mwanaume..nina maana mwanaume kama amegundua wewe ni wife material hawezi kukuacha hivi hivi mtoto hana shida ukimpenda mama lazma umpende na mtoto na ikitokea mwanaume anakwambia mtoto wako umpeleke sehem ili uishi nae ujue hapo kuna masimango sana itakuwa ukimkosea kidogo masimango hayaishi kama sikukukuta bikra, ndio maana ulizaa ikaachwa na mengi mengineyo, mtoto mdogo hali hata robo kilo, kwanini umnyanyapae? wengine wanaogopa gharama za kusomesha mtoto asiye wake, watoto ni malaika tu, nasema hivi ipo mifano mingi tuu watoto wa kuwalea jindi wanavyokuja kuwa msaada hapo baadae kwa familia...Mimi niko na mtoto namlea na huwezi jua kama c wangu na hata jina shuleni nimemuandikisha la kwangu na di yeye wala ndugu zake wote wanajua ni wanangu wa damu na waka sijawahi juwaza kumpunguzia ama kumfikiria mara mbili wanayopata wakwangu ndivho hicho anachopata yeye na ajabu ya mungu huyu mtoto nimefanana nae sana, na akili mno darasani, yaani ndio hivyo inatokana na roho ya mtu ningekuwa na uwezo ningeenda hata kutafuta ktk vituo niwachuke nikao nao sina uwezo tuu....ila ukiona mwanaume anamchukia mwanao ni bora kuendelea na maisha yako kuliko kuikimbilia hiyo ndoa na kukitesa kiumbe kisicho na hatia...ni hayo tu.