TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Watu wanakupenda wanakumic ndomna wanapenda kukuzingua
Wakiona uko kimya wanakutafutia chokochoko

Ova

🤗

Nabasoma wananipa kila jina na kunifikiri nisiwo.. unajua chokochoko yao.. nakwenda nawo sambamba.. hata wale wametaka kunifukuza humu..wameshindwa.. so 😂
 
Wanabodi

Introduction ya Mada
Hii ni mada very serious kwasababu inaijadili idara yetu nyeti ya TISS ambayo kutokana na unyeti wa idara hii, issues za idara hii huwa hazijadiliwi hovyo hovyo, hivyo ukiona hadi watu tunaojinasibu humu kuwa ni wazalendo wa taifa hili halafu tukajitokeza waziwazi humu kuijadili TISS huku tukitumia majina yetu hali, huu ni uthibitisho kuwa tunaleta mjadala huu kwa nia njema ya uzalendo wa kulisaidia taifa letu pale idara yake nyeti hii inapochafuliwa kwa kusingiziwa tuhuma za uongo, lakini pia kama ni kweli TISS inahusika, then tukubaliane kuwa TISS imechafuka na inahitaji kusafishwa.

Topic ya mjadala huu ni TISS Ikanushe Tuhuma za Uvamizi, Utekaji, Utesaji na Mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge Kwa Uwazi bali Wachunguzwe, Wakithibitika Kuhusika, Wafumuliwe Kwa Kusafishwa Tujenge TISS Safi!

Hivyo naomba mjadala huu ufanyike kwa heshima, staha na uangalifu mkubwa ili badiko hili lisionekane ni bandiko la kukosa uzalendo bali liwe ni bandiko la uzalendo wa kweli kwa taifa lalo lenye lengo la kusadia taifa letu kwasababu haya matukio ya ajabu ajabu yanayohusishwa na TISS, yanaichafua Taswira ya TISS yetu, ambapo kikawaida TISS inapaswa kuwa kama Ikulu, Ikulu ni mahali patakatifu, na TISS inapaswa kuwa ni Idara Takatifu, uadilifu wa TISS, unapaswa uwe ni uadilifu wa kiwango cha juu kabisa ambao haupaswi kutiliwa shaka yoyote, unapaswa kuwa ni uadilifu wa kiwango cha mke wa Kaisari, ile kutuhumiwa tuu ni kosa tosha hata bila kuthibitishwa, anahukumiwa!, hivyo hizi tuhuma mbalimbali za Uvamizi, Utekaji, Utesaji na Mauaji zinazoelekezwa TISS bila ya kukanushwa, zinapelekea TISS yetu kuhukumiwa na mahakama ya umma ambayo haihitaji ushahidi kama tuhuma tuu za mke wa Kaisari, hivyo lengo la bandiko hili ni ushauri wa bure kwa TISS yetu kuwa haya mambo mabaya ambayo TISS inanyooshewa kidole kuwa inahusika, kama haisiki, TISS i come to an open, ikanushe!, ukituhumiwa tuhuma za uongo, ukinyamaza kimya bila kukanusha, hiyo silence inachukuliwa kama ni admission of guilty.

Declaration of Interest
Tunapojadili jambo nyeti kama hili, ni vizuri ku declare interest ili kwanza kujenga imani kwenu wasomaji wangu kuwa mwandishi wa makala hii ni mtu wa kuaminika, hizi data kwenye bandiko hili ni data za kuaminika authentic na bonafide genuine sio data za kuokoteza, data za kubuni au data za kuzua,hivyo ni vyema mimi nikajitambulisha kidogo kwenu, pia kwa sababu mtu unapotoa data nyeti from time to time katika mabandiko yako, huchelewe kunyooshewa kidole kuwa huyu jamaa ni TISS, hivyo na mimi kudhaniwa ni TISS, hivyo bandiko kama hili, litawafungua macho wengi humu kuwa huyu mtoa mada atakuwa ni TISS wa ajabu kweli kuilaumu ofisi yake mitandaoni.

