Toa ushuhuda wowote ambao unadhani bila Mungu usingetoboa

Jamaa ile ya kwanza iliondoka na mama yangu πŸ₯ΊπŸ₯ΊπŸ₯ΊπŸ₯Ί


Zab 125:1 SUV​

Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.
 
Mungu hufanya njia pasipo na njia 😍😍🀣🀣🀣 barikiwa sana jamaa
 

Yer 1:5 SUV​

Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

========

Nalikuchagua kabla sijakuumba
 
mwaka wa 8 huu sina ajira.. kujiajiri nako imekua kimbembe!

ila nipo!

nina Afya njema nazidi kupambana!

naamini bila Mungu nisingekua hivi
Wakati wa Mungu utakufikia soon, keep believing
 
Tuseme Amen ,Sometimes inashangaza sana kuna wakati unamuasi sana Mungu kusali kwa tabu lakini inashangaza pale ambapo unapiga goti na kumuomba unashangaa boom umekipata .

Wakati nasoma nakumbuka nlikua mkorofi sema nikienda kanisani naomba kweli basi Mungu aliamua kunidhirihishia miujiza yake kipindi kile unakuta umelala unaota mitihani kesho ukiingia unakuta ni ileile ulioiota au unakuta bado dakika 5 lakini kuna roho inakulazimisha ufungue ukurasa usome na kweli ukiingia unaukuta

Miujiza yake Aisee ni Mingi yani wakati mwengine unapata tatizo lakini ghafla anatokea mtu ambaye hutegemei anakuja kukusaidia
 
Akika ayo yote aliyonitendea Mungu ni mfano wa punje ya haradali hii pumzi nayo jidai nayo inatosha kabisa kuwa ushuhuda kamili bila ya kuniuliza juu ya ushuhuda wa Mungu kwangu na kwa wengine
 
Watakupinga na kukubeza but i think I UNDERSTAND this feeling you express here...
Sisemi nakuunga mkono ila NIMEKUELEWA SITUATION YAKO and i dont judge you at all.

Wengi ni wanafik wakikuponda hapa au pengine Mungu KAWAPENDELEA SANAA but guys kuna watu wana mateso sana na kuna wakat tunateseka sana..Anyway Mungu sijui huwa anakua wapi.

Namuamini Mungu ila kuna wakat NAPATA MASHAKA MAKUBWA SANA
 
Ilikua mwaka jana kwa mambo haya ya ulevi cku hiyo nilizima watu wakaja niokota nilikaa ICU wiki moja nilikuwa sitambui chochote.Mama mkwe na wife walikua bega kwa bega nami mpaka nikapata nafuu namshukuru Allah maana ningeweza poteza maisha mwenyez mungu naomba umpe maisha marefu mama mkwe nampenda sana alinipigania mpaka nikawa sawa
 
Ashukuriwe Allah kwa kukuokoa na mautiπŸ™πŸ»πŸ™πŸ»πŸ™πŸ»
 
Pole sana ndugu.
Asante mkuu, she went in a week hapo Mloganzira it was February 4th 2021 ila uzuri na uhakika na lipo.

I'm very sure of itπŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

Ufu 14:13​

Ufu 14:13 SUV​

Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
 
nipo nae mi huwa siachagi mke hata akiniwekea sumu nikipona naendelea nae mimi sipo kama mungu shetan kakosea kidogo kamfukuza mimi naangalia hadi mwisho kitakuwa nini, yaani mm ndio mwisho wa matatizo yote
Kwaio umemzidi Mungu 🀣🀣
 
Sasa usifanye dhambi kizembe

Rum 6:1-7​

Rum 6:1-7 SUV​

Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.
 
Akika ayo yote aliyonitendea Mungu ni mfano wa punje ya haradali hii pumzi nayo jidai nayo inatosha kabisa kuwa ushuhuda kamili bila ya kuniuliza juu ya ushuhuda wa Mungu kwangu na kwa wengine
Mungu akupe miaka mingi tena uone wajukuu zako
 
Siku kama ya leo mwakani nitakuwepo tena ofisini kwangu kama ilivyo leo; ni ushuhuda ulio mbele kwa sababu nina agano na Mungu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…