Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 32,254
- 44,363
siku hizi baadhi ya makampuni makubwa yameanza kuitambua mkv, mfano microsoft kweny windows 10 ame add support ya mkv native bila kutumia 3rd party software kama vlc, ila bado safari ni ndefu. kuna makampuni makubwa mengi tu kama Apple, makampuni ya movies etc bado hawana time na mkv.Mkuu nimenot kitu hapo. Umesema MKV inatumika kwenye piracy. HOW na ni format gani nyingine amabazo sio official recognized.
kivipi mkv inatumika kwenye piracy? unatakiwa ujue hizi mp4, avi, mkv etc unazoziona mbele ya jina la video sio format za video bali ni macontainer tu. yenyewe ndani ndio yanahifadhi video, audio, subtitle etc. container la mkv linakubali almost video format yoyote ile na audio yoyote ile na idadi yoyote ile.
leo naweza download movie torrent ikawa na audio halisi mfano kingereza, halafu ikawa na audio zaidi, kirusi, kichina, kihindi etc utaona kwa mbele ya movie wanaadika neno kama dual audio, mambo haya yanawezekana kwa mkv.
na unaweza ukakuta video ya mkv ina audio kali sana, pengine lossless ambayo hio audio isingewezekana kuwekwa kwenye mp4.
mp4 yenyewe kila video au audio inayokaa kwenye container lake lazima iwe imekuwa defined na MPEG. huwezi kujiamulia.
vitu vingi vya piracy kwenye movies vinatokana na rips, mtu ananunua cd kisha anairip kwenye computer yake na kuisambaza online watu wadownload. wanaorip wengi wanaprefer uhuru wa kutumia video/audio/subtitle format anayoitaka yeye hivyo kupelekea kutumia zaidi mkv.
tofauti na mkv zipo format nyengine za macontainer kama avi, mov na mp4 ila hizi sio maarufu kwenye piracy kama mkv.