Titi Mohamed na Tatu bint Mzee Marafiki Wawili Walioweka Msingi wa Wanawake Kujiunga na TANU

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,261
BIBI TITI MOHAMED NA BI. TATU BINT MZEE MARAFIKI WAWILI WALIOWEKA MSINGI WA WANAWAKE KUJIUNGA NA TANU

Historia ya wanawake kujiunga na TANU inaanza na safari ya Mwingereza John Hatch alipokuja Tanganyika kwa mwaliko wa TANU mwaka wa 1954.

Huyu alikuwa mbunge na mwanachama wa Labour Party aliyekuwa anaunga mkono harakati za Waafrika wa Tanganyika kupata uhuru wao.

Hatch ndiye aliyemshauri Schneider Abdillah Plantan TANU ianzishe tawi la akina mama.

Schneider ni mtoto wa Chief Mohosh Shangaan aliyekuja German Ostafrika na Hermann von Wissmann akiwa kiongozi wa jeshi la Wazulu wapatao 400 kuja kupigana na Abushiri Pangani.

Mohosh alikuja baadae kujulikana kama Afande Plantan.

Kaka yake mkubwa Mwalimu Thomas Plantan alipata kuwa Rais wa TAA na ndiye rais wa mwisho katika mlolongo wa viongozi waliosoma katika shule za Wajerumani.

Schneider ndiye aliyesimama kidete mwaka wa 1950 kuhakikisha kuwa vijana wanashika uongozi katika TAA na TAA ikapata uongozi wa Dr. Vedasto Kyaruzi, President na Abdul Sykes, Secretary.

Schneider akaja tena kuipa TANU wanachama shupavu wanawake, Bibi Titi Mohamed na Bi. Tatu bint Mzee.

Schneider alimfikiria Bi. Tatu bint Mzee kuwa mwanamke ambae angefaa kuunda tawi la wanawake.

Lakini Schneider alipompa Bi. Tatu fikra hii yeye akamwambia kuwa Titi Mohamed angeweza kulikamilisha hili kuliko yeye.

Hivi ndivyo Bi. Titi Mohamed alivyoingia TANU.
Yaliyobakia hivi sasa ni historia.

1701055806175.png

 
Back
Top Bottom