busara na busara ni akili. Sasa, busara za MBOWE ndizo akili zenyewe na akili za LISSU ndizo busara zenyewe.

Umetoa mfano kwamba alitakiwa ajifunze sana kutoka kwa kina Mandela, Lowassa. Huu ni ujinga mkubwa sana. Ndo maana kwa unazozisema, Lowassa alishindwa hata kuwa provocative baada ya kuporwa ushindi.
 
Inawezekana usemacho au la, but suala la busara, hekima na akili nadhan ungeliweka kwa mapana zaid, maan wapo ambao kufyatuka bila staha ni wengi sana. Na kama una nia kweli ya kueleimisha ungewa address wa pande zote hapo ungepata credit.
 
Freeman Mbowe
Mbowe kwa upande wa akili. Hana. Ila anajitahidi wakati mwingine kuonesha ana busara. But angekuwa na akili na busara angekuwa mwanasiasa mzuri zaidi. Kuna kipindi sababu ya kukosa akili anakosea steps.

Mfano:
Suala la kusema alivamiwa akapigwa kuvunjwa mguu halikuwa na ukweli. Ilikuwa ni performance ambayo haikuwa na tija. Alichemka sana ktk hilo. Alianguka kwa sababu ambazo anazijua si kupigwa. Ifikie hatua tuwe wakweli tu.

But kuna kipindi anakuwa na utulivu flani mzuri. Ila bado kuna kipindi anakurupuka sana. Jana hakuweza ichambua kisomi hotuba ya Mh. Rais akakimbilia ku conclude kukatisha tamaa juhudi za Rais kuwa wakutane. Nadhani alipaswa kutulia. Kutafakari.

Tundu Antipas Lissu
Ana akili sana. Anaweza jenga hoja. Anajiamini. ila anakosa Busara na si mwanasiasa mzuri. Matamko yake huwa yanaonesha ana utoto/ujana mwingi sana. Hafikirii kabla ya kutamka. Anatamka anakuja fikiria baadaye.

Mfano:
Aliyoyaongea baada ya kifo cha Magufuli yalionesha utoto, kukosa busara n.k hata kama aliumizwa sana na Utawala ule kipindi hiki ndo angeweza kujichukulia credit kwa kuongea kama mtu aliyekomaa, but akaanza kupita akifanya sherehe na kutukana. Huo uli kuwa ni utoto.

Ukosefu wa Busara. Jambo ambalo linaonesha ana immaturity katika siasa na nini cha kuongea. Shida kubwa ya Lissu ni kuwa na mihemko. Rejea kauli ya kuwa Nyerere ali.... Kwenye bunge la katiba. Hakupaswa anene hayo. Anahitaji kujifunza nini cha kuongea na wakati gani.

Tundu Lissu angejifunza kwa akina Mandela, Lowassa n.k

Mbowe aambiwe wakati flani ni vizuri kunyamaza aonekane ana busara kuliko kuzungumza. Na anapotaka kuzungumza anapaswa aangalie nini cha kuzungumza.
Unaonaje ujisalimishe Mirembe kupima afya ya akili zako?
 
Hata usipouhalalisha ushoga upo. Ukitaka kujua jiulize ni kwanini Kabudi alimkana Makonda ktk msimamo wa serikali
Pia ukitaka kujua hili tatizo ni sensitive hakuna Rais nchi hii atazungumzia, atazungumzia madawa ya kulevya lakini hapo hawagusi kabisa, tatizo lipo kutatua linahitaji utulivu sana ni sawa na biashara ya ngono utatuzi wake ni mgumu
 
Back
Top Bottom