Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,925
- 30,273
SIKU YA MWANAMKE DUNIANI
Gazeti la Mwananchi la leo limechapa makala ambayo walinitembelea Maktaba nami nikawazungusha katika mitaa ambayo wanawawake wa Tanganyika walikuwa hawapunguia katika harakati zao za kupigania uhuru.
Naanza na kipande hicho hapo chini kinachomjulisha Bibi Titi miaka ya mwanzo ya TANU.
Baadae In Shaa Allah tutawatembelea wanawake wengine waliopita katika mlango aliofungua Bibi Titi.
Mikutano ya TANU ya siku za mwanzo ilikuwa ikifanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja mbele ya Princess Hotel.
Kwenye jukwaa lililojengwa kwa miti walikuwa wakikaa wale viongozi wa mstari wa mbele ndani ya TANU - Nyerere rais wa TANU, Sheikh Suleiman Takadir, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU, Bibi Titi Mohamed, John Rupia na Clement Mtamila.
Sahani ya santuri ilikuwa ikipigwa katika gramafoni kupitia kipaaza sauti.
Mwimbo uliokuwa ukipigwa ulikuwa wa Frank Humplink. Frank alikuwa kijana wa Kichagga kutoka Moshi.
Baba yake alikuwa Mzungu.
Humplink alikuwa mwimbaji na mpiga gitaa maarufu sana wakati ule akipiga muziki wake na dada zake wawili Maria na Regina Humplink.
Wimbo uliopendwa sana na TANU na ndiyo uliokuwa ukipigwa katika mikutano yake yote na uliosisimua wananchi ulikuwa na mashairi yafuatayo, ‘’Uganda nayo iende, Tanganyika ikichangamka, Kenya na Nyasa zitaumana.’’
Mwimbo huu ulikuwa na ujumbe wa kisiasa kwa Waafrika wa Tanganyika.
Ujumbe katika wimbo huo ulikuwa kuwa, Tanganyika itakapoamka, kutakuwa vilevile na mapambano nchini Uganda, Kenya na Nyasaland.
Wimbo huu ulikuwa ukivuma toka kwenye vipaza sauti mfululizo kabla ya mkutano huku watu wakikusanyika viwanjani.
Haikupita muda mrefu serikali ya kikoloni ilipata maana halisi ya wimbo huo. Mara moja mwimbo huo ukapigwa marufuku na serikali.
Serikali ya kikoloni iliamuru kwamba mashairi ya wimbo huo yalikuwa watu kuasi.
Lakini kabla ya wimbo huo kupigwa marufuku ulipendwa sana na ulikuwa ukiombwa na wasikilizaji na kupigwa katika kituo cha radio Sauti ya Dar es Salaam.
Baada ya amri ya serikali kituo hicho kiliacha kupiga wimbo huo.
Huenda huu ulikuwa wimbo wa kwanza kupigwa marufuku katika historia ya utangazaji Tanganyika.
Kwa muda mrefu sana wimbo huu ulikuwa kama wimbo rasmi wa TANU.
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)
Katika gazeti hili hapo chini mwandishi Imani Makongoro kaeleza kutokana na mazungumzo yetu historia ya wanawake wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika lakini hawafahamiki na mchango wao bado kutambulika.:
Amina Kinabo
Halima Selengia
Halima Khamis
Shariffa bint Mzee
Nyange bint Chande
Zarula bint Abdulrahman
Tatu bint Mzee