Mimi Pascal Mayalla ni mwandishi wa habari wa kujitegemea mwenye uwezo wa kuandika Investigative Stories, (IJ), ila pia nimepata bahati ya kuzaliwa na kukulia katika familia ya TISS kwa wazazi wangu wote wawili, baba na mama. Baba Mzee Andrew Mayalla (RIP) ameishatangulia mbele ya haki, na mama bado yuko hai, hivyo baadhi ya hoja zangu za kiitelijensia, sio kwasababu mwana wa nyoka ni nyoka, bali mtoto ukizaliwa kwa wazazi wote wawili ni wana inteligensia wa TISS, unazaliwa na natural intelligence ambayo ni tool muhimu sana kuweza kuwa Investigative Journalist.

Tuhuma Mbalimbali TISS
Kuna matukio mbalimbali yametokea na kuhusishwa na TISS, mengine ni visible, mengine ni invisible, sasa kwa sababu watu wote wenye akili timamu, wanajua TISS zote duniani huwa zinafanya matukio, yale matukio ambayo in invisible yanayohusishwa na TISS, kama kupotea kwa Ben Saanane na Azory Gwanda, sitahitaji TISS wajitokeza kuyakanusha kwasababu ni tuhuma za hisia tuu, lakini kwa yale matukio visible kama kushambuliwa kwa Tundu Lissu, kuvamiwa kwa Clouds Media na wale makirikiri wa Mkuu wa Mkoa wa DSM na yule mpuuzi aliyemtishia bastola Waziri Nape kuelezwa kuwa wale ni TISS kunaichafua idara yetu nyeti ya TISS!. Hivyo kama wale makirikiri waliovamia Clouds TV sio watu wao, TISS wasikae kimya wajitokeze wawakane na kukanusha uhusika wa TISS!. Kama yule mpuuzi aliyemtishia Nape kwa bastola sio mtu wao, TISS wajitokeze wamkane na wakanushe. Huku kutokea kwa matukio kama haya na kuhusishwa na TISS, halafu TISS wanajua sii kweli, sii wao, huku kukaa kimya bila TISS kukanusha uhusika wake, kunachukuliwa ni admission of guilt!.

Jee Tuhuma za Uhusika wa TISS zinatolewa Wapi na Zinatolewa na Nani?.
Nyingi ya tuhuma za kuhusika kwa TISS katika baadhi ya matukio ya hovyo, huanza kwa kutolewa na watu tuu wa kawaida, tuhuma zinapotolewa na watu wa kawaida tuu, watu ambao they are nobody, na zinatolewa kwenye vijiwe vya kahawa, it is right, kuzipuuza, lakini tuhuma hizi dhidi ya TISS zinapofikia kiwango cha kutolewa ndani ya Bunge letu Tukufu, tuhuma hizi sio za kuzipuuzia hata kidogo kwasababu Bunge ni chombo rasmi, wabunge wtu ni wawakilishi rasmi wa wananchi, wanapoituhumu TISS Bungeni, this is something very serious, sio jambo la kupuuziwa kwasababu TISS iko chini ya Ikulu yetu, na Ikulu ni mahala patakatifu, tuhuma tuu kumhusu mke wa Kaisari zinatosha kumuondoa Ikulu asije akapanajisi patakatifu petu!. Hiyo TISS isikae kimya lazima iibuke kuja kukanusha kutohusika kwake na kujisafisha na uchafu wa makandokando haya!, winginevyo kama ni kweli inahusika, ijitathimini yenyewe kwa kuwajibika au iwajibishwe kwa kusafishwa!.

Jee TISS ni Chafu Inahitaji Kusafishwa?.
Huu mjadala unaoendelea kuhusu utekaji, utesaji na mauaji ambavyo vinahusishwa na idara yetu nyeti ya Usalama wa Taifa, TISS ni uthibitisho tosha kuwa TISS imechafuka inahitaji au kujisafisha au kusafishwa!.

Pamoja na Tanzania kuridhia mkakati wa Open Government Initiatives lakini kuna vitu huwezi kuvijadili openly lakini bado unaweza kuvichunguza na kuvifanyia kazi kimya kimya ila public ikaona matokeo na kurudisha imani.

