Timu Mbowe si tulikubaliana hakuna kuhama Chama?

Timu Mbowe si tulikubaliana hakuna kuhama Chama?

Nyie akina Kigaila, Mwalimu, Catherine, Mrema, Mwita na wengine wote wa G55 mmesahau kiapo chetu kuwa baada ya kushindwa uchaguzi hakuna mtu atahama Chama? Sasa imekuwaje wenzetu mnabwaga manyanga?

Je ni kweli ninyi mlikuwa virusi ndani ya Chadema na kwamba mlikuwa mnajaza matumbo yenu kupitia kupitia kumpetipeti Mwenyekiti Mbowe? Kwamba baada ya Mbowe kushindwa uchaguzi mirija yenu imekatwa?

Kila la heri huko kwa Mzee Umbwabwa. Hongera sana Mzee Rungwe a.k.a Mzee wa Ubwabwa kuvuna wanachama wapya lakini chukua tahadhari hao wanachama wapya wanapenda sana vyeo bila hivyo watakupindua au watakuhama!

Ila ile ahadi yako ya kutulisha ubwabwa Watanzania wote achana nayo kwani tumekwisha kuwa watu wazima mambo ya ubwabwa ni kwa watoto tu!
Jana nimemsikia Salum Mwalim anasema uongoxi mpya unaharibu malengo ya watu. Yaani nimecheka hadi watu wa karibu yangu wakashangaa. Yaani huku nje watu wao wanajua walikua na viongozi wanaopigania maslahi ya chama na wananchi kumbe watu wana malengo yao binafsi🤣🤣🤣🤣.
Mnaotegemea upinzani huu wa akina mwalimu poleni sana , 🤣🤣🤣🤣
 
Sasa hata wakigombea katika UCHAGUZI huu, si watafanyiwa mizengwe Kwa Sheria iliyopo ya UCHAGUZI? Je wapiga kura si ni watu waelewa TU. Wahame vyama vingine ili wajaze matumbo yenye njaa. Siasa zao si hasa. Tumewapata.
 
Back
Top Bottom