Tofauti Kati ya Watawala na Viongozi: Je, Tanzania Yetu Ina Viongozi au Watawala?"

Je, Tanzania Yetu Ina Viongozi au Watawala?"

  • A. Ina Viongozi

    Votes: 1 7.1%
  • B. Ina Watawala

    Votes: 12 85.7%
  • C. Sifahamu

    Votes: 1 7.1%

  • Total voters
    14
  • Poll closed .

Mwl.RCT

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
13,580
18,618
Sifahamu chochote, ila ambacho nina uhakika nacho ni hiki. Kiongozi yoyote wa ummah, ni zao la jamii anayotoka. Hivyo tabia za kiongozi huakisi mno tabia na aina ya jamii inayotawaliwa....

Tusiwatenge viongozi kama ni binadamu wa aina nyingine tofauti na sisi. Hujiulizi kwanini, watu wanaoonekana ni wazalendo na wachukia ufisadi, hubadilika mno pindi wamepata madaraka.

Mwanafalsafa wa kijerumani Max Weber anasema ukiona kiongozi anaishi kama mtawala "mfalme" na anategemea sana nguvu zake na hulka "charisma" kuliko sheria, kanuni na taratibu basi fahamu fika kwamba jamii anayoiongoza iko nyuma mno kimaendeleo.

Tembea sehemu muhimu za nchi hii kama, taasisi za kielimu, masoko ya ummah, maofisi ya ummah, hospitali za ummah na taasisi za kifedha, halafu angalia aina ya watu waliopo huko ndiyo utafahamu kwanini Tanzania ipo hapa ilipo. Kuna hatari kubwa mno.

Watanzania tusitafute mchawi kabisa, ilhali sisi wenyewe ni watu wa hovyo. Jamii ambayo imejiaminisha kwamba fedha, mali na starehe ndiyo malengo makuu ya binadamu hapa duniani, usitegemee itakuza viongozi wazuri.

Vijana leo hii wanaingia kwenye siasa au wanafanya kazi ili wapate ukwasi wa kupondea raha. Waende sehemu wanywe pombe, wapate wanawake, wawe maarufu au wapate vyeo.

Hedonistic Societies are inherently destructive. Ancient Rome is a prime example.....
 
Kuna watawala na royal families 👪, mpaka zinaachiana majimbo ya kiuchaguzi na kuonyesha kuwa they don't take a s...t,wanaongea in public maana kondoo hawana push back
 
Ni Watawala, yaani tumetoka Dar saa 11, tumesimamishwa Msolwa kupisha msafara wa Makamu wa Rais, hadi saa nne kasoro hii ndio tunapita hapa Mikese mizani. Hawa ni Watawala wanaojijali wenyewe tu
Hii ni changamoto kwakweli.
 
Tusiwatenge viongozi kama ni binadamu wa aina nyingine tofauti na sisi. Hujiulizi kwanini, watu wanaoonekana ni wazalendo na wachukia ufisadi, hubadilika mno pindi wamepata madaraka.
Ni kweli, Mifano hai mingi tunayokwenye jamii yetu
 
Kuna watawala na royal families 👪, mpaka zinaachiana majimbo ya kiuchaguzi na kuonyesha kuwa they don't take a s...t,wanaongea in public maana kondoo hawana push back
Je nini kifanyike?
 
Watanzania tusitafute mchawi kabisa, ilhali sisi wenyewe ni watu wa hovyo. Jamii ambayo imejiaminisha kwamba fedha, mali na starehe ndiyo malengo makuu ya binadamu hapa duniani, usitegemee itakuza viongozi wazuri.

Vijana leo hii wanaingia kwenye siasa au wanafanya kazi ili wapate ukwasi wa kupondea raha. Waende sehemu wanywe pombe, wapate wanawake, wawe maarufu au wapate vyeo.
Ukweli mchungu, Tunatakiwa kubadilika, Jamii inatakiwa kubadilika.
 