Kuna watu wanadhani Usalama wa Taifa TISS wao ni malaika na hawawezi kabisa kufanya makosa kama madudu haya wanayotuhumiwa nayo sasa. No!, TISS ni kweli kwa vile iko chini ya Ikulu, na Ikulu ni mahali patakatifu, TISS pia inapaswa kuwa ni idara takatifu, lakini kwa vile TISS inaendeshwa na binadamu na sio malaika, TISS inaweza kufanya makosa na uchafu huo ukawa ni kweli ni TISS, ndio maana katika bandiko hili nasisitiza tuhuma hizi dhidi ya TISS kama sii kweli, TISS ikanushe, kama ni kweli, TISS imechafuka na inahitaji kusafishwa!. Hii sii mara ya kwanza kwa TISS kuchafuka, huko nyuma kuliwahi kutokea matukio ya TISS kuchafuka na Ilisafishwa!.

TISS Iliwahi Kuchafuka Vipi na Ilisafishwaje?.
Tiss huko nyuma iliwahi kufanya makosa ya utekaji, utesaji na hata uuaji, na ikafumuliwa!. Hivyo kwa vile tayari tunayo precedence ya vitendo viovu vya TISS kuwahi kufanyika huko nyuma, hivyo kwa kuutumia uthibitisho wa uovu huo, una justify kuwa kuna pia kuna wa vitendo hivi viovu ambavyo TISS inashutumiwa navyo, kuna uwezekano kabisa ikawa ni kweli ni TISS wetu ndio is behind huu uovu na uchafu huu unaozungumziwa sasa hadi Bungeni kwetu, ndio maana hadi Bunge linaelezwa halafu TISS wamekaa kimya wakishupaza shingo zao, kwa hoja kuwa "mnaweza kutufanya nini?", it's very true TISS ya nchi zote wakifanya uovu wowote kwa amri halali kutoka juu, no one can do anything!, hawawezi kufanywa lolote wala kuchunguzwa na yoyote, hapa duniani, but kuna mamlaka moja pekee kuu kuliko mamlaka zote, inayoweza kufanya kitu, kupitia kitu kinachoitwa Karma, hakuna atakajua kuwa mamlaka hiyo imefanya, bali matokeo ya karma ndio huonekana!.

Jee ni TISS Wetu Wanafanya Vitendo Hivi au Wanasingiziwa?.
Kuna uwezekano sio kila utekaji, utesaji, mashambulio na mauaji yanafanywa na TISS, inawezekana kabisa sio TISS as TISS bali matukio hayo ni acts za individual members wa TISS wakifanya a "stand alone operations" bila kupokea command yoyote kutoka juu, hivyo vitendo viovu vya members wachache wa TISS, vikaichafua image nzima ya TISS yetu safi collectively under the collective responsibilities formula.

Pia inawezekana kabisa vitendo hivi vinafanywa na wahuni fulani, ambao wana pose as TISS just to make believe kuwa ni TISS kumbe sio TISS bali ni just impostors wanao fanya matukio kwa kupose as TISS ili ionekane ni TISS, hivyo wanaochafua the good image ya TISS wetu waadilifu, this being the case, TISS iwakane wahuni hawa, ijitokeze kukanusha uhusika wake, na wahuni hawa watafutwe na kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa kuchafua good image ya TISS yetu takatifu!.

Whichever the case, TISS ijitokeze ama ijisafishe na iwakane wahuni hawa, ama isafishwe na kurudisha imani na TISS wetu kwa wananchi wa taifa letu.

Sikilizeni Tuhuma za TISS Bungeni Kwetu
Hebu kwanza msikilizeni Mhe. Husein Bashe

Kisha msikilize Mhe. Tundu Lissu anasema nini kuhusu utekaji na utesaji wa TISS, hao anaowatetea ndio wenye bahati who could live to tell, hivyo ndio waliosalimika, only God knows kwa wale wasio na bahati hatima yao ilikuwaje because they couldn't live to tell!.
Ukitaja neno TISS unanikumbusha State Research Bureau (SRB) ya Uganda enzi za Idd Amin, Wahenga wafuatiliaji wa mambo watakumbuka! sina nyongeza bali hatua zichukuliwe kurejesha heshima na hadhi ya idara yetu hii nyeti kwa ajili ya mustakabali mwema wa taifa letu.
 
Yani unaposema TISS wajitokeze kukanusha tuhuma inaonesha ni jinsi gani ulivyo 0 kichwani...

