Tigo mnajali wateja, hizi bando si mchezo

Tigo mnajali wateja, hizi bando si mchezo

Zamani kwa Tsh. 500 nilikuwa napata 70MB. Lakini sasa leo nimeamka nimekuta haya maajabu kwenye menu ya Tigo

Tsh 500: 300MB
Tsh 1000: 750MB
Tsh 2000: 3GB

Tafadhali sana Tigo, hata kama kuna technical issue imesababisha tuone hizo bando motomoto, msibadili, wacha wateja tufaidi. Shikilieni hapo hapo.

Kusema ukweli nilikuwa nimeshaamua kujiunga na mtandao wa Taifa lakini kwa bando hizi, 500 yangu kwa siku mtaendelea kuipata.

Ila fanyeni kwamba MB zikibaki, ninaponunua kifurushi kingine nizipate ila muda unapokuwa umeisha nisiweze kuzitumia hadi ninunue kingine.

Tabutupu
Dodoma,

View attachment 1358100

Sent using Jamii Forums mobile app

Wanawawekeni sawa Kwanza huku wakijua kabisa ni wapi na lini watajilpa kupitia Furaha yenu ya leo ya kupenda Unafuu huu.
 
Umechanganya madesa!!! Achana na hayo mahesabu ya kugawanya na kuzidisha na turudi kwenye kujumlisha!

Sh 5000 = 7GB
Sh 5000 + sh 5000 = Sh. 10,000
7GB + 7GB = 14 GB

Kwa maana nyingine, kwa Jirani Sh 10,000 = napata 14GB wakati kwa Baba TTCL napata 10 GB!!! Ulitakiwa kufanya 10/14 na sio 14/10!!!
Kwa maneno yako mwenyewe ulisema, "TTCL nimewapiga chini na bundle yao ya TZS 10K for 10GB kwa wiki, na nimehamia Halotel ambako ni Sh 5000 for 7GB kwa wiki!"

Tukirudi kwenye kujumlisha,

Sh 10,000 = 10GB
Sh 10,000 + Sh 10,000 = 20,000
10GB + 10GB = 20GB

Kumbuka: Sh 5000 for 7GB kwa wiki!"
 
Attachments

  • 2307796_Screenshot_20200215-140003.jpg
    2307796_Screenshot_20200215-140003.jpg
    16.4 KB · Views: 14
Kama mambo yenyewe ndo haya, basi msiotumia Airtel mnatakiwa mkapimwe akili!! Halafu kumbe ndo maana siku hizi najidai sana, manake laini kwa ajili ya kuongea natumia Airtel TU; uwe Tigo, Voda, hata wapi sijui, mi nakutwangia tu kama sina akili mzuri! Laini yangu ya Tigo washaifungia, na wala sijali manake wala sikumbuki niliitumia lini mara ya mwisho!! Ya Voda hadi nikaisahau, siku naikumbuka nakuta washampa mtu mwingine! Laini pekee ambazo nilihangaika kwenda kuzisajiri ni Halotel, TTCL na Zantel kwa sababu tu speed zao za Internet kwangu ndo best kuliko wengine!
 
Kwa maneno yako mwenyewe ulisema, "TTCL nimewapiga chini na bundle yao ya TZS 10K for 10GB kwa wiki, na nimehamia Halotel ambako ni Sh 5000 for 7GB kwa wiki!"

Tukirudi kwenye kujumlisha,

Sh 10,000 = 10GB
Sh 10,000 + Sh 10,000 = 20,000
10GB + 10GB = 20GB

Kumbuka: Sh 5000 for 7GB kwa wiki!"
Sawa 5000 for 7GB kwa wiki, sasa kwani hiyo 10K for 10GB ni kwa muda gani?! Na kwa kuangalia hiyo screenshot uliyoweka, labda ni offer kwa segment fulani lakini kwangu 10K = 10GB per week
 
Kama mambo yenyewe ndo haya, basi msiotumia Airtel mnatakiwa mkapimwe akili!! Halafu kumbe ndo maana siku hizi najidai sana, manake laini kwa ajili ya kuongea natumia Airtel TU; uwe Tigo, Voda, hata wapi sijui, mi nakutwangia tu kama sina akili mzuri! Laini yangu ya Tigo washaifungia, na wala sijali manake wala sikumbuki niliitumia lini mara ya mwisho!! Ya Voda hadi nikaisahau, siku naikumbuka nakuta washampa mtu mwingine! Laini pekee ambazo nilihangaika kwenda kuzisajiri ni Halotel, TTCL na Zantel kwa sababu tu speed zao za Internet kwangu ndo best kuliko wengine!
Hivi kwa nini wanagawaga namba za watu? Yani laini hujaitumia kidoogo tu, wanaagawa?!?!! Inakuwaje hii? Hatuwezi kuwashtaki!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona bado wamekaza huko tigo sirudi tena,

Cheki mambo ya halotel haya,
500=Mb 500 siku
1000=GB 1 wiki
2000=GB 2 wiki
5000=GB 7 wiki

Ni mwendo wa kuteleza tu na halotel.
 
Mkuu rudi nyumbani, huko ulipo unaibiwa au unajiibia. 10k kwa 10GB ni sawa na 1k kwa 1GB lakini 5k kwa 7GB ni sawa na 1.4k kwa 1GB. Simple math!! .
Ni sawa nani anatoa ofa kama hiyo sasa watu wanakenua meno 500 Tshsb 300 ???
 
I always go where it's worth for my hardly earned money! Kwa sasa TTCL nimewapiga chini na bundle yao ya TZS 10K for 10GB kwa wiki, na nimehamia Halotel ambako ni Sh 5000 for 7GB kwa wiki! Kwa maana nyingine, hivi sasa Sh. 10K napata 14GB kwa wiki!

Samahani BabaTTCL, nimelazimika kutoroka nyumbani manake kwa jirani kumenoga zaidi!

Halotel wanatoa mb nyingi lakini masharti yao magumu mno,,hapo ndipo wanakera,,

MB 500 kwa Sh 500 saa 24,,hawana dakika wala sms
GB 1 kwa Sh 1000 siku 7,,hawana dakika wala sms
GB 7 kwa Sh 5000 siku 7,,hawana dakika wala sms
GB15 kwa Sh 5000 siku 30,,hawana dakika wala sms,,MB500 za day na 14500 za usiku,, zikiisha 500 usubiri za usiku 😁😁 shenzi kabisa
 
Inategemea menu. Halotel option nyingi
 
Back
Top Bottom