Mtazamo wangu unaniambia kwamba.....
Baada ya Nyerere kupokea nchi toka kwa mkoloni, kilikua ni kipindi cha mpito kwaajili ya kutemgemeza katiba na sera za nchi.
 Mwinyi.........
 Mkapa alikua mtawala kwasababu alijiwekea dira kwaajili ya nchi, nalikua anautaratibu wa kurudisha mrejesho kwa WaTanzania hotuba kila mwisho wa mwezi. Yes alikua anafanya maamuzi yenye makosa wakati mwingine, lakini kwangu naweza nikasema alisimamia alicho kiamini na uwajibikaji/nidhamu ilikuepo. Mkapa alikua mkali lakini hakua dictator.
 Jakaya.............
 Magufuli alikua mkali, mkorofi, dictator, mwenye kufanya maamuzi ya haraka hata kama ni maamuzi mabaya ila alifanya. Lakini ukweli nikwamba Magufuli alikua anahuruma sana ukiacha hayo madhaifu yake mengine. Magufuli alikua akiamua kufanya jambo lake kwaajili ya taifa hakurudi nyuma na alifanya hata kama bunge, mahakama na baraza lake halikutaka yeye alifanya tu. Magufuli aliwajua mafisadi walio ifisidi nchi na alikua akiwaonyesha chuki ya wazi na alilalanao mbele pasipo kujali ushkaji ama power ya mafisadi. Magufuli hakua rafiki wa matajiri, na aliwapenda sana watu wenye maisha ya kawaida (kuhusu ufisadi wake sijui).
 Samia.........

Hou ni mtazamo wangu.
 
Je nini kifanyike?
Time itaamua ,binafsi sioni generation hii ikifanya ile push back, tukifanikiwa kupata KATIBA MPYA na sio viraka itasaidia mno ku balance mambo, kuna uzi humu eti TRA officer's wamekamata suspects na kuwapiga ,hii ni makosa makubwa mno,TRA officer's hawana arresting power pia kupiga ni kuvunja sheria ila wanajifanyia with pure impunity, we need mass push back
 
Mbona jibu liko wazi kabisa. Nvhi hii miaka nenda inatawaliwa! Na haiongozwi. Tungekuwa na viongozi, wasingetushika masikio na kutuendesha vile wapendavyo! Huku wakipata msaada wa karibu kutoka policcm.
 
Sifahamu chochote, ila ambacho nina uhakika nacho ni hiki. Kiongozi yoyote wa ummah, ni zao la jamii anayotoka. Hivyo tabia za kiongozi huakisi mno tabia na aina ya jamii inayotawaliwa....

Tusiwatenge viongozi kama ni binadamu wa aina nyingine tofauti na sisi. Hujiulizi kwanini, watu wanaoonekana ni wazalendo na wachukia ufisadi, hubadilika mno pindi wamepata madaraka.

Mwanafalsafa wa kijerumani Max Weber anasema ukiona kiongozi anaishi kama mtawala "mfalme" na anategemea sana nguvu zake na hulka "charisma" kuliko sheria, kanuni na taratibu basi fahamu fika kwamba jamii anayoiongoza iko nyuma mno kimaendeleo.

Tembea sehemu muhimu za nchi hii kama, taasisi za kielimu, masoko ya ummah, maofisi ya ummah, hospitali za ummah na taasisi za kifedha, halafu angalia aina ya watu waliopo huko ndiyo utafahamu kwanini Tanzania ipo hapa ilipo. Kuna hatari kubwa mno.

Watanzania tusitafute mchawi kabisa, ilhali sisi wenyewe ni watu wa hovyo. Jamii ambayo imejiaminisha kwamba fedha, mali na starehe ndiyo malengo makuu ya binadamu hapa duniani, usitegemee itakuza viongozi wazuri.

Vijana leo hii wanaingia kwenye siasa au wanafanya kazi ili wapate ukwasi wa kupondea raha. Waende sehemu wanywe pombe, wapate wanawake, wawe maarufu au wapate vyeo.

Hedonistic Societies are inherently destructive. Ancient Rome is a prime example.....
Inatisha kwa kweli, sijui Tz inaelekea wapi?
 
Back
Top Bottom