Naishia hapa
 
No such a thing called "natural intelligence".
 
TISS haiwezi kuwa sehemu ya mipasho, mbunge kasema wai wajibu kwanza hata thamani yao itaondoka, uzi wako umeegemea sana katika dhana huna huthibitisho wa matendo.... Narudia TISS haiwezi kugeuka kujibu kujibu... TISS si watu wa mipasho....
 
Banyamulenge bamutu na Congo, banapenda kuongea bakiswahili. But na moyi ezali nangai, zambe mobimba 😃😃😃😃 boss una mafua nini?

Congo tena!!!.. yaani wanaume nyie nao.. mie nisiandike meanijia juu kama sijui nini..mwaniweka hukwu na kulwela hamuchoki..hiyo kimobimba nakuachia kikwenu..tulia usije jikaba ukiwa unapandisha suruali juu..kwa kuifikisha shingoni.. 🤣🤣🤣🤣
 
Uandishi wako ni kama Mrundi acha kudhalilisha lugha yetu ya kiswahili!
 
We una amini Pasco alipigwa Summary Dismissal? TISS Wana namna nyingi za kufanya vipenyo waonekane ni wenzetu. Shtuka!
Mkuu Mzito Kabwela , kiukweli nimecheka asubuhi asubuhi. Hivyo inawezekana hata mtu alibandika bandiko hili
anaweza kuwa ni ofisa wao, akizungumzia ofisi yake mitandaoni tena kwa kutumia jina lake halisi ambalo ni verified?!.

Kama ni kweli, then kazi ipo !.

P
 
Mkuu tatizo TISS ni mtoto wa serikali aliyeharibika.
Watoto wengine wa serikali hawana kutia neno juu yake.
Tatizo kubwa zaidi ya matatizo uliyotaja 2017 mwanzo wa mada, ni kuingiliwa kiutendaji kwa hali ya juu na wanasiasa hadi TISS sasa hivi kuchukua a very negative image.

Recruitment ni tatizo, operations kuingiliwa na wakubwa hadi missions zisizo na manufaa kwa Taifa kuagizwa na wakubwa.
Tetesi kuwa TISS is devided hasa miaka mitano iliyopita zipo.

Suala la kupata viongozi from outside wigo wa Idara nalo ni tatizo.
Linaingiza resentment, na tetesi za kilichompata DG Kapilimba zipo mitaani.
MIA ya JWTZ kwa sasa ndiyo iko vizuri na wananchi kwa ujumla walifurahia super stealth operations zake hasa wakati wa makabidhiano na kutetea katiba kumteua Mama Samia katika madaraka ya urais.
Baada ya kuingiliwa miaka mingi TISS haiwezi kuwa as efficient kama zamani, ifanyiwe tathmini na marekebisho.
 
Sina uhakika kama kilichompata DG Kipilimba ndani ya Tiss kiliwahi kuletwa humu JF, mambo mengine ya mitaani bora yaishie huko huko mitaani !. Tena akiwa Balozi Zimbabwe, Kipilimba alielezwa stutus ya hali ya Afya ya JPM, akaamua kuisaidia Idara from Zimbabwe kwa kutia neno...

If you not an insider ans its not a breach, please tumegee japo kidogo hizo super stealth operations

Naunga mkono hoja na hiki ndicho nilicho shauri kwenye andiko hili.
p
 
Mkuu Pasco , katika fani ya inteligensia hakuna kitu cha mitaani.
Ndio maana vijana wanatumwa kwenye mabaa kusikiliza tu watu wanasema nini.
ALL information is collected, wengine ndio wanafanya analysis, true or false.
Kwamba Kapilimba aliondolewa in itself ni moshi uliofukuta.
Uki analyse alichosema Kapilimba akiwa Zimbabwe is probably the official narrative, kama alivyosema Waziri Mkuu Songea.
Lakini mitaani (un official outlets) hadithi ilikuwa tofauti kabisa, na hatimaye ikaonekana kuwa kweli.

Kuna muda mzuri tu chombo chetu hiki kukaa sawa na kutekeleza kazi zake kwa weledi bila kuingiliwa.
 
Back
Top Bottom